Tutamkumbuka mwendazake

pilipili hoho

Member
Jun 15, 2015
86
23
KILA NISOMAPO HOTUBA HII, NA HALI YA LIBYA ILIVYO SASA MACHOZI YANANITOKA.

PUMZIKA WA AMANI MKOMBOZI,MZALENDO.

"Kwa jina la Mwenyezi Mungu (Allah), Mungu mpaji, na mwenye rehema....
Kwa miaka takribani 40 ama ilikuwa zaidi sikumbuki. Nachokumbuka ni kuwa nilifanya kila nilichoweza kuwapa watu wangu nyumba, hospitali na shule. Na kila walipohisi njaa niliwapa chakula. Niliifanya Benghazi kutoka jangwa kuwa ardhi nzuri ya kilimo.
Nilisimama imara dhidi ya Ronald Regan (Rais wa zamani wa Marekani), alipomuua binti yangu niliyemuasili. Alikua anajaribu kuniua mimi lakini akamuua yule binti yatima masikini. Niliwasaidia kaka na dada zangu waafrika fedha kupitia AU.
Nilifanya kila nililoweza kuwafanya watu wangu waelewe maana halisi ya demokrasia; ambapo watu wa tabaka la chini niliwapa madaraka.
Lakini hawakuridhika. Hata aliyekuwa na nyumba ya vyumba kumi, nguo mpya, na fanicha nzuri, hakuridhika. Alihitaji zaidi.
Kwa jinsi walivyokuwa wabinafsi walihitaji zaidi. Hivyo wakawaambia Marekani kuwa wanataka "demokrasia" na "uhuru". Hawakujua kuwa "demokrasia" waliyoitaka ilikua ni mfumo wa unyonyaji ambapo mbwa mwenye nguvu zaidi huwala mbwa wadogo.
Walikua hawasikii wala hawaoni. Walitaka "demokrasia". Wakasahau kuwa hata Marekani hakukuwa na huduma za afya za bure, dawa bure, elimu bure na chakula cha bure. (Huduma hizi za bure zilipatikana Libya tu).
Nchini Marekani mtu masikini/fukara hana cha bure. Labda awe ombaomba au avuje jasho kuhemea.
Haikujalisha nilifanya kwa kiasi gani bado hawakuridhika. Lakini wapo waliojua mimi ni mtoto wa Gamal Abdel Nasser, mwarabu pekee halisi na kiongozi wa kiislamu tuliyewahi kuwa nae tangu enzi za Salah-al-Deen.
Wakati Nasser anapigania mfereji wa Suez kwa watu wake nami nilikua naipigania Libya kwa watu wangu. Nilikua najaribu kufuata nyayo zake ili kuwaweka watu wangu huru kutoka kwenye makucha ya wakoloni wanaotuibia.
Lakini kwa sasa niko mateka katikati ya majeshi makubwa ya dunia katika historia. Mwanangu mpendwa mwenye asili ya Afrika, Obama anataka kuniua.
Ili achukue uhuru wetu, achukue haki yetu ya huduma za bure za afya, huduma za bure za elimu, na chakula chetu; na kutuletea mfumo mpya wa kimarekani wa kuiba uitwao "Ubepari"
Lakini wote katika dunia ya tatu tunajua maana yake. Maana yake ni kuwa "washirika" wanatawala mataifa, wanatawala dunia, na watu wanaishia kuteseka.
Kwa hiyo hakuna mbadala kwangu. Lazima niwe na msimamo. Na kama Mungu atapenda nitakufa kwa mapenzi yake.
Mapenzi yake yaliyofanya nchi yetu kuwa na ardhi yenye rutuba, chakula bora, na huduma bora za afya. Mapenzi ya Allah yaliyowezesha tukawasaidia kaka na dada zetu waafrika na waarabu waliokuwa na shida.
Sipendi kufa; lakini kama nitakufa ili kuiokoa ardhi hii, kuokoa watu wangu, na wengine ambao ni kama wanangu; acha nife.!
Acha sauti hii iwe agano langu kwa dunia kuwa nilisimama kupinga uvamizi wa NATO. Nilisimama kishujaa kupinga usaliti wa nchi za magharibi na nia mbaya za kikoloni. Na hapa nimesimama na ndugu zangu waafrika, kaka na dada zangu waislamu kama ngao yangu ya matumaini.
Wakati wengine walipokuwa wanajenga majumba ya kifahari, mimi niliishi kwenye nyumba ya kawaida na kwenye mahema. Siwezi kusahau maisha yangu ya utoto kule Sirte.
Sikutapanya rasilimali za nchi yangu kipumbavu. Na kama alivyokua Salah-al-Deen, kiongozi wetu katika uislamu, nilichukua kidogo sana kwa ajili yangu, na sehemu kubwa niliwapa wananchi.
Watu wa magharibi wameniita "kichaa", "mwendawazimu" lakini wanajua ukweli kuwa mimi si kichaa wala mwendawazimu; ila waache waendelee kudanganya. Wanajua hii ardhi ni huru na haipo kwenye himaya ya kikoloni. Huu ndio msimamo wangu na dira yangu na imekuwa wazi kwa watu wangu.
Nitapambana hadi pumzi yangu ya mwisho ili watu wangu wawe huru. Mwenyezi Mungu atusaidie tubaki waaminifu na tuwe huru."

Mu'uammar Qaddafi.
 
Hatatokea kiongozi imara, shupavu na mzalendo katika Afrika kama Muammar al-Gaddaf.
Walibya sasa wanaishia bahari ya Mediteranean kwa kukosa amani na huduma za bure kama za enzi ya Gaddaf.
d46ef7732b64e033771e8c1ba05fe590.jpg
 
Hatatokea kiongozi imara, shupavu na mzalendo katika Afrika kama Muammar al-Gaddaf.
Walibya sasa wanaishia kufia bahari ya Mediteranean kwa kukosa amani na huduma za bure kama za enzi ya Gaddaf.
d46ef7732b64e033771e8c1ba05fe590.jpg
 
Hotuba hiyo nimya kishujaa sana. Tangia niipate nimeifanyia lamination vizuri na nimeitunza vyema. Kuna sehemu inanisikitisha sana hasa kuhusu viongozi wa Afrika. Muamar Gadaffi anasema amesimama na waafrika kama ngao yake ya matumaini lakini viongozi wanafiq wa Afrika ambao walikuwa wakimshangilia na kuchukua misaada toka kwake wakinyamaza kimya wakati Libya inasambaratishwa.
 
Of course Muamar Gadaffi alijitahidi sana tu na kwa nia ya dhati kwamba Africa iwe na mamlaka yake na sauti ya kujiamlia, kwamba Africa iondokane na utegemezi wa magharibi ambao kwakweli ni wakinyonyaji ma wala hauna na hautakuwa na nia njema ya kuiona Africa inakua na kujitegemea kiuchumi.

Lakini kosa au udhaifu wa Gadaff ilikuwa pale tu badala ya kushughulikia uchumi namaendeleo ya Africa kwa waafrica wote, Gadaffi alijikita zaidi kidini. Kwa Gadaffi ni uislam tu ndo dini ya kufaa waafrica wanapaswa kuwanayo akasahau kuwa waafrica kama walivyo watu wengine dunia wanatofautiana ki-imani na wala haiwezekani na haitawezekana kuwafanya waafrica wote wawe wa dini moja kwakuwa maswala ya imani ni mtu binafsi na siyo mambo ya kulazimishwa.

Kwa kuzingatia alivyofanikiwa na utajiri mwingi mno; Muamar Gadaffi alikuwa tayari ameshaanza kupenyeza utajiri wake kwenye mabenki na makampuni yaliyoko barani kote Africa kwa sharti la kuendeshwa kwa shariah za kiislam. Na kwa kutumia umasikini wa nchi nyingi za kia-Africa hayati Gadaffi alikuwa tayari ameshafanikiwa kuwashawishi baadhi ya Maraisi na viongozi wengi kwamba angetoa misaada ya mamilioni ya dola bila riba lakini kwa shariti ya kwamba uislam uwe kipaumbele kwenye hizo nchi.

Nchi za Magharibi zilipojilizisha uwa Gadaffi anautajiri wa kutosha kuwanunua maraisi na viongozi wengi Africa ili mradi wakubali kuupeleka mbele uislam na ikiwezekana shariah za kiislam zianze kuingizwa kwenye katiba za nchi, hapo ndo kivumbi kilianza lengo likiwa ni kumuua kabisa Gadaffi la sivyo aachie uongozi wa Lybia, kwakuachia madaraka ingemaanisha kuwa hata utajiri wake usingeendelea kunawili na hivyo mpango wake ungeshindwa.

Mbali na hilo, nchi za magharibi zilitumia pia mwanya huu kujinufaisha kwa mafuta ya Lybia kupitia makampuni yao ambayo kwa uhai wa Gadaffi yalikuwa yakilipa kodi kubwa serikalini hivyo kuyafanya yapate faida kidogo. Baada ya Gadaffi kufa, magharibi sasa imeelekeza mirija yake Lybia na inanyonya mafuta bure kabisa. Ni huzuni na fedheha kwetu waafrica tunaopenda kuiona Africa ikijitegemea na kujinasua na uporaji wa magharibi, lakini pia hatupendi na hatutaunga mkono kiongozi yoyote mwenye kujaribu kuigawa au kuiparaganisha Africa yetu kwa kutumia mgongo wa dini yake kwani kufanya hivyo ni hatari mno kuliko hata unyonyaji wa kimagharibi. MUNGU ibariki Tanzania; MUNGU ibariki Africa.
 
Back
Top Bottom