UNYAMA: Mtanzania asimulia unyama waliyofanyiwa Msumbiji

Nucky Thompson

JF-Expert Member
Sep 20, 2016
1,817
4,058

msumbiji.jpg

Watanzania waishio nchini Msumbiji wapo katika wakati mgumu kutokana na kufukuzwa kwa nguvu ikiwemo kunyang'anywa mali zao, kupigwa na wanawake kubakwa. Msikilize Mtanzania huyu aitwaye Wille Katulunga anayeishi mkoa wa Cabo Delgado akielezea kupitia Planet FM ya Morogoro kuhusu sakata hilo

KUHUSU YANAYOTOKEA MSUMBIJI

Ni vema sasa serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ikachukua hatua dhidi ya mauaji,utesaji,unyanyasaji,ufilisiwaji unaofanywa kwa Watanzania waishio Msumbiji!

Watanzania wananyang'anywa mali zao na askari wa Msumbiji,wanapigwa,wananyanyaswa,wanabakwa na kulawitiwa bila hatia yoyote!

Kuna vizuizi vikubwa vya kibiashara vimewekwa Msumbiji kukandamiza Watanzania ilihali wao wanafanya shughuli zao vizuri Tanzania bila kubugudhiwa

Hakuna ujirani mwema kati ya Tanzania na Msumbiji,wema ni sisi tu,wao wanatushambulia utadhani sisi ni magaidi!

Ni vema serikali yetu iweke mazingira magumu kwa watu wa Msumbiji ili kila mtu afanye kazi katika eneo lake!

Njia za kidiplomasia zimetumika mara nyingi lakini hazijaleta matunda yoyote!

Msumbiji haina utawala wa sheria inaongozwa ovyo!

Ni vema serikali ikalichukulia hatua kali suala hili!
 
Kisa chenyewe ni hivii?
Kuna mzungu anaitwa Franco,huyu Franco alikuwa anakaa Tanzania Lindi & Mtwara alimiliki maeneo makubwa.
Sasa TZ wakamtimua,akakimbilia Mozambiki,huko mozambki,akapewa eneo kubwa sana,sasa ndani ya eneo hilo kuna madini,kama tulivyo wabongo tukajiongeza kuchimba na kutafuta riziki.
Huku na kule Francoo kastuka hawa si wabongo hawa?...Kwa sasa malori yake ndiyo yanafanya kazi ya kuwasomba toka Msumbiji hadi mpakani.
 
Kisa chenyewe ni hivii?
Kuna mzungu anaitwa Franco,huyu Franco alikuwa anakaa Tanzania Lindi & Mtwara alimiliki maeneo makubwa.
Sasa TZ wakamtimua,akakimbilia Mozambiki,huko mozambki,akapewa eneo kubwa sana,sasa ndani ya eneo hilo kuna madini,kama tulivyo wabongo tukajiongeza kuchimba na kutafuta riziki.
Huku na kule Francoo kastuka hawa si wabongo hawa?...Kwa sasa maloro yake ndiyo yanafanya kasi ya kuwasomba toka Msumbiji hadi mpakani.
Nini hiyo mkuu?
 
Watanzania wapo wengi sana (makumi kwa maelfu) Msumbiji wanaingia bila vibali kuchimba madini na kuvuna mbao kupitia daraja la Mtambaswala na kingo za mto Ruvuma. Hakuna haja ya kulialia tuwaelimishe watu wetu wawe na vibali muhimu.
Unachoongea ni sahihi, ila askari wa kule mda wote ni kama wapo vitani.... Yaani kule bunduki nje nje.

Hawajui kufuata sheria kabisa..... Yaani wao kuja kwenye biashara yako na kuchukua bidhaa yoyote kibabe ni kawaida.....
 
Hivi JF tuanaushawishi wowote kwenye hii serikali, maana mara nyingi huwa naona kimyatu, let say hili sakata la ndugu zetu huko msumbiji serikali siwatusikie waanze nawao kuwatimua wakwao.
Sipendi ujinga kabisa linapokuja suala la utaifa.
 
[QUOTE="idawa
Hawajui kufuata sheria kabisa..... Yaani wao kuja kwenye biashara yako na kuchukua bidhaa yoyote kibabe ni kawaida.....[/QUOTE]

Sheria wanawajua, sema hawafati sheria kwa kujua waTz wanaishi mle (kinyemela ) kwa kuvunja sharia za uhamiaji na kwa hiyo huwezi kuripoti polisi kuwa umeonewa.

Hata hapa Tz ukifanya uhalifu wa kwa kuvunja sheria ya usalama barabarani, askari trafic akachukua Tsh 10,000 ("ya kiwi ") akatia mfukoni badala ya kukutoza faini Sh 30,000 sio kuwa hujui sheria. Ukweli unabaki kuwa una makosa mawili
1.Umevunja sheria ya usalama barabarani.
2.Umetoa rushwa, polisi naye amepokea rushwa.
Jambo moja ni dhahiri kwamba ukiwa msafi kwa maana ya kufuata sheria huwezi kumhofia askari.
 
jino kwa jino tu hapa tuanze msako wa kuwakamata wa mozambique tulipize kisasi hakuna namna tena

Mkuki kwa nguruwe kwa binadamu mchungu?
Wakenya waliwahi kufanya haya Tanzania ikajibu mapigo.
Kuhusu wahamiaji haramu wa Rwanda na Burundi yaliyowakuta sio yale yale ya msiba kwa jirani?
 
[QUOTE="idawa
Hawajui kufuata sheria kabisa..... Yaani wao kuja kwenye biashara yako na kuchukua bidhaa yoyote kibabe ni kawaida.....

Sheria wanawajua, sema hawafati sheria kwa kujua waTz wanaishi mle (kinyemela ) kwa kuvunja sharia za uhamiaji na kwa hiyo huwezi kuripoti polisi kuwa umeonewa.

Hata hapa Tz ukifanya uhalifu wa kwa kuvunja sheria ya usalama barabarani, askari trafic akachukua Tsh 10,000 ("ya kiwi ") akatia mfukoni badala ya kukutoza faini Sh 30,000 sio kuwa hujui sheria. Ukweli unabaki kuwa una makosa mawili
1.Umevunja sheria ya usalama barabarani.
2.Umetoa rushwa, polisi naye amepokea rushwa.
Jambo moja ni dhahiri kwamba ukiwa msafi kwa maana ya kufuata sheria huwezi kumhofia askari.[/QUOTE]
Balozi fanha mpango hao watu waludishwe kwa usalama, inaumiza sana.
 
Serikali itume ndege kuokoa rasmali watu yetu mapema tutapoteza ndugu zetu wakati huo ikiangalia chanzo cha kufukuzwa na kuchukua hatua stahiki.
 
KUHUSU YANAYOTOKEA MSUMBIJI

Ni vema sasa serikali ya Jamhuri ya muungano wa Tanzania ikachukua hatua dhidi ya mauaji,utesaji,unyanyasaji,ufilisiwaji unaofanywa kwa Watanzania waishio Msumbiji!

Watanzania wananyang'anywa mali zao na askari wa Msumbiji,wanapigwa,wananyanyaswa,wanabakwa na kulawitiwa bila hatia yoyote!

Kuna vizuizi vikubwa vya kibiashara vimewekwa Msumbiji kukandamiza Watanzania ilihali wao wanafanya shughuli zao vizuri Tanzania bila kubugudhiwa

Hakuna ujirani mwema kati ya Tanzania na Msumbiji,wema ni sisi tu,wao wanatushambulia utadhani sisi ni magaidi!

Ni vema serikali yetu iweke mazingira magumu kwa watu wa Msumbiji ili kila mtu afanye kazi katika eneo lake!

Njia za kidiplomasia zimetumika mara nyingi lakini hazijaleta matunda yoyote!

Msumbiji haina utawala wa sheria inaongozwa ovyo!

Ni vema serikali ikalichukulia hatua kali suala hili!
 
Attachments

  • msumbiji.jpg
    msumbiji.jpg
    19.5 KB · Views: 277
And Yet Waziri wa mambo ya nje yupo kimya..

Na ikitokea kaonge atajifanya mkarimu..
 
Back
Top Bottom