Tutalalamika mpaka lini? Tunataka nini?

Saguda47

JF-Expert Member
May 1, 2016
11,137
19,882
Ndugu zangu, hasa watanzania wenzangu, naamini tu salama ingawa kuna shida za hapa na pale!!

Mwanadam ni kiumbe asiyetosheka wala kuridhika kwa chochote kile anachotendewa au kufanyiwa, kwa maelfu ya miaka iliyopita kumekuwa na migongano ya fikra na matarajio kati ya watawala na watawaliwa.
Hali hii imekuwa ndio nishati kubwa ya kimsukumo katika vizazi na vizazi vya binadam vikipambana kuleta kinachoitwa MABADILIKO(Changes), hali hii ilisababisha kuibuka kwa kile kinachoitwa DEMOKRASIA,

Sisi kama taifa la Tanzania ni nchi huru kisiasa, kijamii na kiuchumi tuna nguvu ya maamuzi katika nyanja zote,
Mpaka tukipo sasa taifa letu lina umri wa miaka 56 ama nusu karne, Taifa hili lina awamu zipatazo 5 na marais 4 waliostaafu na 1 aliyeko madarakani.

Je, makundi yanayovaa majoho ya RAIA wa Tanzania yana nia gani katika taifa hili? je ni aina gani ya mtanzania anyetakiwa kutuongoza na kukidhi kiu za hawa waliovaa majoho ya utanzania?
je, matatizo yetu binafsi yatamalizwa na serikali ( viongozi)?
La hasha!! tusikwepe wajibu wetu wa kikatiba wa kufanya kazi za kutuingizia kipato kwa kutumia mbinu za kujilinda ( defence mechanism) ijulikanayo kama projection,

projection ni namna ambapo mtu anakwepa lawama inayomhusu na kuielekeza kwa mwingine,

we are complaining of what we are responsible for!!

we must not think that much of our problems will one day be solved by choosing a bright leader, the power of transformation and changes is within our ideologies and our routine actions!!
its neither Jesus nor Muhammad s.a.w who will probably create a clear Tanzania while tanzanians are slumbering!!
God bless Tanzania, God bless our president John pombe magufuli!!
 
Back
Top Bottom