Tutakukumbuka sana Dr.Slaa

juvenile davis

JF-Expert Member
Apr 13, 2015
4,752
4,463
Ilikuwa nitarehe 1.9.2015 mida ya mchana fulani hivi akili yangu ilikosa nguvu sana baada ya kumsikia na kumuona Dr. Slaa ambaye alkuwa ni katibu mkuu wangu wa chama akitamka live kwamba ameachana na siasa.

Alitoa sababu ambazo kwa wajanja ambao tunajua sayansi ya siasa tulimuelewa sana,ila kwa wale mabingwa wa mihemko na siasa za fuata mikumbo hawatakaa wamuelewe hata siku moja.

Kiukweli huyu mzee kanifunza kitu,kwamba mwanaume wa kweli usikubali kufa kizembe,bali ufe kishujaa.Hakuwa tayari kudhalilika kwa sababu ya kumpa furaha mwenyekiti.

Mzee aligoma kabisa,kanifunza ya kwamba kama mwenzako kakukera au kakosea ni afadhari umwambie ungali bado upo hai na yeye angali hai ili ajue ya kwamba alibugi,usimuogope lafiki yako akikosea kitu,we mwambie tu live wala usiogope.

Mzee hakuwa tayari kuyarudia matapishi yake eti kisa Mbowe afurahi,mzee alionesha ya kwamba yeye sio wa kushikiwa akili na mwenyekiti,mzee alionesha wazi kwamba siasa za kinafiki kwake haziwezekani kamwe,haiwezekani useme "mwanamke huyu ni muathirikia na ni malaya siwezi hata kuongozana nae" harafu kesho na kesho kutwa watu wanakuona unamnadi kwa malafiki zako kwa mema na mazuri eti kisa tu wazazi wako wamekwambia wanamtaka.

Mzee kanipa funzo kubwa maishani na nitamkumbuka sana hadi kifo changu,ni mwanasiasa pekee kwa hapa Tanzania ambaye hana unafiki kamwe.

Chama kimepoteza mvuto,nawaonea huruma wabunge na madiwani mana 2020 tutawapoteza wengi sana kwa sababu ya tamaaa ya mwenyekiti tu.

Angalia hata katiba ya chama tumeshindwa kuifuata mana huu ni mwezi wa 6 tumeshindwa kumpata wa kuvaa viatu vya Dr slaa,na usishangae atakaekuja akawa ni genge la Lowassa alilokuja nalo baada tu ya kukatwa jina CCM(tamaaa ya madaraka).

Jamani naomba mwenye namba ya Dr. Slaa anisaidie niweze kuongea nae huyu mtu ambae kaonesha kwamba huwa hayumbishwi na misimamo yake.

Popote ulipo Dr. Slaa naomba namba zako tuwasiliane,kilala heri chama changu CHADEMA kwa kumtafuta katibu mkuu,ila hatutampata kama Dr. Slaa maana chama kinayumba na kupoteza mvuto,wanaofukuzwa CCM na kukatwa huku kwetu imekuwa ndio kimbilio lao sasa,yani wala rushwa na mafisadi ambao wanakataliwa na CCM sisi huku tunawaona ni almasi mwisho tunawapa madaraka,kazi ipo sana.
 
I agree with you 80%.
Hope Mh.Mbowe atafanya masahihisho kwa kukipatia chama mtu bora,bora pengine hata Dr.Slaa.
Alituumiza wengi ila hatupaswi kukisusia chama,tunakisaidia ili kipate mvuto mpya.
 
Walioibiwa wake na Daktari Slaa wakisoma uzi huu watamkumbuka zaidi, lakini wapenda mabadiliko na siasa za kusameheana na kukubaliana na hitaji la wakati watampuuza sana maana hata angegombea yeye sidhani kama angefikisha hata kura milioni tatu ukiacha sita na ushee za Edo.
Siamini kama msimamo wa kubagua watu kujiunga na CHADEMA ni msimamo bora zaidi kuliko msimamo wa kubaki mseja na kuendelea kulitumikia Kanisa Katoriki kwa uaminifu.
:eek::eek::eek:
 
Ni kweli wakati mwingine tusibishane na ukweli na hali halisi hasa ukizingatia Dr.Slaa alianza na chama tangu kichanga kwa hiyo anakifahamu vizuri.

Kitu cha msingi nikuboresha na kuweka sera madhubuti zenye mtazamo na matumaini mapya.
 
Anakufa binadamu sembuse MTU kukihama chama?
Songa mbele yaliyopita yamepita komaa[/
QUOTE]

Imeongea point misimamo mingine haifai kwasababu. Suala la ufisadi ni janga la Taifa kwa sasa hv hata mtumbua majipu naye anamajipu yake.

Muhimu ni kuja na mfumo mpaya utakaowaweka watanzania kwenye mstari.
 
Kuna watu wanajfanya wao no chadema kumbe ni Ccm wakilalamika eti chadema 2015 ilipoteza Na 2020 itapoteaaaa kabisa !!!
Hiyo ni hofu tuu ccm ya kungolewa !!
 
mwanaume wa kweli? wakati alifungwa kamba shingoni na huyo 'mke' wake na kuburuzwa? mwanaume wa kweli hatoroki mapambano na kwenda kujificha ughaibuni. ametoroka aibu asishuhudie chama kilivyojizolea wabunge na madiwani wengi na kuongoza halmashauri za majiji kuliko wakati wa uongozi wake.hatutaki kamanda anayeongozwa kwa amri za kitandani.
 
mwanaume wa kweli? wakati alifungwa kamba shingoni na huyo 'mke' wake na kuburuzwa? mwanaume wa kweli hatoroki mapambano na kwenda kujificha ughaibuni. ametoroka aibu asishuhudie chama kilivyojizolea wabunge na madiwani wengi na kuongoza halmashauri za majiji kuliko wakati wa uongozi wake.hatutaki kamanda anayeongozwa kwa amri za kitandani.

Misingi na uimarishaji wa chama alioweka Dr Slaa ndiyo umewezesha chadema kupata madiwani na wabunge wengi. Hata angegombea urais angeshinda CCM. Tuwe wakweli tu.
 
Back
Top Bottom