Tutakosa wanasiasa na wagombea

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,071
2,000
Nchi hii ina mambo mengi yasiyojulikana kuliko yanayojulikana. Hasa mambo yahusuyo mahusiano kati ya mwanasiasa mmoja na mwingine. Wanasiasa wana nyumba ndogo,za kati na kubwa. Wenyewe kwa wenyewe; wenyewe na wengine. Kama kila kitu kinachowahusu kitaanikwa (tupo tayari kuleta picha,video na sauti kama Mamlaka husika zitaridhia) basi hali ya Taifa itadhoofu.Kwakuwa tutakosa wanasiasa na wagombea.

Leo, kuna mijadala hapa kuhusu Viongozi fulanifulani kutoka pamoja. Sioni tatizo liko wapi. Mosi, mambo hayo ya kikubwa ni ya kawaida sana hapa Tanzania kama nilivyotangulia kusema. Pili, mambo yao wameyafanya sirini kama tulivyozoea. Na tatu, wote ni wakubwa kiuongozi;hakuna wa kumpelekesha mwenzake.Walikubaliana.

Labda, suala liwe ni kweli au si kweli kuwa walitumia fedha za umma kufanya yao. Hapo tu ndiyo penye hoja. Kinyume na hapo, ni majungu tu. Watanzania wenzangu, pale Bungeni kuna sarakasi za kila aina-hata za kimapenzi. apo wanaoporana;wanaopigana vibuti; wanaoombana mahusiano kila kukicha na kadhalika na kadhalika. Yote yapo pale. Ruhusa ikitoka, wengi kama si wote watatajwa na kujadiliwa. Htutabaki na mwanasiasa wala mgombea.

Cha kufanya ni kujadili mambo yenye maslahi kwa Taifa. Tunayo mengi tu. Ya ndani ya Ilani ya CCM yetu na yatokanayo na ahadi zilizotolewa na Wabunge na Madiwani wetu. Muda unaishia hivyo. Mwakani tutaanza na uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Siasa ni hoja.Siasa si kashfa. Hoja ikinyamaziwa hugeuka kuwa kashfa. Ikifikia hapo,mwanasiasa hukosekana. Cha kufanya,ni kujibu kila hoja inayoelekezwa kwa mwanasiasa yoyote.Vizuri zaidi akaijibu mwenyewe aliyetupiwa hoja hiyo. Hoja kwa hoja;swali kwa jibu. Basi.

Watanzania wenzangu, tunayoyajua tu yanatusumbua.Tunajua kuwa huduma za afya zimedorora;elimu inazidi kuporomoka kila mwaka;barabara nyingi ni mbovu;rushwa inatahayari kwelikweli;Polisi wanapambana na wananchi mara kwa mara;wakubwa wa nchi hawagusiki kirahisi; lishe ya mtanzania ni songombingo na mengineyo. Ya chumbani yatatuhusu nini sisi?

Yakiwekwa yote au mengi kuwahusu viongozi wetu hadharani, tutakosa wanasiasa na wagombea.Nani atatuongoza? Turudi kwenye hoja za kitaifa.


Mzee Tupatupa wa Lumumba,Dar es Salaam
 

m4cjb

JF-Expert Member
Jul 23, 2012
7,374
2,000
MBOWE ATHUMAN KAPUYA FREEMAN SLAA ( Wote hawa wamesaliti ndoa zao, wanatakiwa kufungwa jiwe shingoni na kutoswa majini)

Hivi unaweza kufananisha kubaka na kuwa na nyumba ndogo? tukikufatilia kwa undani hata wewe unaweza kuwa mtoto wa nyumba ndogo.Pia una ushahidi na hayo? kapuya ushahidi wa mlalamikaji upo wazi.Madhara ya kufikiri kwa tumbo yanakupoteza bwana mdogo
 

m4cjb

JF-Expert Member
Jul 23, 2012
7,374
2,000
MBOWE ATHUMAN KAPUYA FREEMAN SLAA ( Wote hawa wamesaliti ndoa zao, wanatakiwa kufungwa jiwe shingoni na kutoswa majini)

unataka kusema anayetoka na vick kamata naye atoswe majini? na mama yake riz 1 ndiye huyu salma? vp kuhusu babu seya? pambafuu....
 

MTAZAMO

JF-Expert Member
Feb 8, 2011
16,050
2,000
Nimejaribu kusoma karibia kila comment kwenye ile thread hasa baada ya kuipuuza mwanzoni na baadae kuona imefika michango zaidi ya 800 nikadhani lipo jambo lakini zimejaa porojo ambazo hazisaidii taifa.

Sijui tumekuwa watu wa namna gani! zamani ilikuwa ukiona thread ina watu wengi ujue kuna nondo za uhakika lakini sasa tunatia aibu tu.
 

Abdillahjr

JF-Expert Member
Oct 3, 2011
694
0
Laiti wake za mkulu na wakuu wa wilaya vimada vingewekwa wazi ukiacha wale wanaoenda nje kwenye misafara ya wakuu basi mfalme mswati angekuwa anaonewa!!
 

Chris Lukosi

Verified Member
Aug 23, 2012
4,584
2,000
Umeongea ukweli lakini Mbowe kakosea kutumia cheo chake kuvunjia amri ya sita

Sote tunajua hiyo amri inavunjwaga kikubwa lakini jamaa anavunja kizamani sana
 

manucho

JF-Expert Member
Apr 20, 2012
3,405
1,195
Nimejaribu kusoma karibia kila comment kwenye ile thread hasa baada ya kuipuuza mwanzoni na baadae kuona imefika michango zaidi ya 800 nikadhani lipo jambo lakini zimejaa porojo ambazo hazisaidii taifa.

Sijui tumekuwa watu wa namna gani! zamani ilikuwa ukiona thread ina watu wengi ujue kuna nondo za uhakika lakini sasa tunatia aibu tu.

Hoja za @mwigulunchemba, Taswira utaifakwanza FaizaFoxy lumumba team buku7 hamna kitu, ndicho walichoambiwa na kina Lowassa, JK, Wassira, Werema na Lukuvi.
Hakuna kazi nyingine wanayofanya zaidi ya ujinga huu
 
Last edited by a moderator:

OKW BOBAN SUNZU

JF-Expert Member
Aug 24, 2011
31,437
2,000
Nakumbuka Makamba alitaka kuleta propaganda kama hizi 2010 dhidi ya Dr.Slaa,tukamtuliza.mnajua kabisa sisi ni wehu zaidi yenu
 

Dr.Mo

JF-Expert Member
Mar 28, 2012
3,810
1,225
ni kweli kabisa hayo mambo kwa mwanaume wa kiafrika ni kwaida.....labda uwe mkameruni.....tujadili mambo yenye tija kwa taifa....tuache siasa za kitoto kama hizi.....huwezi ukaka bungeni kuanza kujadili mambo ya wtu kukamua mademu zao,.....kwani ni nani akamui bana
 

Ndikwega

JF-Expert Member
Feb 1, 2012
5,870
2,000
Nakumbuka Makamba alitaka kuleta propaganda kama hizi 2010 dhidi ya Dr.Slaa,tukamtuliza.mnajua kabisa sisi ni wehu zaidi yenu

Ni kweli mkuu,nimekumbuka,kumbe MAKAMBA alimtia mimba binti wa shule na ikamlazimu kuacha shule huyo binti. Siasa raha sana. Hivi huyo mtoto wa Makamba ndiyo huyo February au huyo wa kike maana sijui yupi mkubwa kati yao?
 

capo

JF-Expert Member
Apr 12, 2013
232
170
Humu watu hamko Neutral,kuna waziri aliibiwa Hotel na hawara,wala hamkusema ni mambo binafsi,watu walijadili hapa.
 

mangatara

JF-Expert Member
Jul 6, 2012
14,542
2,000
Mkuu niliuliza swali kuwa; Mwongozo aliouomba Mh. Mwingulu kuhusu Mh. Mbowe kumchomoa Mh. Mukya kutoka kwenye msafara wa NY kwenda Dubai tena kwa memo kwa Katibu wa Bunge letu tukufu; uliwaletea manufaa gani Watu wa jimbo lake la Iramba??? Kweli, ule muda wote Mh. Mwingulu alioutumia kulisemea jambo hilo, huku akijua kuwa anasikika duniani kote, hivi aliamini kuwa anaungwa mkono na wapiga kura wake??
Jamani, msimharibu Mwingulu kwa kumsifia. Mkemeeni huenda akajirudi na kuwaza jimbo lake na utaifa zaidi. Wabunge wa CCM mnafikiri mkijibu hoja hatutawaona jinsi mlivyo mahiri??? Wako wapi akina Tuntemeke Sanga wa leo, Wako wapi kina mzee wa kiko, muhaya aliyetikisa bunge kwa hoja muruwa!! Wamebaki wezi tu wa rasilimali zetu na muda wetu wakidai malipo lukuki ati sitting allowance na standing up fee etc etc na mishahara minono ya kutisha wakati Madaktari na waalimu wanasotea KCC. Mungu ibariki Tanganyika
 

OKW BOBAN SUNZU

JF-Expert Member
Aug 24, 2011
31,437
2,000
Mjadala uwe wa mambo ya kitaifa tu.Kwa haya,wengi watakosa pakuficha sura zao.

mkuu hoja za kijinga huzimwa na hoja za kijinga mwenzie.hapa solution ni kuja na documentary ya michakato ya JK ktk kugonga ngozi.wanadhani hatujui.hapa ni kutupia porn clips zao tu
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom