Tutaje dhambi za zamani ambazo sio dhambi siku hizi!

Back years early 2000s pale FPCT Tabora mchungaji alihubiri Kwa ushujaa akisema simu ni dhambi na zimetengenezwa toka kuzimu kuharibu kizazi hiki! Kwa kuwa wengi hatukuwa na simu tulijikuta kuzichukia!

Few months nimepita pale, Mzee anazo kama 3 na tablet juu!!

Dhambi nyingine zilikuwa kuvaa jinzi, kupaka shedo, kuweka kalikiti kichwani (maarufu kupaka dawa), kuvaa wigi, mwanamke kuvaa suruali, mwanamke kuvaa sketi yenye mpasuo, nk!

Siku hizi hizi sio dhambi, maana madhehebu yote wanajiachia tu!

Tutende mema, huyo Mungu Kama yupo tunamjaza maneno ambayo tunakuja kuyakanusha wenyewe!
Ni kweli hata huko tunakoelekea watu watakuwa wanatembea wamevaa chupi tu, itazoeleka na itakuwa kitu cha kawaida.
 
Mzee aliwahi kutusimulia kuwa siku za nyuma, enzi hizo kusikiliza gitaa (guitar) ilikuwa ni dhambi kubwa sana kiasi kwamba unatengwa na kanisa..
 
Zamani kuvaa kapelo, au kofia inayofunika kichwa ni dhambi, kusikiliza mziki hiphop, rnb, reggae hata style za unyoaji ni dhambi.
Siku hizi zime expire.

Sheria za Mungu.

1. Usiwe na Miungu mingine zaidi ya aliyeumba ulimwengu.

2. Usijifanyie sanamu ya kuchonga yenye mfano wowote wa kitu kilicho duniani au mbinguni na kukiabudu.

3. Usilitaje jina Mungu bure. (Maana jina lake ni takatifu mno)

4.Ikumbuke siku ya saba ya Juma ambayo inaitwa sabato, usifanye kazi yoyote inayokupa ridhiki. Siku ya saba utaitambua kwa kutumia kalenda ya lunisolar calendar ambayo unaweza kuidownload playstore au apple

5.Waheshimu baba na mama yako. Yaani watu wote waliozaliwa kabla yako.

6. Usiue wala kumchukia mwenzako.

7.Usizini na mwanamke, Ufilaji, wala kufanya uasherati.

8. Usiseme uongo. Wala kufanya utapeli wowote. Usitoe taarifa isiyo sahihi, ni bora ukae kimya.

9.Usimtamani mke wa jirani yako. Wala mume wa mtu usimtamani.

10. Usitamani mali ya jirani yako, Kwa maana ya kupora, kufanya fitina ili cha mtu kiwe chako.

Hizo ni Amri kumi zipatikanazo kwenye neno lake Mungu,
Note: Fahirisi imeongezewa kidogo.
 
Miaka ya tisini kuna vijiji wachungaji walikuwa wanahubiri kuwa kujenga nyumba ya bati ni anasa kwa msisitizo na watu wakaitikia amen,leo wachungaji walewale wamejenga za bati na rangi kabisaa!!!!
 
Zamani kuvaa kapelo, au kofia inayofunika kichwa ni dhambi, kusikiliza mziki hiphop, rnb, reggae hata style za unyoaji ni dhambi.
Siku hizi zime expire.

Sheria za Mungu.

1. Usiwe na Miungu mingine zaidi ya aliyeumba ulimwengu.

2. Usijifanyie sanamu ya kuchonga yenye mfano wowote wa kitu kilicho duniani au mbinguni na kukiabudu.

3. Usilitaje jina Mungu bure. (Maana jina lake ni takatifu mno)

4.Ikumbuke siku ya saba ya Juma ambayo inaitwa sabato, usifanye kazi yoyote inayokupa ridhiki. Siku ya saba utaitambua kwa kutumia kalenda ya lunisolar calendar ambayo unaweza kuidownload playstore au apple

5.Waheshimu baba na mama yako. Yaani watu wote waliozaliwa kabla yako.

6. Usiue wala kumchukia mwenzako.

7.Usizini na mwanamke, Ufilaji, wala kufanya uasherati.

8. Usiseme uongo. Wala kufanya utapeli wowote. Usitoe taarifa isiyo sahihi, ni bora ukae kimya.

9.Usimtamani mke wa jirani yako. Wala mume wa mtu usimtamani.

10. Usitamani mali ya jirani yako, Kwa maana ya kupora, kufanya fitina ili cha mtu kiwe chako.

Hizo ni Amri kumi zipatikanazo kwenye neno lake Mungu,
Note: Fahirisi imeongezewa kidogo.
amri ya

6. usizini
 
Rose muhando aliimba kuwa watsapp na Facebook na Twitter dhambi Sasa hivi yumo.Alipoimba Huo wimbo tu nikaacha kununua nyimbo zake
 
Mschana kuzaa nyumbani ilikua ni dhambi kubwa sana, ila siku hz ni kawaida na hata wachungaji wetu husikii wakiubiri kwamba kuzaa nyumbani kabla ya kuolewa ni dhambi, unaweza ukaingia kwenye mji wa mtu ukamwona mwanamke ana watoto 2 ukiulizia unaambiwa ni binti yupo kwao.
zamani nilishuhudia babu akimkimbiza shangazi yetu kisa mjamzito
 
Wabawake kuvaa suruali
Hili.makanisa mengi yakiwemo wasabato,walokole,wakatoliki,anglikana no walilivalia njuga kuwa Biblia inasema mwanamke asivae nguo zimpasazo mwanaume.Wakasahau kuwa jeans za Wanawake Ni tofauti na jeans za wanaume .jeans za kike ni vazi la kike si la kiume sababu jeans za kike hakuna mwanaume aweza vaa.kuna mkutano wa maaskofu katoliki ulitanyika bagamoyo nikaenda kutalii pale beach sehemu ya hoteli ya stela Maris. Kulikuwa na masista wazungu walitoka ulaya walikuwa sehemu ya mkutano Kama sekretariat or whatever walikuwa wamevaa jeans na walikuwa wakienda mkutanoni nazo . .Hakuna Bishop Katoliki aliwaambia wasivae jeans wazungu wale masista mkutanoni.Nikauliza chapombe Askofu mmoja aliyekuwa kakaa nao nikaambiwa ulaya Sio masista wote huvaa gubigubi na hijabu za kisista Kama masista wa Tanzania .Wale huvaa kawaida casual kuonyesha kuwa they are part of the society.Africa naona litakuja tu.Sababu sielewi kwa Nini mkutano ule uliohusisha maaskofu katoliki hawakuzuia masista wazungu kuingia na jeans mikutano yao pale Stella Maris hotel bagamoyo Labda sababu Ni wafadhili.TEC Hilo vipi any comment please
 
Back
Top Bottom