Tutaje dhambi za zamani ambazo sio dhambi siku hizi!

Hivyo vyote bado ni dhambi hata sasa hivi na isitoshe tayari Watu wengi sana wameshagundua Wasabato walikuwa sahihi baada ya kukutwa na maradhi mazito hadi kushauriwa wasitumie kabisa hivyo vinywaji na nafaka
Wasabato ilikua dhambi kunywa soda , majani ya chain , kahawa, kula nyama , ugali wa mahindi yalokobolewa . hizi zote zilikua dhambi huko nyuma
 
Hili.makanisa mengi yakiwemo wasabato,walokole,wakatoliki,anglikana no walilivalia njuga kuwa Biblia inasema mwanamke asivae nguo zimpasazo mwanaume.Wakasahau kuwa jeans za Wanawake Ni tofauti na jeans za wanaume .jeans za kike ni vazi la kike si la kiume sababu jeans za kike hakuna mwanaume aweza vaa.kuna mkutano wa maaskofu katoliki ulitanyika bagamoyo nikaenda kutalii pale beach sehemu ya hoteli ya stela Maris. Kulikuwa na masista wazungu walitoka ulaya walikuwa sehemu ya mkutano Kama sekretariat or whatever walikuwa wamevaa jeans na walikuwa wakienda mkutanoni nazo . .Hakuna Bishop Katoliki aliwaambia wasivae jeans wazungu wale masista mkutanoni.Nikauliza chapombe Askofu mmoja aliyekuwa kakaa nao nikaambiwa ulaya Sio masista wote huvaa gubigubi na hijabu za kisista Kama masista wa Tanzania .Wale huvaa kawaida casual kuonyesha kuwa they are part of the society.Africa naona litakuja tu.Sababu sielewi kwa Nini mkutano ule uliohusisha maaskofu katoliki hawakuzuia masista wazungu kuingia na jeans mikutano yao pale Stella Maris hotel bagamoyo Labda sababu Ni wafadhili.TEC Hilo vipi any comment please
Hilo kanisa la Wasabato wa wapi linaloruhusu Wanawake kuvaa suruali?

Kama ni wale walioenda uwanja wa ndege kutaka kwenda Marekani kumwona Yesu ni sawa lakini tofauti na hapo ni big No.
 
Wasabato ilikua dhambi kunywa soda , majani ya chain , kahawa, kula nyama , ugali wa mahindi yalokobolewa . hizi zote zilikua dhambi huko nyuma
Sio dhambi lakini nikatika kulitunza hekalu LA Rohomtakatifu(mwili).Hivi vyote wasabato walivihubiri miaka mingi iliyopita kwamba havifai kuingia ktk mwili wa binadamu lakini mulikebehi kama hivi.Lakini Leo ukienda hospital na Madoctor wanaimba wimbohuuhuu,sasa na hao madoctor au washauri wa Afya nao ni Wasabato?
 
Back years early 2000s pale FPCT Tabora mchungaji alihubiri Kwa ushujaa akisema simu ni dhambi na zimetengenezwa toka kuzimu kuharibu kizazi hiki! Kwa kuwa wengi hatukuwa na simu tulijikuta kuzichukia!
Few months nimepita pale, Mzee anazo kama 3 na tablet juu!!
Dhambi nyingine zilikuwa kuvaa jinzi, kupaka shedo, kuweka kalikiti kichwani (maarufu kupaka dawa), kuvaa wigi, mwanamke kuvaa suruali, mwanamke kuvaa sketi yenye mpasuo, nk!
Siku hizi hizi sio dhambi, maana madhehebu yote wanajiachia tu!
Tutende mema, huyo Mungu Kama yupo tunamjaza maneno ambayo tunakuja kuyakanusha wenyewe!
Kufungisha ndoa kanisani mwanamke mjamzito.
Mkristo kuwa na mke zaidi ya mmoja.
Kanisa kubariki ndoa za wake wengi.
Mapadri Ku........!!!????? mwe, wee acha tu maana tuhuma ni nyingi sana.
 
Safi sana Chifu, duniani kuna mawatu mabishi sana hatimaye siku hizi wanakatazwa kula hayo hayo manyama sababu ya kutosagika kirahisi(red meat) hadi kupelekea shida katika ini, chai ya rangi 7bu ya nicotine inayoweza kusababisha presha, hayo masoda yenye kemikali nyingi tena kama Coca-Cola iliyo na vimelea vya cocaine.

Mpaka sasa hivi ni hao hao Wasabato ndiyo wanaoongoza kwa matibabu mengi yenye ubora kwa mimea ya asili "herbalistic treatment" kwa magonjwa ya kawaida na sugu(yaliyoshindikana)
Sio dhambi lakini nikatika kulitunza hekalu LA Rohomtakatifu(mwili).Hivi vyote wasabato walivihubiri miaka mingi iliyopita kwamba havifai kuingia ktk mwili wa binadamu lakini mulikebehi kama hivi.Lakini Leo ukienda hospital na Madoctor wanaimba wimbohuuhuu,sasa na hao madoctor au washauri wa Afya nao ni Wasabato?
 
Wachungaji hua wanasema kuangalia picha za ngono ni dhambi,sasa najiuliza wao wamejuaje kama kuna picha za ngono?
Maana yake na wao wanaangalia kwanza,kwa hiyo wengine kuangalia dhambi,ila wao si dhambi,nacheka saaaana!
 
Mbona watu mnataja vitu ambavyo kibiblia bado ni dhambi? Labda tuspecify kwamba “kitu fulani mi kwangu sio dhambi”.

Anyways nani anaijua togwa? Kijijini kwetu ni aina ya kinywaji watu hunywa hasa wakitoka kufanya kazi ngumu mfano kulima, Sasa Kanisani kwetu zamani tulihubiriwa kuwa kunywa togwa ni dhambi, binafsi niliamini na nikawa sinywi, siku hizi nikiikuta mahali napiga tu.
 
Mschana kuzaa nyumbani ilikua ni dhambi kubwa sana, ila siku hz ni kawaida na hata wachungaji wetu husikii wakiubiri kwamba kuzaa nyumbani kabla ya kuolewa ni dhambi, unaweza ukaingia kwenye mji wa mtu ukamwona mwanamke ana watoto 2 ukiulizia unaambiwa ni binti yupo kwao.
kweli akibeba mimba anafukuzwa
 
Leo hii huwezi mfukuza binti yako nyumbani kwa sbb kabeba ujauzito akiwa nyumbani
Inategemea na aina gani ya mzazi, mama yangu ni no nyingine, alishasema mtu akibeba mimba aondoke kabla hajamfukuza mwenyewe.
 
Zamani binti aliposalimiwa kwa salami ya "Mambo" na mvulana au mwanaume alikwenda kusema nyumbani. Siku hizi hadi wazee wanatumia hiyo salamu kwa vijana/watu wazima Wa jinsia zote bila shaka yoyote
 
Back
Top Bottom