Tutaitoa CCM kwa Umafia 2015 - Wananchi | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tutaitoa CCM kwa Umafia 2015 - Wananchi

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by STEIN, Jan 5, 2011.

 1. STEIN

  STEIN JF-Expert Member

  #1
  Jan 5, 2011
  Joined: Aug 29, 2010
  Messages: 1,764
  Likes Received: 4
  Trophy Points: 135
  Nimejaribu kupata maoni ya ya wadau, wapenda nchi hasa Vijana wazalendo wa nchi hii wametoa kauli kuwa 2015 wataiondoa CCM kwa kutumia njia ambazo viongozi na mafisadi wengi wa nchi hii wanaitumia kuihujumu nchi hii na wananchi.

  Njia hiyo ambayo inaamika ilitumika ubungo, Kawe Ukerewe, Ni pamoja na kuhakikisha kuwa wanapitishwa watu ambao ni mafisadi wa kutupwa kwenye chama na kuhakikisha vijana wengi wanaokubalika kwa wananchi wanagombea kwenye kura za maoni ili wakichakachuliwa wataamua kuiunga mkono chama cha upinzani ambacho kina nguvu kwa wakati huu na kimewafungua macho watu wengi.

  Wakizungumza kwa kujiamini vijana hao ambao wengi wao ni wahitimu kutoka UDSM wamesema wao wako tayari kwenda kugombea kila jimbo la uchaguzi na wako tayari kujigawa mpaka waweze kuenea majimbo yote ya uchaguzi nchi nzima. Katika kufanikisha hilo vijana hao watatumia uhalisia uliopo wa waTZ kuhujumiwa sana katika nyanja za ajira kwani maeneo mengi na makampunimengi yamekuwa yakiajiri watu kutoka nje ya nchi kwa kisingizio cha TZ hakuna wataalamu. Katika kuthibitisha hilo vijana hao waekuwa wakikusana takwimu za kujua idadi ya wageni ambao hawana uwezo wa kielimu na huku wameshikilia nafasi za ajira katika makampuni mbali mbali zikiweo za simu, uzalishaji viwandani n.k.

  Vijana hao wameamua kujitupa huko kwenye siasa wakiwa na lengo moja tu la kuiondoa CCM madarakani ili yale yaliyohubiriwa na mgombea urais wa CDM yaweze kutimia kabla ya 2020 ambapo maisha yatakuwa magumu sana kama CCM itapita na kuendelezi ufisadi na uhuni wanaoufanya sasa.

  Vijana hao ambao wengi wao ni wahitimu wa vyuo vikuu hawaelewi na hawoni ni nani wa kumuliza kwa nini nafasi za ajira zimekuwa zikienda kwa Wahindi, wakenya, waarabu na wachina ambao wengi wa wageni hao hawana vibali vya kuishi inchini inakuwaje wanapata nafasi ya ajira? Je, ukienda huko nje unaweza kupewa kazi ile hali huna kibali cha kuingia nchini kwa watu?...... Ni vigumu sana kuelewa.

  Katika hilo hata mimi naungana nao kwani ni jambo la ajabu sana,hivi hawa wageni hata aibu hawana.... Maana wachukue Madini bure, Wachukue nafasi za ajira, K/KOO maduka yote yao je sisi tutaenda wapi? Naomba hili swali kila mtu ajiulize hata kama uko CCM tutapigika wote.

  Katika kuhakikisha wanafanikiwa vijana hao wamesema dawa nikuivunja CCM wiki kama mbili kabla ya uchaguzi ili hata wakichachachua vipi wasiweze kufanikiwa.


  Itaendelea...............
   
 2. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #2
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  waambie hao vijana waache ndoto za mchana, pia nani kawaambia nchi hii inahitaji mapinduzi ya kisiasa tu? Pumbavu zao huko udsm waliendekeza starehe bila kudevelop creative facults zao ambazo zinge badili fikra zao badala ya kua job seekers wawe job creators, sasa njaa zao na uzembe wao wa kifikra umewafanya kufikiria ubunge na siasa ndio suluhisho. Shenzi kabisa kuna mapungufu mangapi ktk jamii ambayo yanahitaji usimamizi wa graduates, na maelekezo kutoka kwao? Useless graduates ni hatari kuwapa madaraka, fanyeni kitu kwanza na mui onyeshe jamii, sio kukimbilia kwenye siasa mnataka easy money? Hatutaki watu wa aina hii katika mchakato mzima wa kuelekea kwenye ukombozi wa kweli na wewe mtoa mada next time chuja kwanza kabla hauja tuchafua fikra zetu, nyammbbaff.
   
 3. K

  Kicheruka JF-Expert Member

  #3
  Jan 5, 2011
  Joined: Feb 2, 2009
  Messages: 791
  Likes Received: 3
  Trophy Points: 35
  Maamuzi yote nchi hii yanafanywa na wanasiasa, wacha vijana waingie siasa wafanye mabadiliko ya nchi yao kwa manufaa ya wote na wasomi msigombanie ubunge tu kuna udiwani ambao ni rahisi kushinda na mipango ya maendeleo inafanywa na halmashari ambako wamejaa madiwani wasio na shule. Vijana msikate tamaa fanyeni maamdalizi na time ikifika ingieni siasa acha porojo za CCM kuwaambia muwe creativity bila mitaji wanataka mkavunje kokoto au kubeba zege na mazingira ya ajira walishaharibu wanaowapa ajira ni watoto wao na ndugu zao
   
 4. Wambugani

  Wambugani JF-Expert Member

  #4
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 8, 2007
  Messages: 1,755
  Likes Received: 47
  Trophy Points: 145
  Kwa nini tusubiri tuwavumilie mafisadi mpaka 2015? Mmeona Serikali imeridhia malipo ya Dowans.

  Mwalimu J. K. Nyerere alisema, "Kinachowezekana leo kisingoje kesho."
   
 5. BRUCE LEE

  BRUCE LEE JF-Expert Member

  #5
  Jan 5, 2011
  Joined: Dec 11, 2010
  Messages: 2,089
  Likes Received: 1,158
  Trophy Points: 280
  kusema wawe creative ina maana kubwa nadhani upeo wako umeshindwa kunisoma, kuna njia nyingi za kutatua matatizo, nani kakwambia mtaji ni pesa tu?mi si ccm na ninaichukia zaidi ya unavyofikiria. Wafanye mambo yaonekane na sio kusema uongozi wa kisiasa tu au ubunge lets say wote wakagombee ubunge na wapate hapo dodoma patatosha? Tunahitaji kupunguza idadi ya wabunge na baraza la mawaziri hadi madiwani ili kupunguza matumizi ya serikali. Mmenisoma?
   
Loading...