Tutafakari zaidi migogoro inayotukumba.

Tutafakari zaidi migogoro inayotukumba.

The Donchop

JF-Expert Member
Joined
Jan 10, 2014
Posts
294
Reaction score
381
Mambo ?
Jamani leo nakuja na mada hii special kwa wote ambao wapo kwenye mahusiano kabla ya ndoa.
Kuna janga nimeliona ndugu zangu. Naomba tujadili leo kwa mapana maana litatusaidia wengi.
Mara kadhaa kumekuwa na mada nyingi za migogoro ya kimapenzi ambayo mwisho wake huvunjika. Mara nyingine zinakuja mada za migogoro muhusika akiomba ushauri baada ya kupata mgogoro, bila kujali aina ya mgogoro, mara nyingi ushauri wa wana jamii forum kwa asilimia kubwa ni ACHANA NAE, HANA MAPENZI YA DHATI KWAKO.
Sikatai, kuna migogoro ambayo unaona wazi kuwa muhusika anatumiwa, ni vizuri kumshauri akajiondokea zake.
Lakini kuna migogoro ambayo haina haja ya kumshauri muhusika kuachana na mwenzi wake. Mfano mgogoro wa kuzimiana simu au kutopokea nk.
Ninachopenda kusema ni kwamba, hizi changamoto zipo kwa kila mtu. Ukimkataa mnuka kwapa kesho unakutana na mnuka mdomo ama asiyeoga kabisa.
Migogoro mingi ni ya kutatulika tu pasipo kufikia kuachana. Unapopata mgogoro, usifikirie kwanza kutafuta mtu mwingine bali fikiria natatuaje hili tatizo? Kama halitatuliki sepa.
Mfano mimi mwenyewe, aisee nilipata mpenzi kwanza mlevi, alafu ana roho ya visasi sana. Nilijaribu kuongea nae, kumshauri na kumsomea hata maneno ya Mungu, ameapa kutobadilika. Nikaamua kuongea na mama mkwe, nae akanihakikishia huyo kijana yupo hivyo toka mdogo hivyo sitamuweza. Nikaamua kuondoka lakini nikiwa nimejaribu njia zote nijuazo.
Hivyo wana jamii hasa vijana ambao wanapata changamoto ikiwa ni wageni wa changamoto hizi, kuna changamoto za kukimbia haraka sana na zile za kusolve. Usitupe upendo wako kapuni sababu ya mgogoro mdogo unaoweza kutatulika.
 
Back
Top Bottom