Tutafakari kwa pamoja ujumbe huu

Matanga

JF-Expert Member
Nov 13, 2019
2,281
3,973
Kila Binadamu anapitia nyakati mbalimbali ikiwemo Furaha na Amani ,ukiwa na Furaha mshukuru Mungu ujue umejariwa kipindi hicho na ndo wakati UNATAKIWA kuwafariji Wenye huzuni!

Lakini ukumbuke kuwa kipo kipindi cha huzuni Wenye Furaha na Amani ndo hujakukufariji nawe, ikiwa unawakwepa Wenye huzuni kisa una Furaha ukumbuke Dawa ya Moto ni moto!

Usitatue tatizo wakati unahasira hutaweza kupata suluhu, ukiona Magumu mengi yamekufika ndo wakati wa kuwa mtulivu kukabiriana changamoto!

Mungu ni wa kwanza kujaria njia njema,ukiamini inawezekana!
 
TUANGALIE IKIWA SHIDA NI MTAJI

Mmoja hana mtaji kweli ila anaona Fursa nyingi mno za kufanya

Namba mbili huyu ana mtaji haoni Fursa ya kufanya kabisa

🟥Umeelewa nini hapo?


Mmoja aliyesema ana Fursa lakini hana mtaji amepewa mtaji ndio lakini anasema hajaanza bado sababu kuu ni Kwamba alivopata mtaji Fursa zimepotea.

Huyu wa pili aliyekuwa na mtaji akihitaji Fursa anadai alivotumia mtaji wake Fursa zimekuwa nyingi mno maana ameanza kuziona!

🟥Shida nini hapo?


Jaribu hii

Watu wengi tunaishi bila mipango kichwani kabisa,hatujui jana yetu ...leo yetu ... kesho yetu na baadae yetu ila tunataka utajiri Mkubwa!

Jaribu kumuuliza rafiki yako ikiwa anampango wowote wa kufuata ambao unamsaidia yeye kupita yaani ramani yake ya kupita utaona hana kabisa ni kweli hajasoma Ujasiriamali lakini ukumbuke ulisoma SOMO LA MAARFA YA JAMII hukukuelewa chochote kuhusu Ramani inafaida gani kwako!

Watu wengi huhitaji kuwekeza au kujiajiri wakati huo wamekataa Maarifa ya kujiajiri kabisa na huwezi kuona Malengo yake katika kujiajiri ila utakutana naye akifeli kujiajiri

Kwa Maisha ya leo kila mmoja ni Mjasiriamali hata kama umeajiriwa hutakwepa kujiajiri sababu tuko kwenye maisha ya jikomboe upige hatua hayupo wa kukukomboa wewe maana baba hali tete mtoto hali tete umebaki na silaha Moja jipiganie jikomboe jiinue

SASA shida sio mtaji shida ni akili yako uandae akili kujikomboa na kujiinua huna wa kumwachia mzigo wako ni wewe na mikoba yako!

Nenda popote kwanini wenye pesa wanalalamika kuliko maskini sababu mwenye pesa anafikiri pesa zinazaa pesa bila akili na maarifa ni Ngumu mno
 
Wewe mjasiriamali na unachakalika kweli je unampango kazi wa shughuri yako ...hapana
wewe Mjasiriamali je unajua Biashara ya Kazi yako inaendaje au unasubiri wakufanyie wengine je soko lake unajua au

Huenda una mradi ok unafahamu vizuri mradi wako unalenga nini unaenda wapi?

Yule mtu anayekosa Fursa huku anamtaji ni yule mtu asiye na Elimu ya mtaji na Elimu ya Fursa

Yule mtu anayekosa mtaji ila anaona Fursa huyo hajui maana ya Fursa na hajua maana ya mtaji ndo maana alivopata mtaji hakuona Fursa!

Ukiwa na Elimu ya ujasiriamali huji kukosa Fursa na huji kukosa mtaji

Sababu mtaji wa kwanza ni Maarifa YALIYO kichwani hutumika kama taa ya kumulika pande mbalimbali kuna nini ni rahisi kutengeneza jambo likakupatia Mtaji kisha Fursa KISHA ukasimama imara tena!

Mtaji wa pili ukiwa na maarifa ni kujua kuishi na watu vizuri usijiinue endelea kuwa yule yule mtiifu wakati wote acha dharau ukiwa nacho ili unapoishiwa uinuliwe na watu hawata kuacha kamwe!

🟥Hivo kuwa na akili na maarifa ya kuwazunguka watu usisubiri watu wakuzunguke utachelewa mno kufikia ndoto zako

 
Unafikiri kwanini Watu ambao ni bahiri huwa hawafanikiwi

Ukirejea neno la Mungu linaeleza wazi wazi kutoa ni kupanda mbegu nzuri, mbegu hiyo unasubiri inaota kisha inakua kisha inazaa matunda mazuri

Mkulima yeyote huenda shambani na mbegu nzuri ili baadae apate mazao mazuri ijapo hutegemeana na huduma yako!

Hivo basi utoaji ni Faida kwa mtoaji kuliko kwa mpokeaji ikiwa tu utoaji huo unaenda kwa moyo wote!

Wengi hawajaelewa maana yake nini

Utoaji unaweza kuwa Muda wako kusaidia wengine
Utoaji unaweza kuwa mali yako kwenda kwa wengine
Utoaji unaweza kuwa Elimu unawapatia wengine kwa upendo bila kutega faida wala kujihesabia Faida

🟥Kadri unavotoa ndivo unavyobarikiwa mno

Ijapo watu wengi huhesabu utoaji wa pesa tu kama ndo ametoa Sana mno ila sio kweli

KUMPATIA MTU MAARIFA NI FAIDA YA KUDUMU AMBAYO NI URITHI TOSHA KULIKO PESA NA MUDA

USIDHARAU MTU ANAYEKUPATIA ZAWADI YA MAARIFA

🟥🟥Ijapo kuna shida mno kwa Mbongo kuheshimu mtu aliyemsaidia akafanikiwa ndo maana msemo ULIKUJA wa tenda wema nenda zako usingoje shukrani

Usimsaidie mtu kuzani akiinuka atakupatia heshima sio kweli huenda akawa wakwanza kukutimulia mavumbi kikubwa sadaka yako ilete Neema ilete Baraka!

Kwa UCHANGA wa akili yangu na UZOEFU wangu mtoaji yeyote hupewa pia na hukumbukwa pia sio wote watakuona hivo ila wapo utakao endana nao siku moja kadri utoavyo kadri ujitoavyo!

Kwa UCHANGA wa akili yangu na UZOEFU wangu bahiri wengi hufa maskini mno hawana maendeleo yoyote kabisa kila mara yuko vile vile tu!

 
Utashangaa kwanini wasio watoaji huwa hawafanikiwi si kunasaidia kumiliki mali zako.

Mali yoyote uliyonayo ukumbuke hukuzaliwa nayo ili toka kwa wengine sasa wakibaini Moyo WAKO ni mchoyo mno maana yake hawatakuleta hiyo mali tena utakosa Kupokea kwao sababu hutoi pia Baraka zinafungwa

Bahiri wengi huwa bahiri kuanzia mali hadi akili yake, hivo huwa hawatoi mali,Muda na maarifa kwa wengine hatimae hata kujifunza kwa wengine huwa Ngumu mno sababu huwachangamani kabisa na wengine!

Bahiri wengi kuna sehemu shetani anawapeleka kupoteza mali zao tu, wengi unakuta wanapenda anasa huko hawaogopi kuacha mali zao Muda wao na maarifa yako njia zao huwa mbaya mno!

Hawaendelei sababu Maisha ni kutegemeana na kushirikiana hivo mtu asiyemtoaji mara zote huwa kinyume kila JAMBO na wengine na huwa nawachukulia kama hawana akili za kesho yake!

 
WIMBO NI ULE ULE

JAMBO lolote usipojua kweli yake huna haki ya kutoa hukumu sababu lazima ukose majibu

Mtaifahamu kweli na kweli itawaweka huru

Tuwe na mandalizi na tujue wakati ujao kuna kuishiwa watakao kuinua ni wale uliowainua na walizoea kuinua wengine!

Usipuzie Maarifa na muda wa mtu alikusaidia kwa kuhesabu msaada mmoja tu wa mali uliyotoa kusaidia wengine!
 
Leo ni niseme!

Penda kujifunza kitu fulani kwa Muunganiko kinaleta tija maana faida huja kwa Muunganiko sio nusu nusu

KUJIFUNZA MUUNGANIKO MAANA YAKE NINI?

Ni pale unapohitaji kufanya jambo fulani ukapata Muda wa kufahamu namna halisi ya kufanikisha jambo lenye na tahadhari zinazoweza kukuzuia kulifanikisha hilo jambo

Usiwe na upande mmoja tu kuwa unataka Kufuga kuku au unataka kulima nyanya BASI unaanza kisa una mtaji na eneo

Unasahau .... Usimamizi,huduma,Mteja lengwa, usifiri kumfikia, biashara yake unaijua, n.k

Lazima uwe na upeo wa kitu unachohitaji kufanya

Una Fursa ya kufanya
Kwanini umechagua hiyo
wapi unafanya
Utawezaje kufanya
Wapi pataleta changamoto panahitaji mtaalamu akuongoze
Malengo yako nini
Muda gani utafanya mpaka kufikia kutimiza lengo lako
Wasimamizi wako ni akina nani
Kwanini umewachagua hao umetumia vigezo gani
Utayari wako ukoje
Ukifeli utafanyaje
Una amani na Kazi yako

Uko TAYARI kuilinda inapoanguka

Unajua kuanguka kupo na USIRUDI haraka je utairudia tena

Ni mwaminifu juu ya mipango yako, Akiba zako, bajeti zako na kukuza Kazi yako

Unaelimu ya soko lake

Unaelimu ya Biashara

Unajua kutenga faida na mtaji

N.k

Jibu maswali hayo ndipo uanze mradi wako hutajuta hutaanguka kizembe

Acha kusingizia wengine, kukukwamisha jitahidi kuangalia ni wapi ulipoteleza!

Mwaabudu Mungu kweli kweli usiabudu kinafiki hutabarikiwa


🟥Ndoto yako haiko kwa mtu iko kwako mwenyewe!

Ila Kumbuka

Code:
Hagai 2:7
nami nitatikisa mataifa yote, na vitu vinavyotamaniwa na mataifa yote vitakuja; nami nitaijaza nyumba hii utukufu, asema BWANA wa majeshi.

Hagai 2:8
Fedha ni mali yangu, na dhahabu ni mali yangu, asema BWANA wa majeshi.

Hagai 2:9
Utukufu wa mwisho wa nyumba hii utakuwa mkuu kuliko utukufu wake wa kwanza, asema BWANA wa majeshi; na katika mahali hapa nitawapa amani, asema BWANA wa majeshi
 
🟥Usiwe na ndoto maskini utegemee ikupe utajiri

Kuna wakati ndoto zetu Malengo yetu tunaweka kwa mihemko bila kujua uhalisia wake ndo maana tunachelewa kufikia Malengo yetu wengi

Je ndoto maskini ikoje na malengo maskini yakoje
 
🟥Mungu ameweka karama gani kwako ya kukupatia Faida na kuwapatia wengine Faida

Ukiona nyuma yako na mbele yako hakuna kundi ulilolipa faida tafuta hiyo faida,

Lazima watu wafanye JAMBO fulani kwenye Mafanikio yao wakuone upo wewe!

Na jambo hilo lazima liwe la ubunifu wako ndani yaani wakuone wewe uliweza kitu ambacho walishindwa wengi na wala hawakufikiria wengi

Na ukifanya hivo unapopokea sifa usijione wewe ndo wewe na kujiinua utapotea bila kujua ......lazima ukubari kuwa yule yule usiyebadilika seti akili yako kuongeza jambo lingine na lingine

KILA siku uwe mdaiwa wa kitu fulani ambacho Mungu ameweka kwako kama TALANTA YA KUSAIDIA WENGINE NA USIOGOPE KUTOA KILE UNACHOJUA KINALETA MANUFAA.

Kuna watu wanavitu vizuri huogopa kuviwasilisha kwa wengine kwa kigezo cha watanionaje,

Nikweli wapo wasomi juu yako wanaelimu za PhD,prof n.k lakini haina maana sio wajinga wakitu fulani nawao hawajui vingi tu mno ndo maana hajaona wakitoa kwa wengine

Ukiona sehemu inawasomi wengi lakini maendeleo hayapo ujue usomi wao hauna uhusiano na kuleta maendeleo usiwashangae kuna fani zingine wanaweza na usiwadharau kuna msaada watakupatia Muda ukifika ijapo sio wote wengi husoma bila kupata maarifa wezeshi Katika kutumia!

🟥Tambua TALANTA yako uwape wengine FAIDA na ikupe FAIDA na wewe!

Je umefanya nini ni mbegu kwa wengine
 
KUFUNGUA miradi Mingi Mingi Bila faida ni kupoteza muda bila kujua

Cha kufanya nini

Simama na mradi hata mmoja uende nao ukianza kuleta faida ndo UNATAKIWA kuruhusu mtawanyiko wa miradi itakayo saidia kuongeza pato

Na miradi yako iwe na uhusiano wa karibu mno Mfano

Unafuga kuku wa Mayai au nyama ukiwa na uwezo wa KUFIKISHA kuku 1000 ni mradi Namba moja huo umesimama

Fikiria mradi Namba mbili Mfano kununua mashine ya kuangua Vifaranga hata Mayai 10000

Ukianza kuuza Vifaranga hesabu kama zao la Mradi Mkuu uhusiano ni wa karibu mno

Nenda nayo miwili ukifika wakati fungua mradi wa kuandaa CHAKULA cha kuku Ili iwe rahisi kuhudumia kuku na Vifaranga

Tayari huo mradi wa TATU
KUMBUKA MIRADI YAKO
kuku 1000
mashine ya kuangua Vifaranga 10000
Mradi wa kuandaa CHAKULA KILA siku walau kilo kilo 1000



Jiulize unapata wapi nafaka

UNATAKIWA kuanza kuzalisha mwenyewe soya, mahindi n.k huo ni mradi mwingine wa kukuvusha hatua ya pili!


Maana yangu nini?

Usianze mradi na Kuacha au miradi Mingi Mingi Bila faida ni HASARA mno

Jikite VIZURI kwenye mradi Mmoja lakini Zingatia usahihi wake!
 
Ukisema una Ng'ombe wa maziwa basi iwe Ng'ombe kweli Ili walau kwa siku upate lita 100+ inasaidia kuleta unafuu wa Maisha!

Usifungue mradi unaokutesa yaani mradi dhaifu HAITAKIWI!

Fanya kitu KIDOGO lakini kilenge Faida kubwa hata kama sio leo basi baadae!
 
Miradi yako ukiitazama au watu wakitazama waone kuwa


Yes ulimshirikisha mtaalamu kuanzisha

Yes unamshirikisha mtaalamu kuendesha..

Yes inaleta faida bila wasiwasi


🟥Mambo yanasababisha tusiwatumie wataalamu wetu KWENYE miradi ni kujihesabia haki mno

Yaani unajiamini mno bila kujua huna utaalamu na hicho kitu

Mungu aliyeweka Walimu tunamkosoa si ndio basi nendeni kwa akili zenu mpate matunda YENU .

Pili jambo linalofanya tusiwatumie wataalamu wetu ni dharau ....
Watu Wengi huona fedheha Kuomba ushauri kwa mtu ambaye akiangalia anaona anamzidi kipato mara Maisha kwa ujumla hivo anapiga Moyo konde jumla huenda ndio ni Sahihi lakini jiulize..... Maarifa juu hilo suala unautajiri nalo

Kuna utajiri wa hekima
Kuna utajiri wa Maarifa
Kuna utajiri wa imani
Kuna utajiri wa mali
Kuna utajiri wa ushauri n.k

Ndo maana ukisoma neno la Mungu isaya UTAONA kumbe kuna watu wao wamejariwa Roho ya hekima wengine Roho ya UFAHAMU n.k

Isaya 11:2
Na roho ya BWANA atakaa juu yake, roho ya hekima na ufahamu, roho ya shauri na uweza, roho ya maarifa na ya kumcha BWANA;


Hivo unapokuwa na mali unahitaji kukamilishwa na vitu VINGINE ambavyo huna .....tuna rudi point ya kufaidiana


Hivo basi usione aibu Kuomba msaada wa kile UNACHOONA hakiendi SAWA!

Kuna watu tukiamua kushirikisha wataalamu ni rahisi kufika

Watu wanamitaji wanaharibu mno kupeleka SEHEMU yenye miiba yaani kusikozaa matunda!
 
Back
Top Bottom