Mwanga Lutila
JF-Expert Member
- Nov 10, 2016
- 4,205
- 14,123
Habari wakuu,
Naombeni tulitafakari hili.
Wazazi wengi sana wanalalamika watoto wao wa siku hizi wengi ni vimeo wameharibika hawapendi mambo Serious wanapenda tu mambo ya hovyo hovyo ambacho hawa wazazi wanasahau wao ndio waliotulea sisi kufika hapa tulipofika kama kuna maadili yaliyopotea basi ujue hawakutukabidhi vema mikoba ya makuzi na malezi.
Kutoka kizazi cha wazazi wetu kuja chetu kuna mambo mengi sana yameporomoka kimaadili, kiuchumi, kisiasa na kiroho. Yale yanayotokea sasa ni matokeo ya yale ambayo hawakutufunza vizuri, wao wanalalamikia kizazi chetu hakina maadili na sisi tumeshaanza kuwaona wadogo zetu na watoto zetu walivyo, tumeanza kulalamika watoto wa siku hizi ni vimeo wote tunalalamikia matokeo.
Katika chunguzi zangu nimebaini kutoka kizazi kimoja kwenda kingine kuna kitu kinapungua katika maadili kwa sababu hiyo kuna "Genarational Consequences" kutoka kizazi kimoja kwenda kingine.
Wazazi wwtu wanalalamika sisi hatuna maadili, na sisi tunalalamikia wale wanaokuja sababu wao wanatuona washamba kama sisi tulivyowaona washamba wazazi wetu na hawajui kitu na wamepitwa na wakati.
Kila mmoja wetu kwenye kizazi chetu anaweza akawa ana -imapact kizazi kijacho kiweje, kiwe kinawa namna gani, kiwe kinaongea namna gani, kiwe kinavaa namna gani, kiwe kinaamua namna gani.
Enzi za baba zetu Wanawake bikira ndio walikuwa marketable na wazazi walikuwa wanajisikia vibaya mtoto wao akipoteza bikira, Kizazi chetu tulichukuwa nacho sisi Mwanamke bikira anachekwa eti mkubwa mzima hajawahi kufanya!!! utaendaje kwenye ndoa hujawahi fanya kwa kujua ama kutokujua umetengeneza "Generational Impact" na sasa usishangae watoto wenu wakapoteza bikira wakiwa darasa la pili A. Na wajukuu wako wakapoteza wakiwa "Vidudu" kwa sababu kutokuwa nayo itakuwa ndio Fashion na wewe mama au baba umejenga tofali la uharibu wa kizazi chako cha 3 na 4 (Generational Consequences).
Kuna mambo usipoyafanya kwenye kizazi chetu unaweza kuonekana kuwa umepitwa na wakati na ni mshamba ila watu hawajui kuwa unajenga tofali la watoto wako na wajukuu wako, kwa kufanya ujue umefungulia milango kwenye uzao wako..Generational Thinking inapelekea "Generational Consequences" Hii inazaa "Generational Death" Unabisha? Hebu angalia Wazazi wetu walizaliwa wangapi kwao, Halafu sisi tumezaliwa wangapi, Halafu wewe una watoto au una mpango wa kuwa na watoto wangapi, Kisha angalia watoto wako watazaa wangapi halafu ukitizama kwa jicho la tatu utaona kuna "Generational Death".
Tafakari hili.