Uchaguzi 2020 Tutafakari haya yaliyopita

onjwayo

JF-Expert Member
Apr 8, 2020
1,350
1,307
Watanzania wenzangu tunaingia tena kusikiliza zile nyimbo nzuri za kampeni. Ilani zinazotia matumaini huku wanaozitoa wakijua wanatudanganya. Ilani zilizoshiba matumaini kwa kada masikini wa kutupa. Tunaelekea wakati ambapo watoa ahadi watatuonyesha ukarimu hadi wa kushare pamoja mlo wa mahindi na matembele iliyotiwa chumvi.

Tunaelekea kipindi cha kutembeleana na kujaribu kuwa karibu na ndugu tukionyeshwa mapenzi mazito kabisa. Tunatesti mitambo ambapo tutashuhudia burudani za kila aina ilimradi tu mtanzania aweze kutupigia makofi kuwa tunafaa. Tutaona mengi na kwa upande mwingine tutashuhudia ukarimu wa kupindukia tukibugia bia na gongo live.

Tunaelekea kipindi ambacho biashara za watu zitakuwa huru bila kuwekewa vikwazo. Nakuambia hata gongo sasa inaweza kupigwa live sababu tu mwananchi asibughudhiwe. Njama za kila aina zitapangwa ili tujilazimishe kupenda na hatimaye tutoe kura. Kila aina ya uzuri lakini tutafakari haya yaliyopita.

1. Tushawahi kujiona tuko ndani Dubai kama tulivyoahidiwa?
2. Tanzania ya viwanda imefikia wapi, au mimi ndio mshamba na sitembei?
3. Zile milioni 10 zimemezwa na watendaji wa kijiji au mie ndio sifiki huko kijijini?
4. Ajira kwa vijana wetu tayari au mie ndio sina vijana kwa kuwa kikongwe?
5. Wafanyakazi wetu wanayo maslahi yale waliyoahahidiwa kuboreshewa miundo ya mishahara na kuongezwa mishahara?
6. Utumishi wa umma umeboreshwa baada ya lile zoezi la kuounguza wafanyakazi wenye vyeti feki na hewa?
7. Wanafunzi vyuo vikuu wanapata mikopo kwa wakati na kwa kiwango kinachotosheleza?
8. Haki ya binadamu kwa nchi hii imeboreshwa kwa kiwango gani?
9. Vipi kuhudu wale mafisadi, bado wapo au jela zimejaa wanasubiri awamu nyingine?
Huduma za kijamii mf afya na elimu zina ubora wa kiwango cha kuridhisha?
10. Miundombinu barabara na reli ni kama tulivyowasikia wakijinadi, huko makwenu njia inapitika misimu yote?
11. Je, mawasiliano ni huru kwa kiwango gani na uhuru wa kujieleza badoga upo kwenye vyombo vyetu?
12. Utawala bora kwenu huko madc na marc badoga wanawaweka ndani kama mbuzi?
13. Wale watu wasiojulikana badoga wapo?
14. Tume ya uchaguzi ni huru kwa kiwango gani?
15. Rushwa huko kwenu bado upo?

Natafakari, ila niko hapa nje naona Tanzania ni ile ile kabla ya uhuru isipokuwa kuna vilami na nyumba za bati kidogo. Ahadi ya Dubai tutegemee kwingine ila siyo CCM tena. Hawa washatudanganya tangu uhuru.
 
onjwayo,

Natafakari, ila niko hapa nje naona Tanzania ni ile ile kabla ya uhuru isipokuwa kuna vilami na nyumba za bati kidogo. Ahadi ya Dubai tutegemee kwingine ila siyo CCM tena. Hawa washatudanganya tangu uhuru.
 
CCM mkisha iba kura, chukueni kura zote za hapana, mpelekeeni mwenyekiti wenu Kisha mwambieni hizi ndio salamu halisi kutoka kwa Watanzania, hicho kiti tumekubeba tu na kukukalisha hapo
 
Back
Top Bottom