Bulelaa
JF-Expert Member
- Jun 28, 2024
- 1,143
- 2,871
Je, Ni kosa kuwa mfuasi wa Chadema na au kuwa upinzani?
Ni dhambi kutoka chama kimoja na kwenda kuwa mfuasi wa Chadema na vyama vingine?
Ni kweli kabisa wanaohusika mara nyingi kuwatesa na saa nyingine kuwapoteza viongozi na wafuasi mbalimbali wa vyama vya upinzani, hujiridhisha kuwa ndio haswaa ni wavunjaji wa sheria za nchi na adhabu yao ni kupotezwa?
Kunashida ipi ikiwa mmoja wetu anakumbusha wajibu wa mwingine kushughurikia masuala na kero za wananchi hali ya kuwa naye ni Mtanzania?
Ni kweli kwamba tumeamua tufikie kiwango cha kuhukumu kifo kwa wengine na hakuna sheria stahiki inayowahukumu ilihali hata tusipofanya hivyo bado kifo kipo pale pale kwa wote?
Ni lini tutafikia kiwango cha kuchukua mema ya wakosoaji na yale yasiyofaa tukayapuuza na kuwapuuza?
Natamani nchi yetu, tuwe na viongozi wengi wenye kupuuzia mambo kama alivyokuwa msaatafu Rais Kikwete!
Eee! MUNGU wa Tanzania, umeamua kunyamazia hukumu zako zinapoingiliwa na uliowaumba?
MWENYEZI MUNGU, TANZANIA yote inajua kuwa wewe upo, unaona, Na kwamba, wewe hautakaa utulie, pale wenye haki wako wanapolia machozi ya damu
TANZANIA NAKUPENDA
MUNGU, UWABARIKI VIONGOZI WETU
UWABARIKI VIONGOZI MBALIMBALI WA KISIASA!
AMINA
Mwisho, Tanzania ni yetu sote, ingelikuwa ni jambo zuri iwapo tukikubaliana kisheria na kikatiba, kiwango cha kila mtu anapotoa maoni kuhusiana na mwelekeo wa nchi yetu, aongozwe na sheria zipi na akikiuka atachukuliwa na sheria fulani na ama tukubaliane tuwe na chama kimoja
Hii itaondoa damu za wengine kuwa kama dhabihu katika taifa lao kwa mambo ya kupuuzwa tu!