Tusonge mbele

singidadodoma

JF-Expert Member
Nov 11, 2013
4,394
1,536
MAPEMA wiki hii, serikali ilinunua mashine mpya ya CT-Scan inayotajwa kugharimu dola za Marekani milioni 1.7, kwa ajili ya kutoa huduma za uchunguzi wa magonjwa mbalimbali katika Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH), jijini Dar es Salaam.

Inatambulika kwamba uamuzi wa kununua mashine hiyo umetokana na msukumo ama agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Magufuli, ambaye amepata kufanya ziara ya kushtukiza hospitalini hapo na kubaini kasoro kadhaa zinazokwamisha utoaji wa huduma bora kwa wagonjwa.

Kati ya kasoro alizobaini Magufuli katika ziara yake hiyo ni kuharibika mara kwa mara kwa mashine ya CT-Scan iliyokuwapo awali, ikidaiwa kwamba uharibifu huo umekuwa ukifanywa kwa makusudi ili wagonjwa wakalipie huduma hiyo kwenye hospitali binafsi ambazo, hatimaye, sehemu kidogo ya mapato inawarudia baadhi ya wahusika katika mtandao wa hujuma dhidi ya CT-Scan hiyo ya awali.

Kwa ujumla, katika tiba ya mwanadamu, mashine ya CT-Scan ina umuhimu wake hasa kwa wale wenye matatizo ya ubongo, moyo, tumbo na kifua. Hiyo ndiyo mashine inayoweza kuchunguza kwa ufasaha maeneo hayo ya ugonjwa katika mwili wa binadamu, na kisha mgonjwa kupatiwa tiba husika.

Kwa upande wetu, tunaamini mashine hiyo ambayo haikununuliwa kwa fedha za mkopo bali fedha za kodi ya wananchi, itatunzwa na waendeshaji wake hapo Muhimbili kwa umakini, tena kwa maslahi ya wananchi wote wakiwamo wale ambao hawana uwezo wa kifedha kwenda kutafuta huduma hiyo katika hospitali binafsi kutokana na gharama kubwa zinazotozwa huko.

Ni lazima wataalamu katika Hospitali ya Taifa Muhimbili watambue kwamba Watanzania wanahitaji kuona fahari ya kutibiwa katika hospitali yao ya umma.

Lakini si kwa wataalamu wa Muhimbili pekee, bali hata kwa watendaji wakuu serikalini, nao ni lazima watambue na kuweka kipaumbele katika sekta ya afya, kwamba sekta ya afya sasa inahitaji uwekezaji mkubwa na makini zaidi.

Kwa hiyo, tunashauri hatua hii ya ununuzi wa mashine ya CT-Scan kwa fedha za ndani badala ya mkopo iwe chachu ya kuhakikisha sekta ya afya, hasa katika taasisi za serikali inaimarishwa zaidi, kwa manufaa ya Watanzania wote.

Chanzo: Raia Mwema
 
NA TUSONGE MBELE HAKIKA.

MUNGU IBARIKI TANZANIA
MUNGU MBARIKI RAISI WETU.

AMEN.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom