Tusizunguke mbuyu kuhusu wasiojulikana

Tusizunguke mbuyu kuhusu wasiojulikana

Sexless

JF-Expert Member
Joined
Mar 11, 2017
Posts
27,640
Reaction score
65,112
Kuna watanzania wengi sana waliodhulumiwa uhai, waliojeruhiwa na waliotekwa na kuteswa na hawa WASIOJULIKANA. Swali LA kujiuliza hapa ni kwamba: mbona WAATHIRIKA wote wana mlengo mmoja? Wote ni wakosoaji wa serikali. Kwanini?

Watanzania siyo wajinga.

Kule Rwanda kuna INTERAHAMWE, Burundi kuna MBONERAKULE, Zanzibar kuna MAZOMBI. Makundi yote haya yanafanya kazi kwa mtindo, malengo na nia sawa na iWASIOJULIKANA. Na yote yana kinga dhidi ya mkono wa dola.

Tena hao interahamwe wamaekuwa wakiwafuatilia wapinzani wa PK hata nje ya nchi na kuwaua.

Watanzania siyo wajinga.
Muda utaongea.
 
Word up
IMG_20190728_085033.jpeg
 
Jakaya alikuwa mwelewa amezunguka duniani alijua nini maana ya democracy na namna ya kuongoza watu sio hii mbuzi yenye bichwa ka korosho lilifaa kuwa nyapara la barabara tu, hivi anajua kuwa tumemchoka? Na tumemchoka kweli it's just a matter of time.
duuuh aisee
 
Duuuh, duuuh, duuuuh....

Unaonekana una hasira sana mkubwa......

Msamehe tu rafiki, amekuja na soon or later ataondoka tu.....

Msamaha una nguvu sana kwa ajili ya furaha na amani yako no matter what.....!

Kwa hiyo msamaha siyo kwa ajili yake 100%, isipokuwa ni kwa ajili yako haswaa.....!!
 
Boss Sexless Ukweli mchungu
Tawala na Serikali zote Duniani zina hicho kitengo

Nachojua hicho Kitengo kinatakiwa kifanye kazi zake kwa Usiri mkubwa sana.

Tatizo letu hapa nyumbani, Hiki KItengo ni Dhaifu sana, na kinafanya mambo yake sio kwa Usiri na Low Standard.

Watu kutekwa na kuuwawa hakujaanzia Awamu hii, Hata awamu ya Mwalimu kilikuwepo.

Labda swali tujiulize, Kwanini Awamu hii, Haya Matukio yamekuwa mengi sana na mno?

Je ni kwa sababu wanajulikana kabla ya Mission yao na zao kufanyika?

Je Watu wasiojulikana wanatumia mbinu dhaifu kiasi kwamba wanahisiwa ni wao?

Mbona awamu hii matukio yao yanaripotiwa sana na mno?

Ushauri wangu, Jamhuri inaweza kuwa na Kitengo hichi, lakini kisiwe kinapoteza watu sana na mno.

Siku zote kuua ni Dhambi, Ukiua kwa upanga, nawe utauliwa kwa upanga.

Wanasema, Ukishaanza kutapakaa Damu, hauachi.

Karma is the Bitch.
 
Jakaya alikuwa mwelewa amezunguka duniani alijua nini maana ya democracy na namna ya kuongoza watu sio hii mbuzi yenye bichwa ka korosho lilifaa kuwa nyapara la barabara tu, hivi anajua kuwa tumemchoka? Na tumemchoka kweli it's just a matter of time.
Sema umemchoka baada ya kubnwa kwa sababu tabia zako ovu tunamhitaji sana Magufuli kuliko unavyowaza.
 
Hebu kaangalieni jicho pevu makala kama parueanja la mihadarati na upelelezi wa kifo cha saitoti
 
Labda swali tujiulize, Kwanini Awamu hii, Haya Matukio yamekuwa mengi sana na mno???
Mkuu ni kweli kitengo hiki kipo kwa kila serikali.

Kwann tunalalamikia awamu hii?
Serikali nyingi duniani kitengo kama hiki kinashughulikia watu wanaohatarisha usalama wa taifa kwa kiwango KILICHOKITHIRI.

Na kamwe hutasikia watu wakitamba (kama afanyavyo Musiba) kuwapoteza watu kwa mambo ya hovyo na madogo madogo kama kumkosoa rais ama kuikosoa serikali. Tatizo ni hilo mkuu.

Itafikia mahali mtu akichepuka na hawara wa Musiba anatekwa na kuuawa.
 
Jakaya alikuwa mwelewa amezunguka duniani alijua nini maana ya democracy na namna ya kuongoza watu sio hii mbuzi yenye bichwa ka korosho lilifaa kuwa nyapara la barabara tu, hivi anajua kuwa tumemchoka? Na tumemchoka kweli it's just a matter of time.
Umechoka wewe na familia yako!
 
Hata panya wakiunganisha nguvu zao paka anaweza akawakimbia
Mh! Nyati wenyewe na miguvu yao lakini simba mmoja tu akitaka kumla mmoja wao, wote hukimbia na kusambaratika kutetea nafsi zao. Sembuse panya!
 
Jakaya alikuwa mwelewa amezunguka duniani alijua nini maana ya democracy na namna ya kuongoza watu sio hii mbuzi yenye bichwa ka korosho lilifaa kuwa nyapara la barabara tu, hivi anajua kuwa tumemchoka? Na tumemchoka kweli it's just a matter of time.
Sema umemchoka wewe. Wengine tunamuona ni rais material na tunampenda bila unafiki.
 
Wasiojulikana wamejificha katika kumtanguliza Mungu mbele
 
Huu ujinga wote mbona unajulikana...

Ni sawa na mbuni kujificha kwa kufukia kichwa chake mchangani wakati kiwiliwili chote kipo nje...

Cc: mahondaw
 
Back
Top Bottom