Tathmini ya makabiliano ya CHADEMA na vyombo vya dola tarehe 23 Septemba 2024

Doctor Mama Amon

JF-Expert Member
Mar 30, 2018
2,058
2,623



"Tulia RPC Muliro. Kwani shida iko wapi mpaka unikamate? Shida iko wapi? Watu wanatekwa, watu wanateswa. Watu wanaumizwa. Lazima watu wengine tusimame kuwatetea. Lazima tuseme. Lazima tusikike. Kuna mbinu nyingi za kufanya siasa makini lakini kumwaga damu isiyo na hatia sio miongoni mwake. "

--Freeman Mbowe, 23 Septemba 2024, Magomeni, Dar es Salaam.


Utangulizi

Tangu mwaka 2016 Chadema wanalalamikia watukanaji, watekaji, watesaji na wauaji holela wa wafuasi wao, hasa wale wanaoikosoa serikali, ambapo vijana wengi wafuasi wa Chadema wanalengwa na watu wasiojulikana.

Hivyo, hivi karibuni Chadema walifikia hatua ya kuitisha maandamano ya kupaza sauti dhidi ya utekaji, utesaji na uuaji holela ambao sio sehemu ya utamaduni wa Tanzania ya Nyerere unaoheshimu misingi ya utu, kama tunavyosoma katika Katiba ya nchi (1977).

Katika wito wao Chadema walivituhumu vyombo vya ulinzi na usalama kuhusika katika kuasisi na kutekeleza utamaduni wa kumwaga damu ya wapinzani, kwa kuwa wote waliotekwa, kuteswa na/au kuuwawa ni wale waliotamka ama kwa maneno au kwa vitendo kwamba "siitaki CCM na serikali yake."

Vyombo vya ulinzi na usalama vinasimamiwa na Rais Samia Suluhu Hassan, ambaye anavaa kofia nne kwa mpigo: Ni Mkuu wa serikali, Mkuu wa Nchi, Amiri Jeshi Mkuu, na Mwenyekiti wa CCM inayopingwa na wanaotekwa, kuteswa na kuuwawa.

Kwa kuzingatia muktadha huu sasa nafanya tathmini ili kuonyesha nani mshindi katika makabiliano yanayojadiliwa hapa.

Hali ilivyokuwa siku ya tarehe 23 Sep 2024

Japo Chadema waliitisha maandamano ya umma kupaza sauti ya kupinga umwagajim damu, vyombo vya dola vikaharakisha kujikusanya Dares Salaam na kuziba barabara na mitaa yote ya Dar na hatimaye kufanikiwa kuyakwamisha maandamano.

Viongozi wakuu wa Chadema waliojitokeza barabarani wamekamatwa, wamepelekwa polisi, wamefunguliwa majalada, wamedhaminiwa na kuachiwa kwa dhamana.

Kanuni ya mwenye nguvu ndiye mwenye haki ilionekana kutawala mitaa ya Dar es Salaam tangu tarehe 20 Septemba.

Silaha za kila aina zilionekana kubebwa na watu waliovalia nguo za kipolisi, japo silaha zenyewe hutumiwa na wanajeshi.

Lakini jambo kubwa ni kwamba Freeman Mbowe alitoa kauli thabiti. Kwamba "bado tundai watu wote waliotekwa waachiwe huru, na watu wote waliouwawa miili yao ipatikane." Sikiliza kwa makini video ndogo hapo juu kuhusu tamkjoi zima kabla hajakamatwa.

Uamuzi wa mshindi na mshindwa

Hivyo tunapaswa kujiuliza: nani alishinda katika makabiliano ya Chadema na vyombo vya dola?

Binafsi sioni mshindi, na sote kama Taifa tumepata pigo.

Siyo Chadema, CCM, Polisi, Taifa wala wananchi wa kada fulani walioshinda.

Wote tulishindwa kwa kuwa changamoto zilizosababisha wito wa maandamano hazikutatuliwa.

Tumetumia hela nyingi.

Tumewajaza hofu wapiga kura.

Tumepunguza imani ya wananchi kwa jeshi la polisi na serikali.

Tumeharibu sifa ya kuwa nchi ya kidemokrasia, amani na haki.

Tumejipaka matope mbele ya jumuiya ya kimataifa.

Lakini kubwa zaidi ni kwamba bado tatizo liko pale pale maana waliotekwa bado kupatikana na watekaji hawajafikishwa mahakamani.

Kimsingi, kilichofanywa na vyombo vya dola ni kama kuzika magugu aina ya kwekwe ardhini.

Magugu haya huwa hayaozi. Kuyafukia ardhini ni kuyapa fursa ya kuota upya. Badala ya kutibu tatizo wao wameliahirisha tu.

Tafsiri yangu: Kitendawili cha kuzuia udikteta wa umma kwa kutumia udikteta wa kijeshi

Rais Samia alikula kiapo cha kulinda katiba ya Tanzania (1977), ambayo inasema yafuatayo kuhusu haki ya kujieleza na kukusanyika, kati ya mambo mengine mengi:

"20(1) Kila mtu anastahili kuwa huru, bila ya kuathiri sheriaza nchi, kukutana na watu wengine kwa hiari yake na kwa amani,kuchanganyika na kushirikiana na watu wengine, kutoa mawazo hadharani, na hasa zaidi kuanzisha au kujiunga na vyama aumashirika yaliyoanzishwa kwa madhumuni ya kuhifadhi aukuendeleza imani au maslahi yake au maslahi mengineyo..."
"20(4) Bila ya kuathiri sheria za nchi zinazohusika ni marufuku kwa mtu yeyote kulazimishwa kujiunga na chama chochote aushirika lolote..."

Lakini leo tunaona watu wanaosema kuwa "siitaki CCM na serikali yake" wanateswa kwa kutumia majambia, kama ambavyo mfano wa kutekwa kwa Sativa kunathibitisha.

Tunaona maandamano yanachukuliwa kuwa ni jambo haramu.

Yeye anatamka wazi kuwa "maandamano sio sera yetu" wakati kwa mujibu wa Katiba ya Tanzania maandamano ni sera "yetu" sisi Watanzania kwa kujumuisha wana ccm, wana chadema, wana ACT na kadhalika.

Kwa hiyo swali linazuka: Rais anapotumia kiwakilishi "yetu" anamaannisha yeye kina nani?

Hatimaye, kwa mtu yeyote mdadisi swali kubwa linaloibuliwa na ubabe wa serikali dhidi ya Chadema ni hili hapa:

Hivi maamuzi ya serikali yanaongozwa na nadharia gani na yenye asilia yake wapi?

Tafsiri yangu ya matukio haya ni rahisi na ni kama ifuatavyo.

Intelijensia ya siasa za kimataifa, inanionyesha kwamba, utamaduni mpya wa siasa za kumwaga damu ya wakosoaji wa serikali unaegemea zaidi katika utamaduni wa umwagaji damu kwa kutumia upanga/jambia uliozoeleka kwenye nchi za Kiarabu na Kiislamu huko Mashariki ya Kati.

Hizi ni nchi zenye kusifika zaidfi kwa utawala wa kiimla (Autocracy) badala ya utawala wa kidemokrasia (Democracy) .

Nawaalika wasioona ukweli huu kusoma Kitabu kilichoambatanishwa, yaani Ibrahim Elbadawi and Samir Makdisi (2011), Democracy in the Arab World: Explaining the deficit (London/New York: Routledge)

Kwa mujibu wa kitabu hiki, Waarabu-Waislamu wenye asili yao huko Mashariki ya Kati, ambao kwa sasa ni washauri wakuu wa baadhi ya viongozi wetu wakuu, wanaamini yafuatayo kuhusu uhusiano uliopo kati ya demokrasia na autokrasia:
  • "A backward society cannot but produce a backward socialism and cannot but produce a backward democracy. Therefore, priority must begiven to the revolutionary transformation of that society." (p.21)
  • "Giving freedom to the people could lead to the tyranny of the majority, given the multiple pathologies of Arab (and African) civil society"(p.22)
Nchi hizi zinaamini katika matumizi ya jambia kama mbinu rasmi ya kueneza imani, sera na mikakati yao kwa kuwatisha, kuwateka, kuwatesa na kuwachinja wote wasiokubaliana na imani, sera na mikakati yao.

Ushahidi wa kihistoria upo bayana. Ukweli ni kwamba Mtume Mohamed aliasisi mbinu za kibabe za kueneza imani, sera na mikakati y Uislamu wake katika karne ya saba, yaani mbinu ya kutafuta wafuasi kwa kutumia upanga na jambia.

Historia hii imeandikwa vema na Serge Trifkovic (2002), katika kitabu chake, "The Sword of the Prophet (Boston, MA: Regina Orthodox)."

Maelezo ya Serge Trifkovic (2002) yanaungwa mkono na Robert Goldston (1979:49), katika kitabu chake kiitwacho "The Sword of the Prophet: A History of the Arab World from the Time of Mohammed to the Present Day (Fawcett Crest Books)."

BwanaRobert Goldston (1979:49) anaandika yafuatyayo:

"The prophet Muhammad moved with his followers from Mecca to Medina on the neighboring Arabian Peninsula in 622 A.D./1 A.H. By the end of the 7th century the religion of Islam had spread through conversion at the edge of a sword and military conquest throughout the Middle East and North Africa. By 733, just 100 years after the death of Muhammad, an Islamic empire stretched from India in the east to Spain in the west."

Onwuchekwa Jemie(2009), katika andiko lake, "The Arab quest for Lebensraum in Africa and the challenge to Pan Africanism," anadadavua zaidi kuhusu tatizo hili kwa maneno yafuatayo:

"Arab Expansionism in Africa, 640-1900 AD: How many Africans today wonder how Arabs, whose homeland is the Arabian Peninsula, came to occupy all of supra-Sahara Africa, from the Sinai peninsula across to Morocco’s Atlantic coast? And what they did to the Black Egyptians, Black Berbers and other blacks who were the aborigines of all that expanse of land?
Similarly, Africans need to inquire into why and how an Arab minority has ruled Sudan since 1956? And how did it come about that we hear of Arab tribes in Darfur, Chad and even in Nigeria’s Bornu state?
Until 640 AD, there were no Arab settlers of any kind in all those places. But in that year hungry Arab hordes desperate for plunder and greener pastures charged out of Arabia, flying the flag of their new religion, Islam, and conquered Egypt by 642.
Egypt thereafter became their base for invading and seizing lebensraum all the way west to Morocco and Mauritania, and southward up the Nile...
It should be noted that the core Islamic countries that stretch contiguously from the Maghreb to Pakistan are fragments of the empire that Arabs conquered and ruled from 632 to 1517 when the Turks, under Selim the Grim, conquered Egypt and Syria and extinguished the Arab Abbasid Caliphate. Thus, the core lands of Dar-al-Islam today are a continuation of the Arab Empire.
Just as the Commonwealth is the euphemistic PR name for the enduring British Empire, so too Dar-al-Islam is the euphemistic PR name for the enduring Arab Empire.
In fact Dar-al-Islam is simply the Arab empire in religious camouflage, and the Umma are the Arab citizens/masters while the non-Arab are the subjects of the enduring Arab Empire."

Huu ni ushahidi tosha kuhusu "Utamaduni wa Jambia la Mtume Mohamed" unaotekelezwa nchini Tanzania tangu mwaka 2026 kwa ajili ya kueneza imani, sera na mikakati ya CCM.

Kuna wakati hayati Magufuli alipingwa na umma kwa sababu hii. Bado ni kwa sababi zile zile Chadema wanaipinga serikali ya Rais Samia. Hujambo Lakini sasa kuna ukatili wa ziada umeongezeka chini ya Rais Samia. Hali ni mbaya sana.

Tunakopaswa kwenda baada ya hapa

Lakini mauaji ya raia wasio na hatia katika dola ambayo inaongozwa na Katiba ya kijamhuri na kidemokrasia sio jambo la kufumbia macho kamwe.

Hata wana CCM makini hawakubaliani na umwagaji damu kama mbinu makini ya kisiasa.

Kwa hiyo, sasa maswali kumi ya kimkakati yanazuka na yanapaswa kujadiliwa kwa kina na wajasiriadola wote makini wanaotaka kukomeshwa kwa mauaji Holela:
  1. Katika mtazamo wa kihistoria sisi Watanzania tumetoka wapi, ni kina nani, sio kina nani na kwa nini sisi ni tofauti na mataifa baki? (History: Who are we and where did we come from?)
  2. Kwa sasa tuko katika mazingira gani kama tukifanya Uchambuzi wa NUFU, yaani uchambuzi wa Nguvu, Udhaifu, Fursa na Utisho (SWOT Analysis) dhidi yetu? (Current situation analysis: where are we now in terms of strengths, weaknesses, opportunities and threats analysis?)
  3. Ifikapo Desemba 2024 Sisi kama Taifa tunaka kuendelea kubaki kwenye bonde la utekaji, utesaji na uuaji au kupanda kwenye kilele cha mlima wa uhuru, uzima tele, udugu na ustawi endelevu? (Vision: Where do we want to be by December 2024?)
  4. Kusudi tuweze kutoka hapa na kufika tunakotaka kwenda, tutapitia upande gani na kwa nini? (Strategic orientation: By using our strengths to overcome our weaknesses, defeat threats and seize opportunities, what exactly will we do in order to get where we want to go?)
  5. Ni mbinu gani zitatumika kutekeleza mkakati wetu wa kukomesha utekaji, utesaji, na uuaji wa wakosoaji wa serikali ? (Tactics: How will we get our strategy implemented?)
  6. KIna nani wanapaswa kuhusika katika mkakati huu mpya wa kukomesha utekaji, utesaji, na uuaji wa wakosoaji wa serikali? (Division of labour: Who can and will do which tasks effectively and efficiently?)
  7. Katika mikoa 31, majimbo ya uchaguzi 239, tarafa 570, Kata 3, 956, vijiji 12,333, mitaa 4,269 na vitongoji 66,274 tunahitaji uhamasishaji wa rasilimali mahalia (local resoiurces mobilisation) kiasi gani kwa ajili ya kufanikisha mkakati wetu wa kukomesha utekaji, utesaji, na uuaji wa wakosoaji wa serikali? (Budget: How much resources does our journey require?)
  8. Katika mkakati wetu wa kukomesha utekaji, utesaji, na uuaji wa wakosoaji wa serikali jukumu gani litatekelezwa wakati upi? (Time table/work plan: How long will our journey take?)
  9. Tukifika mwisho wa safari yetu kuna alama gani na tutazitambuaje? (Key performance indicators (KPIs) and strategic review: What are the signs of our destination and how will we know them?)
  10. Tukifika mwisho wa safari salama tuchukue tahadhari gani za kiusalama? (Security: What should be our security management strategies in our bid to sustainably defend of success story?)
Majumuisho

Sasa tujadili bila jaziba. Hatimaye nitafanya majumuisho ya mawazo ya wachangiaji na kuyaweka hapa chini. Kwa wale wasiopenda kuchangia wazi wazi wanitumie maoni kwa njia binafsi via private messages menu hapo juu

 

Attachments

  • IDL-44957 (1).pdf
    2 MB · Views: 6
Unahitaji upinzani thabiti, serious, usio na udini, ukabila, ukanda, dharau kwa Watanzania ndani yake.
Unafikiri mfano hii CDM ikipata madaraka kesho Lissu, Mbowe, Lema, Mrema ndio viongozi wakuu kutakuwa na tofauti yoyote kwa Mtanzania wa kawaida? JPM alileta tofauti kwa Mtanzania wa kawaida mkampinga, mkamtukana, mkamwita mshamba, dikteka uchwara akaamua kuwa dikteta kamili.

Kiufupi CDM haiwezi kuungwa mkono na Watanzania wengi, watapata support ya watoto wa mjini, makabila, dini kadhaa basi.

Inahitajika upinzani mpya utakaoanzishwa na vijana wote wa Kitanzania. Wakipigia rasilimali zao zitumike vizuri, kuondoa kodi, tozo, kandamizi, uwajibikaji serikalini kwenye kila sekta.
 
Unahitaji upinzani thabiti, serious, usio na udini, ukabila, ukanda, dharau kwa Watanzania ndani yake.
Unafikiri mfano hii CDM ikipata madaraka kesho Lissu, Mbowe, Lema, Mrema ndio viongozi wakuu kutakuwa na tofauti yoyote kwa Mtanzania wa kawaida? JPM alileta tofauti kwa Mtanzania wa kawaida mkampinga, mkamtukana, mkamwita mshamba, dikteka uchwara akaamua kuwa dikteta kamili.

Kiufupi CDM haiwezi kuungwa mkono na Watanzania wengi, watapata support ya watoto wa mjini, makabila, dini kadhaa basi.

Inahitajika upinzani mpya utakaoanzishwa na vijana wote wa Kitanzania. Wakipigia rasilimali zao kutumika vizuri, kuondoa kodi, tozo, kandamizi, uwajibikaji serikalini kwenye kila sekta.
Acha unafiki, mngeruhusu halafu tuone kama watu wasingejitokeza ndio mseme.
 
Unahitaji upinzani thabiti, serious, usio na udini, ukabila, ukanda, dharau kwa Watanzania ndani yake.
Unafikiri mfano hii CDM ikipata madaraka kesho Lissu, Mbowe, Lema, Mrema ndio viongozi wakuu kutakuwa na tofauti yoyote kwa Mtanzania wa kawaida? JPM alileta tofauti kwa Mtanzania wa kawaida mkampinga, mkamtukana, mkamwita mshamba, dikteka uchwara akaamua kuwa dikteta kamili.

Kiufupi CDM haiwezi kuungwa mkono na Watanzania wengi, watapata support ya watoto wa mjini, makabila, dini kadhaa basi.

Inahitajika upinzani mpya utakaoanzishwa na vijana wote wa Kitanzania. Wakipigia rasilimali zao zitumike vizuri, kuondoa kodi, tozo, kandamizi, uwajibikaji serikalini kwenye kila sekta.
Unahamisha mjadala! Soma tena andiko la mleta mada.
 
bado hatuna kizazi kilicho tayari as a group kupigania haki.. tuna few individuals wenye huo ujasiri.'
chadema iangalie namna ya kujilinda na kuwalinda viongozi wake pamoja na mpango mpya wa kupambana na ccm ila sio kupitia mobilization ya watu, kwa sasa uwoga, umaskini na kukata tamaa vimewatawala wanachi hvyo kupata mafuriko kama ya zama za kina dr slaa na lowassa ni ngumu.
watu warud chimbo wachore raman upya na waliandae taifa kwa hzo movement posibly kuleta mabadiliko chaguzi za 2030 kuendelea. ila 2025 bado hakuna uwezo wa kubadilisha kitu, given condition ya watawala na ya watawaliwa kwa sasa, angalia misimamo ya bunge, ya mahakama zetu, ya jeshi la polisi, na unyonge wa wanachi, uliochochewa na woga, umaskini, pamoja na unafki/uchawa wa kutisha.
 
Unahitaji upinzani thabiti, serious, usio na udini, ukabila, ukanda, dharau kwa Watanzania ndani yake.
Unafikiri mfano hii CDM ikipata madaraka kesho Lissu, Mbowe, Lema, Mrema ndio viongozi wakuu kutakuwa na tofauti yoyote kwa Mtanzania wa kawaida? JPM alileta tofauti kwa Mtanzania wa kawaida mkampinga, mkamtukana, mkamwita mshamba, dikteka uchwara akaamua kuwa dikteta kamili.

Kiufupi CDM haiwezi kuungwa mkono na Watanzania wengi, watapata support ya watoto wa mjini, makabila, dini kadhaa basi.

Inahitajika upinzani mpya utakaoanzishwa na vijana wote wa Kitanzania. Wakipigia rasilimali zao kutumika vizuri, kuondoa kodi, tozo, kandamizi, uwajibikaji serikalini kwenye kila sekta.
Hakuna watu wenye udini, ukabila na ukanda kama watu ambao wako obsessed na huo udini, ukabila na udini. Hii inaitwa 'psychological projection' - yaani tatizo ulilonalo wewe, lakini unakuwa na tendency ya kuliona kwa wengine. Mfano, mchepukaji anamwonea wivu mke/mumewe. Kwa nini? Kwa sababu anaona udhaifu wake si kwake mwenyewe, bali kwa mtu mwingine. Kwa kusoma uliyoandika hapa, usije na wewe ukawa na hiyo 'psychological projection'.
 
Mbaya zaidi kesi za utekaji waliofanya wenyewe kwa ushahidi wa kimazingira wanataka wawape viongozi wa CDM, shuruba zote wanazopitia bado, maumivu ya misiba na upoteaji wa watu wao, bado mnataka muwape kesi na mnajua fika hawajafanya!

Honestly hakuna atakayewachekea, Ujumbe ni lazima uwafikie kwa namna yeyote. Ikiwemo hiyo adhabu ya kuandamana kwa niaba ya waandamanaji.

Mnapenda mno wanyonge na makondoo.
 
Unahitaji upinzani thabiti, serious, usio na udini, ukabila, ukanda, dharau kwa Watanzania ndani yake.
Unafikiri mfano hii CDM ikipata madaraka kesho Lissu, Mbowe, Lema, Mrema ndio viongozi wakuu kutakuwa na tofauti yoyote kwa Mtanzania wa kawaida? JPM alileta tofauti kwa Mtanzania wa kawaida mkampinga, mkamtukana, mkamwita mshamba, dikteka uchwara akaamua kuwa dikteta kamili.

Kiufupi CDM haiwezi kuungwa mkono na Watanzania wengi, watapata support ya watoto wa mjini, makabila, dini kadhaa basi.

Inahitajika upinzani mpya utakaoanzishwa na vijana wote wa Kitanzania. Wakipigia rasilimali zao kutumika vizuri, kuondoa kodi, tozo, kandamizi, uwajibikaji serikalini kwenye kila sekta.
Lugha laini na tamu inayofurahiwa kutamkwa ki CCM,yaani ungeongeza neno kuwategemea CCM waendelee kutawala hadi vijana watakaoletwa toka peponi,lini sijui wewe na mimi.Mawazo ya ki CCM ya kuwakatisha tamaa watanganyika.wabaki kujadili watu badala ya kujenga mfumo wa UPINZANI,kama hivyo,Mbowe,Lissu wabaki peke yao,Mawazo ya Shetani mwenye husuda kwa wapinzani mpenda CCM huyu.
 
"Tulia RPC Muliro. Kwani shida iko wapi mpaka unikamate? Shida iko wapi? Watu wanatekwa, watu wanateswa. Watu wanaumizwa. Lazima watu wengine tuseme kuwatetea. Lazima tuseme. Lazima tusikike."--Freeman Mbowe, 23 Septemba 2024, Magomeni.

Chadema wanalalamikia watekaji, watesaji na wauaji holela wa wafuasi wao wanaoikosoa serikali, ambapo sasa vijana wengi wafuasi wa Chadema wanalengwa na watu wasiojulikana.

Hivyo, Chadema waliitisha maandamano ya kupaza sauti dhidi ya utekaji, utesaji na uuaji holela sio sehemu ya utamaduni wa Tanzania ya Nyerere unaoheshimu misingi ya utu, kama tunavyosoma katika Katiba ya nchi (1977).

Chadema wanavituhumu vyombo vya ulinzi na usalama kuhusika katika kuasisi na kutekeleza utamaduni wa kumwaga damu ya wapinzani, kwa kuwa wote waliotekwa, kuteswa na/au kuuwawa ni wale waliotamka ama kwa maneno au kwa vitendo kwamba "siitaki CCM na serikali yake."

Vyombo hivyo vinasimamiwa na Rais Samia, ambaye ni Mkuu wa serikali, Mkuu wa Nchi, Amiri Jeshi Mkuu, na Mwenyekiti wa CCM inayopingwa na wanaotekwa, kuteswa na kuuwawa.

Sasa ni wazi kwamba, utamaduni huu mpya unaegemea zaidi katika utamaduni wa umwagaji damu uliozoeleka kwenye nchi za Kiarabu na Kiislamu huko Mashariki ya Kati, nchi zenye kusifika zaidfi kwa AUTOCRTACY badala ya DEMPCRACY (Tazaman Kitabu kilichoambatanishwa).

Nchi hizi zinazoamini katika matumizi ya jambia kama mbinu rasmi ya kueneza imani, sera na mikakati yao kwa kutumia upanga kuwateka, kuwatesa na kuwachinja wote wasiokubaliana na imani, sera na mikakati yao.

Kuna wakati hayati Magufuli alipingwa na umma kwa sababu hii. Bado ni katika mazingira haya, Chadema wanaipinga serikali ya Rais Samia

Hivyo Chadema waliitisha maandamano kupaza sauti ya kupinga. Lakini vyombo vya dola vikaharakisha kujikusanya Dares Salaam na kukaziba barabara na mitaa yote ya Dar na hatimaye kufanikiwa kuyakwamisha maandamano.

Viongozi wakuu wa Chadema waliojitokeza barabarani wamekamatwa, wamepelekwa polisi, wamefunguliwa majalada, wamedhaminiwa na kuachiwa kwa dhamana.

Maswali yanazuka:
  • Tangu mwanzo sisi kama Taifa tulitaka kwenda kwenye utekaji, utesaji na uuaji?
  • Katika safari yetu ya kuelekea kwenye ndoto kuu, leo bado tuko kwenye barabara tuliyokubaliana kupitia?
  • Kama jawabu ni hapana tumefikaje hapa kwenye bonde la utekaji, utesaji na uuaji wa raia wasio na hatia, yaani chanzo cha mkwamo huu ni nini?
  • Kuna njia tatu za kutatua matatizo, additive problem solving strategy, subtractive problem solving strategy and problem resolving strategy.
    • Je, kuna kitu kinahitajika lakini hakipo mahali pake na kinahitajika ili kiwekwe hii ikiwa ni additive problem solving strategy?
    • Kuna kitu hakihitajiki lakini kiko mahali fulani na hivyo inabidi kiondelewe hii ikiwa ni subtractive problem solving strategy?
    • Au labda badala ya additive and subtractive problem solving strategies kuna njia ya tatu yaani problem resolving strategy inayoweza kutuvusha katika bonde la utekaji, utesaji na uuaji ulio kinyume na mila na desturi za Wabantu wa Tanzania?
  • Tunajikwamuaje na kwenda tunakopaswa kwenda?
  • KIna nani wanapaswa kuhusika katika mkakati huu mpya na kwa nini?
Tujadili bila jaziba.
acha upotoshaji my lovely Mom,
sio maandamano ya kupaza sauti ni maandamano ya Samia must Go, ya kuvuruga umoja, amani, utulivu na demokrasia ya Tanzania, kitu ambacho hakikubaliki na kisingeweza kuruhusiwa na serikali yoyote duniani, mbona hilo liko wazi kabisa na linafahamika ulimwenguni kote 🐒

Samia Must Go, ilibadilishwa saa ngapi, na kwanini, hata ikawa maandamano ya kupaza sauti kama unavyopotosha?

kwamba chadema wanatikisa kiberiti, au wanajaribu kuonja sumu kwa ulimi? labda wakajaribu nchi jirani sio Tanzania..

Umoja, amani na utulivu wa wanainchi Tanzania utalindwa kwa nguvu zote na gharama yoyote ile 🐒
 
Unahamisha mjadala! Soma tena andiko la mleta mada.

Mjadala ni mpana, kimsingi ni kwanini maandamo hayakufanikiwa. Sababu zinaweza kuwa nyingi, zaidi, nyingine kuliko mtoa mada alivyouweka very narrow from her own perspective. Tunaweza kutoa perspectives nyingine ambazo hakuzifikiria.
 
Chadema wanalalamikia watekaji, watesaji na wauaji holela wa wafuasi wao wanaoikosoa serikali, ambapo sasa vijana wengi wafuasi wa Chadema wanalengwa na watu wasiojulikana.

Hivyo Chadema waliitisha maandamano kupaza sauti ya kupinga. Lakini vyombo vya dola vikaharakisha kujikusanya Dares Salaam na kukaziba barabara na mitaa yote ya Dar na hatimaye kufanikiwa kuyakwamisha maandamano.

Tujadili bila jaziba.
Asante sana, hakika wewe ni baraka sana hapa jf kwasababu watu wenye uwezo wa kufanya tathmini ni wachache na wa kutafuta kwa tochi!.
Ubarikiwe sana.
P
 
Mama Amon, ngoja waje humu machawa wakupe jina la mwanaChadema, wakati sote tunajua humu wewe si mwanaChadema.

Inahitaji mtanzania wa kawaida mwenye damu nyekundu kutambua kuwa mambo hayako sawa, na ni mabaya na timing ni mbovu!

Wana CCM wenye akili wamejificha wapi aisee?
 
Mbaya zaidi kesi za utekaji waliofanya wenyewe kwa ushahidi wa kimazingira wanataka wawape viongozi wa CDM, shuruba zote wanazopigia bado, maumivu ya misiba na upoteaji wa watu wao, bado mnataka muwape kesi na mnajua fika hawajafanya!

Honestly hakuna atakayewachekea, Ujumbe ni lazima uwafikie kwa namna yeyote. Ikiwemo hiyo adhabu ya kuandamana kwa niaba ya waandamanaji.

Mnapenda mno wanyonge na makondoo.
 
Lugha laini na tamu inayofurahiwa kutamkwa ki CCM,yaani ungeongeza neno kuwategemea CCM waendelee kutawala hadi vijana watakaoletwa toka peponi,lini sijui wewe na mimi.Mawazo ya ki CCM ya kuwakatisha tamaa watanganyika.wabaki kujadili watu badala ya kujenga mfumo wa UPINZANI,kama hivyo,Mbowe,Lissu wabaki peke yao,Mawazo ya Shetani mwenye husuda kwa wapinzani mpenda CCM huyu.

Wewe hujitambui unamuona mtu kama Ibrahim Traore wa Burkina Faso, vijana wa Kenya, unafikiri vijana wa Kenya wangekubali kuongoozwa na Lowassa, kusifia uongozi dhalimu wa chama tawala kama maneno mliyokuwa mnasema juzi mama anaupigwa mwingi, tatizo ni sukuma gang.

Unafikiri kijana kama Traore akitokea Tanzania hataungwa mkono na Watanzania wengi? Vijana wa Bangladesh, Sri Lanka walikuwa wanagawanya nchi zao. Jifunzeni kutokana na maandamano na nchi, vijana waliofanikisha maandamano kwenye nchi zao.

Naweza kurudi nyuma zaidi hadi French revolution, USA independence na Haiti revolution, Cromwell in Revolution in England. Hata Mwalimu Nyerere alishilikisha kila mtu, kabila, dini, Kanda, kupambana na wakoloni. Mjipime.
 
Back
Top Bottom