Tusiwe na haraka!

Kibirizi

JF-Expert Member
Feb 19, 2011
604
146
Bwana mmoja ambaye alikuwa na wivu sana wa mapenzi kwa mke wake siku moja aliaibika.Bwana huyu alitoka safari na kurudi nyumbani, alipofika nyumbani moja moja alienda chumbani kwake kwa lengo la kufumania mke wake, alipofika chumbani aliona miguu minne imelala kitandani kwake yaani sehemu iliyobaki imefunikwa na shuka gubi gubi, bila kufikiri, haraka haraka akachukua kitu kizito na kupiga/kutwanga miguu hiyo minne na kutoka chumbani hadi sebuleni, alipofika sebuleni akamkuta mke wake amekaa, akashangaa kumwona sebuleni, yule mke wake akamwambia mume wangu wazazi wako wamekuja kutoka kijijini kwenu sasa waliniomba wapumzike nikawapisha chumbani. Yule bwana alipoteza fahamu pale pale kwani ameshaua wazazi wake.
 
Back
Top Bottom