Tusiwazibe midomo wapotoshaji, bali tufunge masikio yetu na kuwapuuza

KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
5,313
2,000
"I might disapprove of what you say, but I will defend to the death your right to say it"

Siafiki mengi yanayosemwa na wapotoshaji.., lakini sifurahii kuwaziba midomo so called wapotoshaji, sababu kama tukiwaziba midomo leo na kweli wamepotosha uzibaji midomo huo huo unaweza kutumika kesho kuziba wasema ukweli.

Binafsi naamini kabisa kila mtu ana haki ya kuwa Mpuuzi ila wale wanaomzunguka ndio inabidi wawe na busara zaidi ili wasiendeshwe wala kumfuata mpuuzi.

Ifike wakati kila mtu aendeshwe kwa fikra na busara zake, na sio utashi wa Jirani yake. Ifike wakati wanajamii wenyewe ndio wabishe na kupinga kwa hoja au kumpuuza mwendawazimu na sio kuomba mamlaka iwafunge midomo wale so called wendawazimu.
 
Yoda

JF-Expert Member
Jul 22, 2018
12,811
2,000
Ikifika mahali kila mtu akawa anaendeshwa na utashi na busara zake badala ya sayansi na common sense tutakuwa taifa la waliovurugikiwa.
 
KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
5,313
2,000
Ikifika mahali kila mtu akawa anaendeshwa na utashi na busara zake badala ya sayansi na common sense tutakuwa taifa la waliovurugikiwa.
Sayansi na Common Sense sio Busara na Utashi wa Mtu ? Mtu anayeendeshwa kwa fikra lazima atafikiri na atakuwa led na logic..., hauwezi kuwa mtu wa kufikiri alafu ukaendekeza vitu illogical...
 
EINSTEIN112

JF-Expert Member
Oct 26, 2018
13,875
2,000
Saivi ukianzisha uzi kupinga chanjo wanaufuta. Najiuliza so tujadili kukubaliana tu na chanjo na si vinginevyo??

Siku hizi Jf imekuwa wakala wa Serekali, mwanzoni tulihisi ni kwa sababu ya JPM ila naona mwendo ni ule ule
 
macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
14,755
2,000
"I might disapprove of what you say, but I will defend to the death your right to say it"

Siafiki mengi yanayosemwa na wapotoshaji.., lakini sifurahii kuwaziba midomo so called wapotoshaji, sababu kama tukiwaziba midomo leo na kweli wamepotosha uzibaji midomo huo huo unaweza kutumika kesho kuziba wasema ukweli.

Binafsi naamini kabisa kila mtu ana haki ya kuwa Mpuuzi ila wale wanaomzunguka ndio inabidi wawe na busara zaidi ili wasiendeshwe wala kumfuata mpuuzi.

Ifike wakati kila mtu aendeshwe kwa fikra na busara zake, na sio utashi wa Jirani yake. Ifike wakati wanajamii wenyewe ndio wabishe na kupinga kwa hoja au kumpuuza mwendawazimu na sio kuomba mamlaka iwafunge midomo wale so called wendawazimu.
Serikali yoyote iliyo makini inaadhibu waposhaji na kesho haiwezi kuadhibu wasema ukweli. Nazungumzia serikali makini yenye watu wenye akili na vision. Ukiona serikali inafuata theory ulisema basi hiyo serikali haifai
 
KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
5,313
2,000
Serikali yoyote iliyo makini inaadhibu waposhaji na kesho haiwezi kuadhibu wasema ukweli. Nazungumzia serikali makini yenye watu wenye akili na vision. Ukiona serikali inafuata theory ulisema basi hiyo serikali haifai
Serikali au sehemu yoyote yenye freedom of speech ndio nayopenda kuishi mimi..., Ukweli na Upotoshaji unaweza ukawa subjective..., ila point yangu kubwa ni kwamba tusisubiri serikali itoe definition ya ukweli na upotoshaji bali sisi kwa fikra zetu tunaopotoshwa tuweze kupambanua mbivu na mbichi...

Tatizo tukitumia nguvu kwa kuwaziba watu midogo amini nakwambia hii inaweza kuleta precedence ya kuwaziba wote wenye sauti kwa definition ya anayekamata..., sababu ndio atachagua definition.

Tunajua wenyewe na tumeona.., nyekundu na njano ya jana leo inaitwa nyeusi....
 
Niza doyi

JF-Expert Member
Dec 10, 2019
1,250

Wakijaribu kuwaziba kwa nguvu hawa wanaitwa wapotoshaji ndo watawapa nguvu,dawa ni kuwapuuza,Kama Kikwete alivyompuuza Magufuli alipolazima Jengo la Tanesco Ubungo libomolewa. akidai JK asimamie sheria aliyoisaini mwenyewe JK.
Kaupepo kakapita.
 
Au tukimziba mpotoshaji wa leo kuhusu mabeberu kutuwekea Corona kwenye Barakoa..., Je akim-qoute the president aliyetoka kwamba ndio proof yake..., si hapo tutakuwa tunabishana na vichaa kwa kutumia kodi za wananchi ?

Ingawa nadhani kuna njia nyingine badala ya nchi / serikali / kodi zetu kutumika na kupotezeana muda na watu kama hawa mwananchi individually anaweza akajitokeza na kumfungulia mashitaka mpotoshaji (kwamba labda kaharibu soko langu kwa slander na kuongea vitu ambavyo sio kweli) yaani ku-deal nao individually na sio kama taifa...
 
macho_mdiliko

JF-Expert Member
Mar 10, 2008
14,755
2,000
Serikali au sehemu yoyote yenye freedom of speech ndio nayopenda kuishi mimi..., Ukweli na Upotoshaji unaweza ukawa subjective..., ila point yangu kubwa ni kwamba tusisubiri serikali itoe definition ya ukweli na upotoshaji bali sisi kwa fikra zetu tunaopotoshwa tuweze kupambanua mbivu na mbichi...

Tatizo tukitumia nguvu kwa kuwaziba watu midogo amini nakwambia hii inaweza kuleta precedence ya kuwaziba wote wenye sauti kwa definition ya anayekamata..., sababu ndio atachagua definition.

Tunajua wenyewe na tumeona.., nyekundu na njano ya jana leo inaitwa nyeusi....
Nimekuelewa. Lakini Gwajima kuchukuwa hatua ni jambo la muhimu. Sisemi polisi wamkamate au apelekwe mahakamani la hasha. Chama chake kimchukilie hatua kwa kwenda kinyume na kanini zake. Anyang'anywe ubunge ili asiendelee kuwa nadani ya chama ambacho haamini viongozi wake. Mimi sina tatizo na yeye kutumia kanisa lake kupotosha. Nchi zilizo makini mwanachama wa chama cha kisiasa akifanya ndivyo sivyo anachukuliwa hatua na chama. Nikupe mfano: Nilikuwa Finland kipindi fulani akatokea mbunge wa chama akatoa comments zinazoashiria ubaguzi wa rangi i.e. kuwabagua wageni na kusema ni wahalifu. Hii kwa kawaida ni freedom of speech na ametoa maoni yake. Kilichofuatia ni chama chake kumtenga na kumuondoa kwenye chama kwa sababu alikwenda kinyume na msimamo wa chama. Hivyo mkuu nimekuelewa sana, na hata USA sasa hivi na nchi nyingi tu kuna watu wanatoa maoni ya kukandia chanjo kama Gwajima, na hawachukiliwi hatua za kisheria, lakini kama wanakinzana na sehemu zao wanazoziongoza inabidi waondoke huko kwanza.
 
Kelvin X

JF-Expert Member
Jun 28, 2011
1,260
2,000
Serikali au sehemu yoyote yenye freedom of speech ndio nayopenda kuishi mimi..., Ukweli na Upotoshaji unaweza ukawa subjective..., ila point yangu kubwa ni kwamba tusisubiri serikali itoe definition ya ukweli na upotoshaji bali sisi kwa fikra zetu tunaopotoshwa tuweze kupambanua mbivu na mbichi...

Tatizo tukitumia nguvu kwa kuwaziba watu midogo amini nakwambia hii inaweza kuleta precedence ya kuwaziba wote wenye sauti kwa definition ya anayekamata..., sababu ndio atachagua definition.

Tunajua wenyewe na tumeona.., nyekundu na njano ya jana leo inaitwa nyeusi....
Tatizo serekali lazima isimamie wale wenye uwelewa mdogo wasi bebwe na upepo wa conspiracy, ambao amini usiamini ni wengi
 
KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
5,313
2,000
Tatizo serekali lazima isimamie wale wenye uwelewa mdogo wasi bebwe na upepo wa conspiracy, ambao amini usiamini ni wengi
Naam ni kweli ila tatizo la kufanya hivyo unaweza ukawa unampiga chura teke... (kwamba si unaona wameniziba mdomo kwa mabavu) wamelipwa ili wanifunge....

Ingawa am sure legally uwezo wanao na sidhani kama kibali chake cha kutangaza neno linampa mamlaka ya kutoa elimu ya kitaaluma (hayo anayosema hapa angeyasema Bungeni)
 
Niza doyi

JF-Expert Member
Dec 10, 2019
1,250
2,000
Au tukimziba mpotoshaji wa leo kuhusu mabeberu kutuwekea Corona kwenye Barakoa..., Je akim-qoute the president aliyetoka kwamba ndio proof yake..., si hapo tutakuwa tunabishana na vichaa kwa kutumia kodi za wananchi ?

Ingawa nadhani kuna njia nyingine badala ya nchi / serikali / kodi zetu kutumika na kupotezeana muda na watu kama hawa mwananchi individually anaweza akajitokeza na kumfungulia mashitaka mpotoshaji (kwamba labda kaharibu soko langu kwa slander na kuongea vitu ambavyo sio kweli) yaani ku-deal nao individually na sio kama taifa...
Individual? Nani ajaribu kumfunga paka kengere?
 
Nyumisi

JF-Expert Member
Nov 10, 2010
7,129
2,000
Unaweza kujiona mjanja kumbe wewe ndo mpotoshaji, hata Galileo Galilei alivyosema dunia ni duara aliitwa mpotoshaji na akaishia kunyongwa...
 
Igombe fisherman

JF-Expert Member
Apr 28, 2017
1,357
2,000
Chanjo yenyewe niyakudunga watu milioni moja. Sasa wote tukiunga mkono watu milion 60 itatosha kweli. Inatakiwa watu kama akina gwajima wawepo ili chanjo itoshe kwa wanaoihitaji. Tunahitaji watu zaidi ya 1000 kama akina gwajima na kila mtu mawazo yake yafuatwe na watu zaidi ya 50,000 ili watu zaidi ya milion 50 wakatae chanjo. Hapo ndo itatosha kwa waliobaki. Sasa wasipokuwepo hao watu tutahitaji zaidi ya ndege 60 kama zile kuleta chanjo ya kutosha watu wote. Mi naona gwajima nimfano wa kuigwa na wana ccm wengine 999 ndo tunafanikiwa
 
KeyserSoze

JF-Expert Member
Feb 26, 2014
5,313
2,000
Unaweza kujiona mjanja kumbe wewe ndo mpotoshaji, hata Galileo Galilei alivyosema dunia ni duara aliitwa mpotoshaji na akaishia kunyongwa...
Alisema tu au alikuja na concrete evidence..., uzuri wa Sayansi hata wewe leo ukitaka kusema dunia ni kama bakuli ukaja na concrete evidence na vithibitisho ni ruksa wala haina shida (tena unakaribishwa ili uendelee kuleta mchango wako katika jamii)

Tofauti na kuja na kutoa hadithi kwamba hiki hakipo hivi bila kuwa na vithibitisho ambavyo vipo backed na up..., huwezi tu ukaamka asubuhi na kuanza kuwaambia watu mchele wa Kyela una sumu bila kuthibitisha; lakini kama ukionyesha watu kadhaa wamekufa au wamepata tatizo ukawashirikisha wataalamu wa sekta husika ili uchunguzi ufanyike hapo ndio utakuwa umefanya kazi yako kwa ufanisi kama mwanajamii bila kuleta taharuki...
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom