Logikos
JF-Expert Member
- Feb 26, 2014
- 12,436
- 19,452
"I might disapprove of what you say, but I will defend to the death your right to say it"
Siafiki mengi yanayosemwa na wapotoshaji.., lakini sifurahii kuwaziba midomo so called wapotoshaji, sababu kama tukiwaziba midomo leo na kweli wamepotosha uzibaji midomo huo huo unaweza kutumika kesho kuziba wasema ukweli.
Binafsi naamini kabisa kila mtu ana haki ya kuwa Mpuuzi ila wale wanaomzunguka ndio inabidi wawe na busara zaidi ili wasiendeshwe wala kumfuata mpuuzi.
Ifike wakati kila mtu aendeshwe kwa fikra na busara zake, na sio utashi wa Jirani yake. Ifike wakati wanajamii wenyewe ndio wabishe na kupinga kwa hoja au kumpuuza mwendawazimu na sio kuomba mamlaka iwafunge midomo wale so called wendawazimu.