Tusiwanyanyapae wenye maambukizi

Tusiwanyanyapae wenye maambukizi

unkown_member

Member
Joined
Jan 31, 2018
Posts
27
Reaction score
32
Katika pita pita zangu nikiwa kama kidume rijali mwaka jana mwezi wa sita nilitapa ajali! Nilipata bahati mbaya ya condom kupasuka basi baada ya kupasuka nikamaliza kula tunda nikamwambia bibie tukapime nikiwaza ili nianze kugegeda kavu kavu!

Looh kumbe bibie ameungua (ni anaishi na maambukizi).

Nilichanganikiwa nikawaelezea manesi pale nikapewa mzigo wa PEP dose ya siku 28!!

Namshukuru MUNGU juzi( 15/4/2018) nimepima kwa mara ya mwisho majibu ni negative!

Yatokanayo!!
1. Kipindi hicho kilikuwa kigumu saana kwa kweli. Sikumsimulia mtu yeyote ilikuwa siri yangu. Nilikuwa mtu mwenye mawazo saana!

2. Dawa hizo za PEP ni kali mno zina nguvu mno na pia zinalevya saana ukiacha ndoto za mawenge na njaa!!

Hitimisho.
1. Kutoka mwaka jana mwezi sita sijawahi kuwa na hamu ya Papuchi tena. Tusipime kwa macho wakuu!! Yaani yule binti ukimwona kwa macho hautoamini ana maambukizi!! Ni mnene, pia ana chura wa kutisha!!
Tusipime kwa macho mazee!!

2. Wenye maambukizi ya VVU ni watu waliopo katika wakati mgumu mno!! Kipindi hicho natumia PEP nilipata funzo zuri! Niwaombe kuwa watu hawa wenye VVU tuwapende kwani wanahitaji upendo na faraja wa dhati. Tuwapende na tuwasaidie.

3. Tusiwanyanyapae hata kidogo
 
Natamani kungelikuwa na namna ya kutambua asili za maambukizi kwa kila mwathirika.
Binadamu kama huyu!! Anaamua kupotezea watoto kama hawa

ANAONA UMBWA UNATHAMANI KULIKO WATOTO NA FAMMILIA YENYE AMANI NA MAONO.

Hakika ni muuaji!.

MAMA YAO ASINGKUWA NA UWEZO NA UFAHAMU, WANGEKUAJE? AKILI ZA HAYO MAMALAYA YAKE, ZINAISHIA KWENYE FEDHA TU. MWANAMKE MPUMBAVU ANADHANI FEDHA INATOSHA KULEA WATOTO. ZARINA ANAJUA MAHITAJI YA WATOTO ZAIDI YA FEDHA.

HUYU KIJANA NI MPUNVUBAVU SANA ASIYEJITAMBUA NA MAISHA YAKE NI AFADHALI YA NGUFURWE.
 
Mmh. Kipindi cha nyuma ndio Ukimwi ulikuwa unaogopwa ila now days mmh.

Umekuwa ugonjwa wa kawaida na watu hawana habari, wala hofu nao nadhani moja ya sababu ni hizi dawa za kuongeza makali hivyo kila anayempima mwenzie kwa kutumia macho anamuona ni mzima.

Ni kumi kwa mmoja wenye kuwaza kupima kabla ya kufanya yale mambo yetu walio wengi wanaamini hiyo mipira kwa 100% na kupimana kwa macho.
 
Asee yaani unaweza ukawa mjanja lakn usiombe kabisa yakakukuta! Sa hv sitaki mchezo kabisaa!! Hata Papuchi siitaki
 
Hakuna ugonjwa wa ukimwi, mtu yeyote anaugua pindi kinga yake ya mwili ikiwa chini, hivyo msipime ukimwi mkiwa mnaumwa maradhi ya kuambukizwa kama malaria au kipindupindu maana kipimo cha HIV huangalia kinga ya mwili na sio kirusi
 
Natamani kungelikuwa na namna ya kutambua asili za maambukizi.

Binadamu kama huyu!!
1. Kufanya tendo la Ndoa na aliyeathirika bila kinga.

2. Mama na mtoto kipindi cha kujifungua endapo mama ni muathirika, hapa inatokea wakati mama na mtoto wanatenganishwa na damu yao ikichanganyikana wakati Umbilical cord inakatwa.

3. Kupokea Damu/Kuongezewa Damu yenye VVU.

4. Kushirikiana vifaa vyenye ncha kali mfano sindano, kiwembe na aliyeathirika.

5. N.k

NB: Sio wote walioathirika ni kutokana na mapenzi yasiyo salama au kuwa na wapenzi wengi kama tunavyojiaminisha miongoni mwa wengi siku hizi.
 
Hakuna ugonjwa wa ukimwi, mtu yeyote anaugua pindi kinga yake ya mwili ikiwa chini, hivyo msipime ukimwi mkiwa mnaumwa maradhi ya kuambukizwa kama malaria au kipindupindu maana kipimo cha HIV huangalia kinga ya mwili na sio kirusi
Kinapima antibodies Specific kwa hHIV
 
Back
Top Bottom