Tusiwalaumu akina Makonda, Chalamila, Hapi, Ole Sabaya na wengineo

AbuuMaryam

JF-Expert Member
Dec 26, 2015
2,537
4,519
Unajua watu tunatofautiana perceptions. Ndio maana kuna tafsiri mbalimbali za maendeleo.

Kwa sababu inategemea na point of view ya mtu.

Kwahiyo utendaji wa mtu inategemea mnategemea nini kwenye utendaji wake.

Ukiangalia utendaji kazi wa Makonda, Chalamila yule wa Katavi kuloga watu wapige kura na wengine kama hak. Unaweza ukasema katika watendaji hovyo kabisa ni hao.

Na wengi tunamuona anthony mtaka ndio kiongozi bora. Kweli kabisa kwenye macho yetu.

Lakini kwenye macho ya aliyewaajiri ni tofauti kabisa. Yaani vice versa.

Angalia interview yoyote ya makonda na wenzake akina muro...Haijawahi tokea wasiseme neno bila kumtaja boss wao. Yaani boss wao ndio mungu wao.

Na hicho boss wao ndio anapenda. Viongozi ambao watamsifia na kumuacha kila kitu afanye yeye...Ndio maana hata ccm wameliona hilo...Na ndio maana wanafanya hivyo...Sio kwamba hawaoni makosa yoyote.La hasha Ila ndio wanacheza na mziki wa mkuu wao.

Kwahiyo mkitaka mkune akili ya mzee ni mumsifie na mumtukuze tu mtaona mambo mengi mazuri...Ambalo wengi wengi ambao hatuna wa kumtukuza zaidi ya allah tu na mitume wake.

Hamjawahi jiuliza kwanini kwa utendaji bora wa mtaka kwanini asimpromote...Au asimwamishe kwenye mikoa yenye changamoto kama dar es salaam. Na huyu aliyeko huko dar akapewa kazi nyingine kwa mfano ile kazi ya msemaji wa serikali...Hio ndio inamfaa sana.

Kwahiyo tusiwalaumu hawa viongozi wanaofanya blandaz...Hizo blandaz ni dhahabu mbele ya macho ya boss wao.

Wanacheza kulingana na beat ya boss wao.

Ukiona tbc wanasifia tu ujue ndio boss anataka hivyo.

Ukiona bungeni wanasifia tu.

Ukiona wanaoitwa viongozi wa dini wanatukuza...Ujue ndio boss anataka hivyo.

Ukiona makongamano ya sifa na utukufu...Ndio boss anapenda hivyo.

Tusiwalaumu.

Wallaaahi, Mtu anayependa sifa na utukufu hivi...Atafikia level za firauni hivi karibuni kujiita mungu kabisa.
 
Hakika uzima wa milele tumeujaalia kwa wale ambao hawapend na hawataki ukubwa wala kutukuzwa na hakika mwisho mwema wataupata wale wenye kumcha kwel Allah
 
Umenena vyema ndugu yangu,huyu bwana anapenda kuhusudiwa,kusifiwa na kuabudiwa.Ukimsifu na kumsujudia tayari cheo unalamba na hata ukivurunda haoni. Chochote.Ndoo maana anatoa kauli ya dharau kuwa haoni mtu yeyote mwenye utimam wa kuchukua nchi na kufanya anayoyafanya.Huyu jamaa ana kiburi sana na dharau kubwa.Anahisi yeye ndoo wa kwanza duniani kuwa rais, sijui angetawala nchi kubwa kiuchumi kama Urusi,Amerika Japan au China sijui ingekuwaje
 
Enda na beat usiharibu pozi hatuwezi cheza twanga pepeta huku tunamskia juma nature
 
Unajua watu tunatofautiana perceptions. Ndio maana kuna tafsiri mbalimbali za maendeleo.

Kwa sababu inategemea na point of view ya mtu.

Kwahiyo utendaji wa mtu inategemea mnategemea nini kwenye utendaji wake.

Ukiangalia utendaji kazi wa Makonda, Chalamila yule wa Katavi kuloga watu wapige kura na wengine kama hak. Unaweza ukasema katika watendaji hovyo kabisa ni hao.

Na wengi tunamuona anthony mtaka ndio kiongozi bora. Kweli kabisa kwenye macho yetu.

Lakini kwenye macho ya aliyewaajiri ni tofauti kabisa. Yaani vice versa.

Angalia interview yoyote ya makonda na wenzake akina muro...Haijawahi tokea wasiseme neno bila kumtaja boss wao. Yaani boss wao ndio mungu wao.

Na hicho boss wao ndio anapenda. Viongozi ambao watamsifia na kumuacha kila kitu afanye yeye...Ndio maana hata ccm wameliona hilo...Na ndio maana wanafanya hivyo...Sio kwamba hawaoni makosa yoyote.La hasha Ila ndio wanacheza na mziki wa mkuu wao.

Kwahiyo mkitaka mkune akili ya mzee ni mumsifie na mumtukuze tu mtaona mambo mengi mazuri...Ambalo wengi wengi ambao hatuna wa kumtukuza zaidi ya allah tu na mitume wake.

Hamjawahi jiuliza kwanini kwa utendaji bora wa mtaka kwanini asimpromote...Au asimwamishe kwenye mikoa yenye changamoto kama dar es salaam. Na huyu aliyeko huko dar akapewa kazi nyingine kwa mfano ile kazi ya msemaji wa serikali...Hio ndio inamfaa sana.

Kwahiyo tusiwalaumu hawa viongozi wanaofanya blandaz...Hizo blandaz ni dhahabu mbele ya macho ya boss wao.

Wanacheza kulingana na beat ya boss wao.

Ukiona tbc wanasifia tu ujue ndio boss anataka hivyo.

Ukiona bungeni wanasifia tu.

Ukiona wanaoitwa viongozi wa dini wanatukuza...Ujue ndio boss anataka hivyo.

Ukiona makongamano ya sifa na utukufu...Ndio boss anapenda hivyo.

Tusiwalaumu.

Wallaaahi, Mtu anayependa sifa na utukufu hivi...Atafikia level za firauni hivi karibuni kujiita mungu kabisa.
Wakati mwingine ndiyo hasa taswila ya elimu, akili na utashi wao katika kupambana na changamoto za maisha.
 
Umenena vyema ndugu yangu,huyu bwana anapenda kuhusudiwa,kusifiwa na kuabudiwa.Ukimsifu na kumsujudia tayari cheo unalamba na hata ukivurunda haoni. Chochote.Ndoo maana anatoa kauli ya dharau kuwa haoni mtu yeyote mwenye utimam wa kuchukua nchi na kufanya anayoyafanya.Huyu jamaa ana kiburi sana na dharau kubwa.Anahisi yeye ndoo wa kwanza duniani kuwa rais, sijui angetawala nchi kubwa kiuchumi kama Urusi,Amerika Japan au China sijui ingekuwaje
Mwanzoni nilidhani wanamuonea...au wanamshobokea...yeye hapendi...lakini sijawahi kumuona hata siku moja akiwakataza...isitoshe matumizi ya neno MIMI MIMI MIMI...NIME...NITA...NIMEKUTEUA...

NA HATA MASIFA MENGINE ANAYOPEWA MBELE YAKE...YEYE ANAONA ANASTAHILI...KIASI KWAMBA...HAWAMTAJI MOLA WAO VILE WANAVYOMTAJA YEYE...

NIKAJUA WAZI KABISA WAZI KUWA HUYU ANAPENDA...
 
Very selfish thinking. Kwa hiyo unadhani wana Simiyu hawadeserve RC makini kama Mtaka bali anawafaa wana Dar es Salaam tuu?

Unforgetable
Sina maana hiyo...mara nyingi huwa mtu anahamishwa kutokana na umuhimu wake na unyeti wa jambo...mfano...Mtaka alivyo bora vile...anaweza akapewa sehemu zenye changamoto pia aende akasettle...
 
Ngoja na mimi nianze kusifia! Nitaweka na namba yangu simu na email yangu mwishoni. Huwezi jua, utashangaa na mimi pia nakumbukwa! 🚶🚶🚶🚶🚶🚶🚶
 
Sina maana hiyo...mara nyingi huwa mtu anahamishwa kutokana na umuhimu wake na unyeti wa jambo...mfano...Mtaka alivyo bora vile...anaweza akapewa sehemu zenye changamoto pia aende akasettle...
du mtaka ana ubora gani mbona ni rais wa riadha alafu kuna madudu matupu kulee
 
Back
Top Bottom