Tusiwalaani wanaoiandama JF, tuwaombee tu

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,097
2,000
Kila kitu na wakati wake. Tulikuwa na zama za ujima, ruksa , uswahili na sasa.........Kawaida ya aina na namna ya utawala huathiri mwenendo wa kila siku wa maisha na aghalabu maono ya kiongozi wa juu huwa ndio mtindo. Tena katika kila eneo iwe mtazamo wa uchumi, elimu, ajira, afya na mengineyo. Kiongozi mkuu atakavyokuwa na kufikiria ndio huwa mwelekeo wetu. Hii ni kwa sababu tumekosa misingi ya kikatiba kuiweka Tanzania tuitakayo kuwa vile inavyotakiwa.


Sioni ajabu haya yanayoiiandama JF, kwani lipi jipya? yalianza na siasa zetu watu wakapiga kelele, wengine walipuuza, yakaja ya bungeni, ya kutumbuana na ikaja zamu ya vyombo vya habari. Tulinyamaza wengine wakisifu.

Kwangu mimi hakuna namna maana anayesimamia haya ana akili timamu na anafahamu kinachoendelea hapa nchini. Kama ni manunguniko anayasikia, kama ni kusifia na kumpongeza anasikia na akikosea pia anapata habari . Lakini kwa nini hakuna mabadiliko? Hulka tu na Tabia ndio tatizo.

Kwa msingi huo hata wasaidizi na waliopewa majukumu wana kazi kubwa. Hawatapona wakienda kinyume na matakwa na ndio nikasema haya yanayoiandama JF si bure . Katika hali hiyo tusiwalaumu waliopewa kazi ya kuiandama JF iwe Polisi au TCRA, hayo ndio majaliwa yao kwa sasa.


Siamini kuwa wadau wa JF wakiwemo viongozi walioko madarakani kwamba wanafurahia haya, lakini wangefanyaje kwa mfano? Waje hadharani wapaze sauti kupinga? Thubutu' Mimi nafikiri tuwaombee tu.

Kishada.
 

Mulhat Mpunga

JF-Expert Member
Oct 28, 2010
27,357
2,000
wanaoiandama jf watakuwa wale mafisadi majangili majizi ya kwenye serikali hii unaweza kukuta jangili limetajwa humu linataka kulipiza kisasi hii nchi ina mambo mengi sana ya ajabu
 

KISHADA

JF-Expert Member
Oct 18, 2012
2,097
2,000
wanaoiandama jf watakuwa wale mafisadi majangili majizi ya kwenye serikali hii unaweza kukuta jangili limetajwa humu linataka kulipiza kisasi hii nchi ina mambo mengi sana ya ajabu
Tuna mwaka tu katika awamu hii. JF iliwahi kusemwa na sasa imeandamwa. Tujiulize hivi watu wote sisi hatuna akili na hatujui umuhimu wa JF ? Nini kinatatiza na kutisha watawala hasa ?
 

Adolph hitler jr

JF-Expert Member
Nov 5, 2016
1,897
2,000
Ukiona hapa dunian huna adui muombe muumba akushushie walau mmoja...maana tunajifunza kutokana na wao...
ONYO : SIYO KWA POMB@ ...maana akili yake anaijua mwenyewe...(akili za maraisi wa Afrika) eti hawajaribiwi (Ant christians)
 

Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom