Tusiwakubali wanaomwaga damu za Watu, tuwafichueni !!!!!!!!!!


mwanawao

mwanawao

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2010
Messages
2,100
Likes
1,987
Points
280
mwanawao

mwanawao

JF-Expert Member
Joined Aug 18, 2010
2,100 1,987 280
Inauma sana. Inasikitisha sana. Jaribu kuchukulia kuwa ni ndugu yako asiye na hatia ameingia kwenye nyumba ya ibada na kuuawa. Au ndugu yako kaenda tu kwenye mkutano wa Siasa iwe ni wa CCM, CHADEMA, CUF, NCCR Mageuzi n.k. ili kutambua tu kuwa ni nani anayeweza kuleta maendeleo kwenye jamii yake anauawa.

Nina imani wapo watu wenye mapenzi mema na nchi yetu bila kujali itikadi zao za kidini, au kisiasa. Kuna watu ambao ni Wakristo hawapendi kumuona Muislamu akionewa kwa sababu tu ya Imani yake, Pia kuna watu ambao ni Waislamu wana mapenzi mema na Wakristo hapendi kuona Mkristo akionewa kwa sababu ya tu ya Imani yake.

Vivyo hivyo kwenye siasa, si watu wote wanapenda kuona mwenzake akionewa kwa sababu tu ya mrengo wa Kisiasa alio nao. Nina imani wapo wana CCM wengi hawapendi kuona wapinzani wakionewa iwe ni CHADEMA, CUF, NCCR-Mageuzi kwa sababu tu amekuwa mpinzani. Pia wapo wapinzani ambao hawapendi kuona mwana CCM akionewa kwa sababu tu ya U-CCM wake.

Rai yangu ni kwamba tuwafichueni watu wote wanaojaribu kutugawa kwa sababu tu ya itikadi zetu. Amani ya nchi yetu ikipotea ni gharama kubwa mno kuitafuta tena na kuipata. Watawala kuweni macho kuwakemea wote walio karibu nanyi pale wanapokuwa wanashindwa kuleta amani katika nchi bila kuwa na upendeleo wa aina yoyote ile, na huu ndio uongozi dhabiti unaotarajiwa na jamii ya Watanzania. Ni vyema kumweka mbali rafiki anayekumalizia ndugu zako mbali nawe kuliko kuendelea kumkumbatia akakufanya baaada ya muda mchache kubakia mpweke bila ndugu.

Tushikamane kufanya maombi kwa bidii, wanao fanya mambo hayo yote ya kuchafua nchi yetu iwe ni katika mrengo wa kidini au kisiasa inawekana wakajificha katika macho ya Nyama lakini hwawezi kujificha mbele za Mungu. Tukishikamana katika maombi Watanzania wote nina Imani Mungu atawafichua tu, atawaweka hadharani kweupee kabisa, maana Mungu wetu hadhihakiwi na tena ni moto ulao, damu zilizomwagwa pasipo hatia zitawarudia juu ya vichwa vyao tu. Tusishangae wakaanza kuokota makopo. Mungu hata cku moja hawezi akaacha kusikiliza Watanzania zaidi ya milioni arobaini walioshikamana kumlilia yeye.

Tuilindeni amani na utulivu kidogo tuliyo nayo katika nchi yetu isipotee. Tuwakatae kabisa wote wenye ushawishi mbovu wa kuliangamiza Taifa letu. Tutee haki zetu kwa njia ya amani. Tuwafichuoni wote walio na malengo ya uovu iwe katika dini ama siasa, iwe ndani ya CCM au Upinzani.

MUNGU ATUSAIDIE!!!

 
mwanawao

mwanawao

JF-Expert Member
Joined
Aug 18, 2010
Messages
2,100
Likes
1,987
Points
280
mwanawao

mwanawao

JF-Expert Member
Joined Aug 18, 2010
2,100 1,987 280
I wish wangepatikana wakawekwa hadharani na kufungiwa jiwe na kutoswa baharini kabisa.
 
M

mmaroroi

JF-Expert Member
Joined
May 8, 2008
Messages
2,534
Likes
31
Points
135
M

mmaroroi

JF-Expert Member
Joined May 8, 2008
2,534 31 135
Subiri watapatikana ila inaweza kuwa kama tukio la kutekwa kwa Ulimboka, kuawa kwa Daudi Mwangosi na kutekwa kwa Kibanda, maana sasa kama wahusika ndio hao wanaotakiwa kukamata na kushitaki inakuwa ngumu.
 

Forum statistics

Threads 1,274,151
Members 490,601
Posts 30,502,798