Tusisherekee Mauwaji ya Arusha | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tusisherekee Mauwaji ya Arusha

Discussion in 'Jukwaa la Siasa' started by BLUE BALAA, Jan 14, 2011.

 1. BLUE BALAA

  BLUE BALAA JF-Expert Member

  #1
  Jan 14, 2011
  Joined: Nov 30, 2010
  Messages: 899
  Likes Received: 6
  Trophy Points: 35
  Arusha si shwari hata kidogo, kumekuwa na series ya events tokea kura za maoni, kampeni, uchaguzi mkuu, matokeo kutangazwa, uchaguzi wa umeya, maandamano na mwisho mauwaji. Tukae tukijua dunia imekuwa ikishuhudia yote haya. Sisi tukikaa hapa tunaongelea mabaya ya Ivory coast, Sudan na sasa Tunisia. Tutambue ya kwamba na sisi sasa tunaongelewa na nchi nyingine na siyo Arusha tu bali Tanzania nzima.

  Nataka kujua je viongozi wetu wa siasa (Chadema na CCM) wanajua cost ya haya mambo yote? Je wamejiandaaje na mavuno ya haya matukio? Kuna analysis yoyote imeshafanyika kujua cost ambayo tayari tume incur? Kuna tetesi kwamba kuna watalii 5000 wamesha cancell kutembelea Tanzania.

  Obervations zangu naona kama vile tunasheherekea mauwaji ya hawa ndugu zetu kwa ajili ya justification fulani bila kujali kwamba kuna watu have been hitted directly na msiba huu.

  Maoni- Tunaomba viongozi wa vyama husika watumie busara kutatua matatizo ya kisiasa ya mjini Arusha na wasipange mikakati ambayo italeta chokochoko na kusababisha madhara makubwa zaidi kwa Taifa letu. Ukizingatia kwamba kukiwa na vurugu walio kwenye risk ya kuzurika ni wananchi masikini na sio nyie viongozi (Fanya tafiti familia ya marehemu Imail na Dennis) Sisi pia tunahitaji kuishi kwa amani kama nyie mnavyoishi na familia zenu.

  Mungu ibariki Tanzania
   
 2. Ms Judith

  Ms Judith JF-Expert Member

  #2
  Jan 14, 2011
  Joined: Dec 24, 2010
  Messages: 2,569
  Likes Received: 20
  Trophy Points: 135
  haki huinua taifa, bali dhambi ni aibu ya watu wo wote (mithali 14:34)
   
 3. Henge

  Henge JF-Expert Member

  #3
  Jan 14, 2011
  Joined: May 14, 2009
  Messages: 6,765
  Likes Received: 78
  Trophy Points: 145
  We hukusikia kamanda wa polisi bwana JOHN alisema cdm wamesababisha yoote haya. na wao wakaona njia nyepesi ni kulenga vifua kupiga lisasi.
  WATATUUUA WOOTE SISI. HII ISUE ICHUKULIWE SILIASI. PLEASE JK JITAHIDI KUFANYA KAZI.
   
 4. Mwanamageuko

  Mwanamageuko JF-Expert Member

  #4
  Jan 14, 2011
  Joined: Oct 31, 2010
  Messages: 3,796
  Likes Received: 1,294
  Trophy Points: 280
  Wakenya wanajenga uwanja mkubwa wa ndege kilomita chache sana toka mlima Kilimanjaro. Hivyo basi vurugu za Arusha na penginepo na Moshi pia zitawasaidia sana wao kuneemeka kiuchumi. Na hizo ndizo mbinu hutumika ili kukudhoofisha, unaposema unaipigania haki basi wapo wengine wanaotaka haki nyingine toka kwako pasi na wewe kujua! Watatumia fursa zinazopatikana hapo ili wao waneemeke. ukitoka usingizini wao wako hatua kumi mbele wewe ndio unaanza. Ni kweli watalii wengi wameahirisha na huenda wengi zaidi wakafanya hivyo. Lakini kwa kawaida kila vita ina gharama zake. Tunapaswa kujulishwa tu tutafunga mikanda kwa muda gani (kwa maana wenye mahoteli hawatakuwa na biashara, wala wauza vinyago na watembeza watalii) Ili watu wajipange kwa kipindi hicho cha mpito.
   
Loading...