Tusipomsifia, tusipomkosoa na kumshauri Rais,tumsifie/tumkosoe/tumshauri nani?

VUTA-NKUVUTE

JF-Expert Member
Nov 25, 2010
6,136
17,871
Rais ni kiongozi wetu wa juu kabisa wa kinchi. Rais ni nembo yetu. Rais ni kioo chetu. Ni kielelezo chetu. Ni dira yetu. Kwa kuwa ni kiongozi wetu mkuu,nembo,kioo na kielelezo cha nchi,Rais lazima asifiwe,akosolewe na kushauriwa.

Anasifiwa anaposema au kutenda mema ya kinchi. Anakosolewa ili aepuke kutenda au kusema yasiyo vutizi hatimaye atende ya kupiga hatua mbele. Anashauriwa katika kuboresha yake na kuyaongeza kunoga.

Kila mtanzania ana haki na wajibu wa kumsifu,kumkosoa na kumshauri Rais. Inaweza kuwa moja kwa moja au kupitia wateule wake. Kwakuwa nembo,dira,kioo na kiongozi mkuu,Rais hapaswi kutosifiwa,kutokosolewa na kutoshauriwa. Rais ni wetu sote!

Mzee Tupatupa wa Lumumba (kwasasa Singida)
 
Anajiona yeye kama Mungu vile hivyo hastahili kukosolewa kwenye lolote lile, ukimkosoa tu basi utambabikiwa kesi na kuitwa mchochezi! Yaani kiongozi anavurunda Wabunge wa upinzani na Watanzania tunaona hivyo kwamba hapa kiongozi kavurunda lakini anataka watu wakae kimya. Tukimkosoa tu kosa tunaitwa wachochezi!!!!
 
Mkuu, wana CCM wenzio wanataka asifiwe tu na kamwe ASIKOSOLEWE. Ukimkosoa tu, Segerea inakuhusu. Ha, ha, ha, dikteta uchwara buana!
 
Mungu yupo na dunia itaamuru,muda mwingine nahisi labda kalaaniwa au nchi hii ina laana,dah!!!!
 
Anataka kupigiwa makofi hata anapokosea hataki kuguswa kabisa kwenye kukoselewa Tundu Lissu aliongea ukweli kabisa
 
Back
Top Bottom