opudojunior
Senior Member
- Mar 8, 2016
- 168
- 102
Mkuu naomba ukafanye utafiti wa uliyoyaandika hapo juu then utapata jibu mwenyewe.Kuna kitu unapaswa ukielewe ambacho ninahisi haukielewi, ni hivi swala zima za overpopulation siyo tu namba ya watu HAPANA, bali ni uwiano wa ukuaji uchumi na ongezeko la watu yaani uchumi wa nchi husika lazima uendane na ongezeko la idadi ya watu kwa mfano angalia nchi zote tajiri Dunia hii popote pale zilipo ziwe Ulaya, Marekani au Asia kuna kitu kimoja utaona zote zinafanana nazo ni kwamba ongezeko la watu halibadiliki sana yaani watu wanaokufa na wanaozaliwa wanalingana au karibia wanalingana hivyo hii inapelekea idadi ya watu kuwa constant au karibia na constant kwa mfano ukiangali labda Ufaransa utakuta ina watu milioni 60 kwa miaka 30 iliyopita au Ujapan ina watu milioni 120 kwa miaka 30 iliyopita vivyo kama kuna kuna ongezeko basi ni la asilimia ndogo sana ambalo linazidiwa na ukuwaji wa Uchumi au hata uchina ina watu 1.3 bilion kwa miaka 40 iliyopita ni constant!
Sasa sisi kwetu ni kinyume chake, ongezeko la watu siyo constant kwa maana wanaozaliwa ni wengi sana klk wanaokufa na hivyo basi ukuwaji wa uchumi wetu hauendani na ongezeko la watu matokeo yake hakuna kazi za kutosha, hakuna huduma za msingi za kutosha hospitali zinazidiwa kama wewe ni mkazi wa Dar utaliona hili wakati mimi nakuwa mambo ya kulala chini Temake Hospitali au M'mala yalikuwa hayapo leo ni kawaida, Shule hazitoshi, Miundo mbinu michache iliyopo inazidiwa kwa maana watu wameongezeka lkn Miundo ni ile ile, Maji ya kunywa hayatoshi kwa maana Bwawa lililojengwa kuhudumia wakazi milioni 1 leo wako milioni 4 lkn Bwawa ni lile lile, Mabomba ya kusafirishia maji ni yale hivyo yanazidiwa!
Sasa tofauti na nchi ulizozitaja hapo juu TanZania miaka 50 iliyopita tulikuwa milioni 18 leo hii milioni 48 hili ni ongezeko kubwa sana lkn kila kitu ni kile kile, kama ni shule zile zile, br. zile zile, mashamba yale yale, uzalishaji wa chakula ni ule ule na hapo ndipo tatizo lilipo sasa, tufanye nini?
Hakuna njia nyingine isipokuwa kufanya population control kwa uzazi wa mpango ili ongezeko letu la watu liendane na uwezo wetu wa kujihudumia!
Nchi zilizoendeleo kama UK, USA na nchi nyingine za Ulaya na Asia zina kawaida ya kuwa na GDP growth rate ndogo kati ya 0.1 na 4 lakini population growth rate huwa juu ya hapo na sio sawa kama unavyodai wewe. Mfano population growth rate ya UK ni 5.4, Ufaransa ni 4.5 na Ujerumani ni 5 tukija upande wa GDP growth rate ya UK ni1.8 na Ufaransa ni 2. Sasa hapa ukiangalia bado population growth ni kubwa kuliko GDP growth rate na haiwezekani idadi ya watu wanaozaliwa na wanaokufa kuwa sawa. Nchi zote population inaongezeka na uchumi pia unakua
Kuhusu kuongezeka kwa miundombinu ni swala serikali kuangalia hilo barabara hazijengwi na watu binafsi hiyo ni kazi ya serikali na miundombinu ya afya kama hospitali ni uwekezaji wa serikali na secta binafsi sasa kama hatuwekezi ndio tusizae?
Hivi ni kweli kuwa miundombinu iliyoko sasa ndio hiyo hiyo iliyokua miaka ya 90?
Tuwe wawazi tu kuwa serikali zetu zilizopita hazikua makini katika kupanga na kutekeleza mipango wanayopanga, idadi ya watanzania iliyopo sasa sio bahati mbaya serikali ilishajua kwa kufanya projection hivyo ilikua ni swala la kuandaa miundombinu mapema.