Tusimlaumu Rais Magufuli Kwa Kila Kosa, Rais Yeye Hana Kosa Bali Anashauriwa Vibaya!.

Pascal Mayalla

Platinum Member
Sep 22, 2008
52,668
119,281
Wanabodi,

Kumekuwepo malalamiko mengi huku kwenye mitandao ya kijamii kuhusu utendaji wa rais wetu na baadhi ya maamuzi yake yanahojiwa sana huku kwenye mitandao ya kijamii kuwa kuna baadhi ya mambo rais wetu hajafanya the right thing at the right time and hasn't done them right.

Nyingi ya hizi lawama zinaelekezwa direct Kwa rais Magufuli Kwa sababu yeye ndie Mkuu wa nchi. Nchi inatawaliwa kwa mujibu wa Katiba ya Nchi na sio kwa mujibu wa matakwa ya rais ikimaanisha hata rais yuko chini ya Katiba, sasa inapotokea rais akawa juu ya Katiba, sio kosa lake, kwa sababu kila rais anachokifanya anakifanya kwa kupokea ushauri au kabla au ashauriwe baada. Rais akifanya kitu un appropriate na kikaachwa tuu, hili linakuwa sio kosa lake bali kosa la washauri wake kuwa rais wetu ameshauriwa vibaya, hivyo yeye hana makosa, hatuwezi kumlaumu rais Magufuli kwa kila kitu ambacho hakiendi sawa kwa mujibu wa jicho mitandao ya kijamii.

Katiba.q
Kwa mujibu wa katiba yetu kuna vitu imempa mamlaka ya kuvifanya kwa maamuzi yake mwenyewe tuu, yaani at his discretion au at his pleasures bila kupokea ushauri wa mtu yoyote, mfano kwenye baadhi ya teuzi wakiwemo baadhi ya wasaidizi wake.

Kuna teuzi Katiba inaelekeza rais atashauriana na watu fulani, na kuna teuzi ambazo rais atazifanya not at his pleasures bali kwa kufuata maelekezo fulani. Miongoni mwa teuzi hizi ni uteuzi wa Jaji Mkuu, rais hateui tuu for his pleasures bali huteua kwa mujibu wa Katiba ilivyoelekeza.

Huu uteuzi wa Kaimu Jaji Mkuu umezua mjadala hadi rais kulaumiwa huku wengine wakimtetea, hoja yangu katika mada hii sio kila kitu kumlaumu tuu rais, rais anawasaidizi na anawashauri, hivyo kuna baadhi ya mambo akiyafanya no matter how wrong they might seem to be, the president is always right kwa sababu ameshauriwa.

Naomba kukiri nimekuwa inspired kupandisha hoja hii kufuatia majibu ya mwana jf huyu kwenye hoja zangu kwenye mjadala mwingine.

Naomba izingatiwe kuwa msisitizo mweusi na wa italiki ni wa kwangu kwa ajili ya kuweka msisitizo.

Kwanza kabisa, siyo kweli - kama mtu akisoma Katiba - kwamba lengo la kifungu cha kumpa Rais kuteua Kaimu Jaji "kilidhamiria" kuwa atateuliwa pale tu "jaji mkuu yupo" lakini kwa namna fulani anashindwa kutekeleza majukumu yake. Huku ni kudhania (assumption) ambayo haina msingi.

Katiba imesema kuwa endapo mambo matatu yakitokea basi Rais anaweza kuteua Kaimu Jaji Mkuu. Mambo hayo kwa mujibu wa Ibara ya 118:4 ni kuwa Rais anaweza kuteua Kaimu Jaji Mkuu endapo mambo yafuatayo yatatokea: a. Kiti kitakuwa wazi (na hapa ina kuwa implied kwa sababu mbalimbali ikiwemo, kifo, kujiuzulu, kustaafu n.k), b. Jaji Mkuu hayupo Tanzania (sehemu ya hoja yako) na tatu Jaji mkuu atashindwa kutekeleza majukumu yakekwa sababu yeyote ile (na implication hapa ni vitu kama ugonjwa, katekwa n.k) basi Katiba inasema " Rais ataona kuwa kwa muda wa
tukio lolote kati ya hayo matatu inafaa kumteua Kaimu Jaji Mkuu, basi Rais anaweza kumteua Kaimu Jaji Mkuu kutoka miongoni mwa Majaji wa Rufani."


Hivyo, SI KWELI na haina msingi wowote katika Katiba kuwa lengo la Ibara ya 118:4 lilikuwa ni pale tu Jaji anapokuwa yupo lakini hawezi kufanya kazi yake. Hili ni la kujitungia tu halina msingi katika Katiba na ukilifikiria halina mantiki ya kiutendaji. Hivyo, linaanguka lenyewe.
Mkuu Mzee Mwqnakijiji, with due respect tangu mwanzo nilikuambia you've missed the point, na hapa sasa bado you've missed the point again and you will miss it again and again kwa sababu ameisha amini hicho unachojua ndicho kumbe sicho!.

Hizo scenarios zote tatu za kutokuwepo kwa jaji mkuu ni sawa kama ulivyoeleza ila usichojua wewe na sio hujui bali hutaki kujua kuwa uteuzi wa kaimu jaji mkuu hufanyika nafasi hiyo ikiwa wazi kwa sababu nyingine zozote na sio wakati jaji mkuu amemaliza muda wake!.

Kuna sheria kibao zimewekwa kwa nia njema lakini zinakuwa applied wrongly na wakuu wa serikali yetu.

Mfano kwenye uteuzi wa mawaziri katiba inasema mtu kuteuliwa waziri lazima awe mbunge, tumeshuhudia mtu atateuliwa ubunge na kuwa mbunge mteule kisha anateuliwa waziri na kuingia ofisini kabla hajaapishwa kuwa mbunge kamili.
Kuwa waziri kabla ya kuapishwa kuwa mbunge

Hivyo matumizi ya kukaimu kwenye issue ya Jaji Mkuu ni makosa kwa sababu Tume ya Majaji ilikwisha peleka majina matatu, miongoni mwa majina hayo, mmoja wao ateuliwe kuwa Jaji Mkuu. Kitendo cha rais Magufuli kuteua Kaimu Jaji Mkuu ni dharau kubwa kwa Tume ya Majaji.

Kama jina la Prof. Ibrahim Juma lipo miongoni mwa majina matatu hayo, then anachofanya rais Magufuli ni dharau kubwa kwa mhimili wa mahakama. Mahakama ni mhimili wa dola, mhimili ni egemeo, kama yalivyo mafiga matatu yote yanatakiwa kuwa sawa ili chungu kisimame, figa moja likiwa tenge chungu kitakuwa tenge. Kwa nini mhimili huu ukaimiwe? .

Unless kupitia vetting, majina yote matatu yaliyopendekezwa na tume ya majaji yalikataliwa, hivyo rais Magufuli akamteua Kaimu ili kushikilia kwa muda wakati Tume ikitafuta majina mengine!.

Hili pia ndugu yangu Nguruvi kalisema hapo juu; lakini wewe na yeye wote hamsemi je sheria au utaratibu huo unamtaka Rais ateue mtu muda gani tangu apewe majina hayo matatu? Kama kuna mtu anaamini RAis amechelewa kinyume cha sheria tangu apate majina hayo matatu wapo wanasheria makini tu wafungue kesi mahakamani iamuliwe! Lakini sijaona hata mmoja anayedai

Ni kweli sheria haikuweka muda, sio kila kitu sheria imeweka muda, vitu vingine ni application tuu ya logic na common sense ambavyo very unfortunately havipo. Jaji Mkuu amestaafu, amestaafu ghafla kabla ya muda wake, then ingekuwa right kuteua Kaimu wakati tunatafuta Jaji Mkuu, this was not the case!. Do we need kuweka time frame?!

This is very absurd; Inawezekana vipi kiti cha Jaji Mkuu kiwe wazi permanently halafu unataka kijazwe. Au neno "permanently" halina maana tena? Kama kitajazwa hakiko permanently vacant! It is only because it is temporarly vacant ndio maana watu wanataka kijazwe. I don't like self contradictions.
Sometimes tumia context ya nilichomaanisha na sio kutumia syntax ya neno permanently!. Nimekueleza Kaimu Jaji Mkuu anapaswa kuteuliwa wakati nafasi ya Jaji Mkuu inapokuwa wazi temporarily safari au ugonjwa na akirudi au akipona anaendelea. Au Kaimu Jaji Mkuu atateuliwa kikitokea kifo, hili ni tukio la ghafla hivyo hakuna maandalizi yoyote ya kumpata Jaji Mkuu ndipo mtu anateuliwa kukaimu kutoa muda wa kumtafuta Jaji Mkuu. Hivyo hapa Kaimu ni kama kiraka tuu.

Situation iliyopo ya Jaji Mkuu kustaafu kwa umri hivyo maandalizi yote yamekamilika ya replacement. Kustaafu kwa umri ni permanent na sio temporary hadi ku warrant Kaimu!. Hapa Jaji Mkuu has left the office permanently, angekuwa amesafiri then ingekuwa temporarily!. Why uweke Kaimu kwa nafasi wazi ya Mkuu wa chombo cha dola?.
Then, watu wanaoona hivyo wanatakiwa wamtake yeye ajiuzulu siyo wamlazimishe Rais ajaze nafasi. Rais halazimishwi kupokea ushauri wa yeyote kwa mujibu wa Katiba kama sivyo itakuwa ni chaos na hatokuwa huru kivile. Rais akimteua mtu mwingine kesho au akimthibitisha si watu wengine wanaweza kulalamika kuwa Rais kashinikizwa au kalazimika na hivyo itatolewa hoja nyingine kabisa.

Mbona hii si nafasi ya kwanza ambayo inakaimiwa wakati mtu anasubiriwa kuteuliwa.
Yote usemayo kuhusu rais ni kweli, kitendo tuu cha kuteuliwa kuwa Kaimu ni Heshima tosha, hakuna anayemlazimisha rais kutimiza wajibu wake lakini hakijawahi kutokea katika historia ya nchi yetu nafasi ya mhimili mmoja wa dola kukaimiwa kwa kipindi kirefu hivi huku nafasi ikiwa wazi permanently!.

Kitendo cha kumkaimisha Prof. Juma ni kama kutuambia kuwa hatoshi ndio maana yuko under probation!. Tunamlazimisha rais Magufuli amthibitishe na ikitokea akamteua mtu mwingine (probably kwa kumtafuta Msukuma popote), then Dr.Juma aage tuu na kujipumzikia kwa amani.

Una assume mambo mengi sana. Kwanini unafikiria sijui tofauti ya kukaimu mbalimbali; si ndio maana ya swali langu hapa? Suala la nafasi ya jaji hakuna mtu anayesema Rais amevunja Katiba; na kama hajavunja sasa shida iko wapi? Ni kweli kawaida au taratibu ni kama sheria lakini neno "kama" ina nguvu yake; kawaida si sheria! Ukitaka iwe sheria ifanye sheria.

Mfano Bunge likitaka kufanya impeachment process Kaimu Jaji Mkuu hawezi kwa sababu aliielezwa kwenye sheria ni Jaji Mkuu.

Sio naasume, bali huu ndio ukweli wenyewe ndio maana kwako kukaimu ni kukaimu tuu, hujui tofauti ya nafasi wazi temporarily kunakohitaji Kaimu na nafasi wazi permeability kunako hitaji replacement!.

Kwa kumalizia Magufuli ni rais wetu ila vingi anafanya ndivyo sivyo, wahusika wa kumshauri kwa karibu ndio hawa wanamuogopa. Huku kwenye social media kwa kwa manguli critical kama Mzee Mwanakijiji ndio hawa sasa wanamuabudia hadi kumuita ni Alfa na Omega, unategemea nini?.

Siku ile ulipomuita Magufuli alfa na omega nilikubishia nikakueleza Magufuli is only a human being kama mimi na wewe ila ni rais wetu

Mkuu Mzee Mwanakijiji, Rais Magufuli Sio Alfa na Omega. Rais Sio Mungu! Na Kwenye Utawala ni Katiba!

Nikasema anaweza kuwa anafanya makosa ila sio makosa yake, kwa sababu ana washauri, anaweza kuwa anashauriwa vibaya, hivyo kila analotenda ndivyo sivyo, wa kulaumiwa sio yeye bali ni waliomshauri, au wasaidizi wake wanaoona ndivyo sivyo na wananyamaza badala ya kumshauri kufanya ndivyo.

Wasaidizi wa Rais, Please Msaidieni Rais Wetu Kwenye Public . Msimuachie Kila Kitu Peke Yake! .

Je, wajua amri za Rais sio final and conclusive?. Zinaweza kupigwa chini na mchanga kusafirishwa?

AG, Mshauri Mh.Rais Atoe Maagizo kwa Presidential Decrees Kuyapa Nguvu ya Kisheria

Paskali
 
Huyu huyu aliyesema hasikilizi watu ila anajua mwenyewe?! Huyu huyu dereva wa lori aliyesema hataki kelele za abiria,japo hajui kuwa wanampigia kelele kuwa tairi limechomoka?!

Mimi nataka kusikia tu pale UDOM aliposema kumejaa vilaza,leo atasemaje!!
 
kama anashauriwa ujinga anakubali basi hakuna haja ya kuwa na rais mwenye vigezo,tuweke hata jiwe au mtoto tumshauri,siku akiambiwa na washauri atembee uchi atakubali bila shaka,kma usemacho ni kweli ....naogopa kutekwa
 
Huu ndio ukabila wenyewe huu.Unapakapaka rangi ili iweje
Kama anashauriwa vibaya ubabe,ukali,ushamba na ujuaji vinatoka wapi.Anashauriwa kulinda cheti cha Bashite?Anashauriwa vibaya kutukana na kukejeli wana Bukoba,Anashauriwa vibaya kukandamiza Uhuru wa kujieleza. Kumlinda Lipumba na kuyokemea watekaji.Kukubali ushauri wa hovyo inadhibitisha kuwa hana anachokijua

Sio wewe tu hata huku wasukuma wanapakapaka rangi ili moyoni wabakubali
 
Wanabodi,

Kumekuwepo malalamiko mengi huku kwenye mitandao ya kijamii kuhusu utendaji wa rais wetu na baadhi ya maamuzi yake yanahojiwa sana huku kwenye mitandao ya kijamii kuwa kuna baadhi ya mambo rais wetu hajafanya the right thing at the right time and hasn't done them right.

Nyingi ya hizi lawama zinaelekezwa direct Kwa rais Magufuli Kwa sababu yeye ndie Mkuu wa nchi.

Katiba.q
Kwa mujibu wa ka
my brother, what hasnt done right?
 
Wanabodi,

Kumekuwepo malalamiko mengi huku kwenye mitandao ya kijamii kuhusu utendaji wa rais wetu na baadhi ya maamuzi yake yanahojiwa sana huku kwenye mitandao ya kijamii kuwa kuna baadhi ya mambo rais wetu hajafanya the right thing at the right time and hasn't done them right.

Nyingi ya hizi lawama zinaelekezwa direct Kwa rais Magufuli Kwa sababu yeye ndie Mkuu wa nchi.

Katiba.q
Kwa mujibu wa ka
Ulishawahi ona wapi mume akamlaumu house girl kwa kupika chakula kibichi ili hali mama mwenye nyumba yupo?
 
Hapangiwi cha kufanya huo ushauri mbaya nani anathubutu kumpa?
 
Wanabodi,

Kumekuwepo malalamiko mengi huku kwenye mitandao ya kijamii kuhusu utendaji wa rais wetu na baadhi ya maamuzi yake yanahojiwa sana huku kwenye mitandao ya kijamii kuwa kuna baadhi ya mambo rais wetu hajafanya the right thing at the right time and hasn't done them right.

Nyingi ya hizi lawama zinaelekezwa direct Kwa rais Magufuli Kwa sababu yeye ndie Mkuu wa nchi.

Katiba.q
Kwa mujibu wa ka

Mshauri amuondoe yule anayeitwa Bashite halafu aone tutakavyompongeza
 
Anashauriwa na ziro fa fa bashite unadhani kutakuwa na maendeleo


Swissme
 
Wanabodi,

Kumekuwepo malalamiko mengi huku kwenye mitandao ya kijamii kuhusu utendaji wa rais wetu na baadhi ya maamuzi yake yanahojiwa sana huku kwenye mitandao ya kijamii kuwa kuna baadhi ya mambo rais wetu hajafanya the right thing at the right time and hasn't done them right.

Nyingi ya hizi lawama zinaelekezwa direct Kwa rais Magufuli Kwa sababu yeye ndie Mkuu wa nchi.

Katiba.q
Kwa mujibu wa ka
hivi wewe si ndio siku ile ulikuwa unamtetea muhuni mwenzio nyalandu wakati anasigina haki ya wananchi wa Ilongero kuhusu makao makuu?? hebu ficha aibu yako huko
 
Usiwasingizie washauri..yeye hawasikilizi so kila kinachoharibika ni juu yake...
 
Wanabodi,

Kumekuwepo malalamiko mengi huku kwenye mitandao ya kijamii kuhusu utendaji wa rais wetu na baadhi ya maamuzi yake yanahojiwa sana huku kwenye mitandao ya kijamii kuwa kuna baadhi ya mambo rais wetu hajafanya the right thing at the right time and hasn't done them right.

Nyingi ya hizi lawama zinaelekezwa direct Kwa rais Magufuli Kwa sababu yeye ndie Mkuu wa nchi.

Katiba.q
Kwa mujibu wa ka
Acha dharau!!!
Anashauriwa vibaya na nani? Kama anashauriwa vibaya basi atuonyeshe kuwa anaweza kujishauri vizuri.
Pascal Mayalla ujue tunakuheshimu kiasi!!!
Angalia tusije tukakudharau.

Mkuu wa nchi hajachangia ukuu wa nchi na mtu yoyote FULL STOP
 
Mtu akikuonyesha kipande cha chupa, akasema hii ni almasi, nawe ukakubali, basi utakuwa zuzu - Mwl Nyerere
 
Wanabodi,

Kumekuwepo malalamiko mengi huku kwenye mitandao ya kijamii kuhusu utendaji wa rais wetu na baadhi ya maamuzi yake yanahojiwa sana huku kwenye mitandao ya kijamii kuwa kuna baadhi ya mambo rais wetu hajafanya the right thing at the right time and hasn't done them right.

Nyingi ya hizi lawama zinaelekezwa direct Kwa rais Magufuli Kwa sababu yeye ndie Mkuu wa nchi.

Katiba.q
Kwa mujibu wa ka

Kwa mara ya Kwanza tokea nikufahamu leo ndiyo naona moja ya thread yako iliyokosa nyama za kutosha zitakazoweza kuifanya iwe logical. Kwa kifupi tu Kamarada thread yako kuna baadhi ya nyama fulani fulani muhimu hujaziweka ama kwa kusahau pengine kwa kuwa na haraka au siku hizi na Wewe labda umeanza Kukengeuka Kitaaluma na Kiueledi.
 
Hakusema hashauriwi bali "hapangiwi".... Anashindwa kuelewa kitu kidogo tu, ukiwa kiongozi unapangiwa ila uchaguzi ni wako.

Wasaidizi wa raisi hupeleka taarifa pamoja na recommendations. Sasa mkuu anaona recommendations kama vile anapangiwa fulani hivi. Anakosa mwanya wa kupanga yeye katika mtizamo wake maana wataalamu wamempa limited options za kuchagua.

Mkuu anachotakiwa kufanya ni KUCHAGUA SIO KUPANGA MIPANGO MWENYEWE. Naamini timu inawezakuwa na mipango mizuri kuliko raisi anavyodhania.

Tuombe Mungu siku ifike atambue kuwa yeye kazi ya ofisi yake si kupanga bali kufanya maamuzi ya mwisho kati ya "recommendation options"
 
Back
Top Bottom