‪Tusikubali udhalilishaji wa Jarida la The Economist, lamwita Rais wetu "Dinasauria wa Dodoma” na "bullheaded socialist"

Wanabodi,

Uongo ukisemwa sana na kuachwa kurudiwa rudiwa bila kukanushwa, mwisho wake hugeuka ukweli, baada ya kutokukemea magazeti ya nje kuandika uongo kumhusu rais wetu na kumuita majina ya ajabu ajabu, huku sisi na serikali yetu tumenyamaza , sasa ni zamu ya jarida la The Economist, limemtukana rais wetu "dinasauria wa Dodoma" kisha wakamuita a bad president na hadi kumtukana Baba wa Taifa, "a bullheaded socialist!". Pia kumsingizia mambo mengi ya uongo katika toleo lake la hivi karibuni kama nilivyonukuu hapa.

Wakuu Mwanakwetu na Kibanga, kwanza asanteni kwa bandiko hili, pili
tusikubali uwongo huu wa gazeti la The Economist

Uongo Mbalimbali ambazo Hazijakanushwa.
Hi ni baadhi ya uongo mbalimbali ambazo hazijakanushwa hadi leo ambazo mimi kama Mtanzania Mzalendo, kazi yangu ni kushauri tuu.
  1. Rais wetu alipotuhumiwa kuhongwa suti nilipinga na kushauri.Tuhuma za Rais wetu kuhongwa suti: Marekani ituombe radhi ...
  2. Hata kelele kuhusu udikikiteta wa Magufuli ziliposhika kasi nilishauriUdikiteta: Uongo Ukisemwa Sana na Kuachwa Bila Kukanushwa Hugeuka ...
  3. Magufuli aliposemwa vibaya na SABC, nilishauriSerikali ikanushe uongo huu wa SABC kumsema vibaya Rais wetu ...
  4. Rais Magufuli aliposemwa vibaya kuhusu Mimba za utotoni, pia nilishauriJe, Huku Sio Kudhalilishwa Kwa Rais Wetu na Media za Nje?. Jee ...
  5. Juzi kati hapa serikali yetu ilipoitwa Sinister na Authoritarian, pia nilishauri
    Serikali yetu Kuitwa "Sinister" na "Authoritarian": Je, ni kweli ...
Hitimisho.
Uongo ukisemwa sana sana na kuachwa bila kukanushwa, mwisho wake, sio tuu utaonekana kama ni ukweli, bali una hatari ya kugeuka kuwa ukweli kwa sababu kauli huumba!.
Natoa wito kwa Watanzania wote wazalendo wa kweli wa nchi hii, tusikubali rais wetu kutukanwa. kudhalilishwa na kusingiziwa uongo huku sisi wazalendo tupo na tumenyamaza tuu kimya, bila kufanya lolote. Tusikubali.

Paskali
Kwahiyo umasikini ni uzalendo?? Wewe paskali unafiki unakuweka majaribuni.
 
Uzalendo haulazimishwi, how come mtu anabomelewa nyumba yake then umwambie awe mzalendo, au Mtu ni mfanya biashara ana bambikiziwa kodi na TRA then huyo mtu umwambie asomame aitetee Serikali.

Wale wanao pata keki na waendelee kuitetea
Raisi aliwaomba viongozi wa Mwanza wasiwabomolee nyumba wananchi maana ndio waliompa kura.Mbona Kimara Mbezi wamebomolewa bila fidia tena wengi walikuwa na title deed.Hivi huyu Raisi ni wa wanyonge.Kura za Kimara Ccm waliiba.Hivi unaweza kumweleza mtu huyu uzalendo ?
 
Ndg P
Kwa nini unapoeleza mambo ya uongo unachanganya kiswahili na kiingereza ? Na hii ni kasumba ya waandishi waojificha chini ya jambo Fulani !

Ukifikia kipengele ambacho unajua wengi wataelewa unachowadanganya unatumia kiingereza.!Mbona hayo maneno yana kiswahili chake ? .
Jitahidi Maneno ya Kingereza yatumike pale tu yanapohitaji kwa maana inaondoa maana yote
Ndugu Paschal unajua ni kawaida yetu sisi waafrika kwa ujumla huwa hatupendi kuambiwa ukweli, na ndio maana tukiambiwa ukweli siku zote tunakua wakali. Nampenda mwalimu alituasa kua kufanya kosa sio kosa ila kurudia kosa ni kosa kubwa. Baba akihakikisha watoto wake wanakula na analipa ada ya shule watoto hawana sababu ya kumsifia kwani ni wajibu wake, siku wakilala njaa wanahaki ya kumlaumu kwasababu hajatimiza wajibu. Serikali kufanya yale yaliyo kwenye wajibu wake haistahili sifa na wala haiwezi kudai sifa au kusifiwa maana inatimiza wajibu wake wa kikatiba. Ila the same government ikikosewa lazima ilaumiwe kwasababu inaenda kijnyume na matakwa au wajibu wake. Sasa kama tukiambiwa ukweli tunaona tunaonewa au gazeti liko biased kwasababu halitusifii tunapofanya vizuri then we are dead wrong kwasababu hatutakiwi kudai sifa tunapitimiza wajibu wetu kikatiba na kisheria, ila tukipotoka ni lazima tulaumiwe na ni wajibu wetu kujitazama tunakosea wapi.
 
Dinasauria ndio nini Pascal Mayalla
Paskali amejipa kazi ya kusambaza matusi dhidi ya Rais John Pombe Joseph Magufuli.
Paskali kama Mwanasheria na Mwandishi wa habari anajua fika kuwa kutafasiri maandiko HASI PEKEE ya magazeti ya nje, hususan gazeti la 'The Economist' na kuyabandika JF, lengo lake ni kumtukana na kumdhalilisha JPM kwa jamii ya Watanzania, tena kwa makusudi.
Hii ni kwa sababu Paskali anajua kuwa hakuna Watanzania wanaosoma hayo magazeti isipokuwa yeye na wengine wachache sana.
Kubandika maandiko hayo JF lengo ni moja tu! Kuwashirikisha Watanzania katika kumtusi JPM.
Haiyumkiniki Paskali anatumiwa na mabeberu kuihujumu nchi yetu!
Matusi dhidi ya Rais wetu yana lengo moja tu: Kututoa kwenye mstari Wa maendeleo makubwa tunayopiga kama Taifa chini ya Jemedari JPM.
Naamini Paskali hajakamatwa kwa kuwa ni 'Kabila yetu'
 
Wanabodi,

Uongo ukisemwa sana na kuachwa kurudiwa rudiwa bila kukanushwa, mwisho wake hugeuka ukweli, baada ya kutokukemea magazeti ya nje kuandika uongo kumhusu rais wetu na kumuita majina ya ajabu ajabu, huku sisi na serikali yetu tumenyamaza , sasa ni zamu ya jarida la The Economist, limemtukana rais wetu "dinasauria wa Dodoma" kisha wakamuita a bad president na hadi kumtukana Baba wa Taifa, "a bullheaded socialist!". Pia kumsingizia mambo mengi ya uongo katika toleo lake la hivi karibuni kama nilivyonukuu hapa.
Uongo ukisemwa sana sana na kuachwa bila kukanushwa, mwisho wake, sio tuu utaonekana kama ni ukweli, bali una hatari ya kugeuka kuwa ukweli kwa sababu kauli huumba!.
Natoa wito kwa Watanzania wote wazalendo wa kweli wa nchi hii, tusikubali rais wetu kutukanwa. kudhalilishwa na kusingiziwa uongo huku sisi wazalendo tupo na tumenyamaza tuu kimya, bila kufanya lolote. Tusikubali.

Paskali
Wanabodi, ni katika kukumbushana tuu, kuwa uongo ukisemwa sana na kuachwa kurudiwa rudiwa bila kukanushwa, hugeuka kuwa ukweli!.
Huu ulikuwa ni uongo wa jarida The Economist, haukukanushwa, sasa umetokea kweli!. Dunia sasa itazidi kuliamini jarida la The Economist kuwa lilisema kweli kuhusu Tanzania!.

Funzo kwa serikali yetu, kauli huumba!, kunapotolewa kauli yoyote ya uongo mkubwa kama huu kuihusu nchi yetu, inapotolewa na vyombo vikubwa vya habari vya mabeberu wa kimataifa, tuzikanushe!. Kwa kuto zikanusha, kauli hizi zimeumba. Sasa kwa huku bara, upinzani ni umekufa, unasubiri mazishi tuu, unless rais Magufuli aingie huruma awateua wapinzani wawili watu kuwa wabunge wa kuteuliwa ili angalau kulichangamsha Bunge!.
Paskali
 
Wanabodi,

Uongo ukisemwa sana na kuachwa kurudiwa rudiwa bila kukanushwa, mwisho wake hugeuka ukweli, baada ya kutokukemea magazeti ya nje kuandika uongo kumhusu rais wetu na kumuita majina ya ajabu ajabu, huku sisi na serikali yetu tumenyamaza , sasa ni zamu ya jarida la The Economist, limemtukana rais wetu "dinasauria wa Dodoma" kisha wakamuita a bad president na hadi kumtukana Baba wa Taifa, "a bullheaded socialist!". Pia kumsingizia mambo mengi ya uongo katika toleo lake la hivi karibuni kama nilivyonukuu hapa.

Wakuu Mwanakwetu na Kibanga, kwanza asanteni kwa bandiko hili, pili
tusikubali uwongo huu wa gazeti la The Economist

Uongo Mbalimbali ambazo Hazijakanushwa.
Hi ni baadhi ya uongo mbalimbali ambazo hazijakanushwa hadi leo ambazo mimi kama Mtanzania Mzalendo, kazi yangu ni kushauri tuu.
  1. Rais wetu alipotuhumiwa kuhongwa suti nilipinga na kushauri.Tuhuma za Rais wetu kuhongwa suti: Marekani ituombe radhi ...
  2. Hata kelele kuhusu udikikiteta wa Magufuli ziliposhika kasi nilishauriUdikiteta: Uongo Ukisemwa Sana na Kuachwa Bila Kukanushwa Hugeuka ...
  3. Magufuli aliposemwa vibaya na SABC, nilishauriSerikali ikanushe uongo huu wa SABC kumsema vibaya Rais wetu ...
  4. Rais Magufuli aliposemwa vibaya kuhusu Mimba za utotoni, pia nilishauriJe, Huku Sio Kudhalilishwa Kwa Rais Wetu na Media za Nje?. Jee ...
  5. Juzi kati hapa serikali yetu ilipoitwa Sinister na Authoritarian, pia nilishauri
    Serikali yetu Kuitwa "Sinister" na "Authoritarian": Je, ni kweli ...
Hitimisho.
Uongo ukisemwa sana sana na kuachwa bila kukanushwa, mwisho wake, sio tuu utaonekana kama ni ukweli, bali una hatari ya kugeuka kuwa ukweli kwa sababu kauli huumba!.
Natoa wito kwa Watanzania wote wazalendo wa kweli wa nchi hii, tusikubali rais wetu kutukanwa. kudhalilishwa na kusingiziwa uongo huku sisi wazalendo tupo na tumenyamaza tuu kimya, bila kufanya lolote. Tusikubali.

Paskali
Kuitwa " DINASAURIA WA DODOMA AU BULLHEAD SOCIALIST" Kwangu naona wamemsifia. Huyu ni shetani, muuaji, Primitive minded.
 
Back
Top Bottom