mchajikobe
JF-Expert Member
- Aug 14, 2009
- 2,652
- 1,238
Mbona Okwi umesahau kumtaja haa haaWanabodi,
Uongo ukisemwa sana na kuachwa kurudiwa rudiwa bila kukanushwa, mwisho wake hugeuka ukweli, baada ya kutokukemea magazeti ya nje kuandika uongo kumhusu rais wetu na kumuita majina ya ajabu ajabu, huku sisi na serikali yetu tumenyamaza , sasa ni zamu ya jarida la The Economist, limemtukana rais wetu "dinasauria wa Dodoma" kisha wakamuita a bad president na hadi kumtukana Baba wa Taifa, "a bullheaded socialist!". Pia kumsingizia mambo mengi ya uongo katika toleo lake la hivi karibuni kama nilivyonukuu hapa.
Wakuu Mwanakwetu na Kibanga, kwanza asanteni kwa bandiko hili, pili
tusikubali uwongo huu wa gazeti la The Economist
Uongo Mbalimbali ambazo Hazijakanushwa.
Hi ni baadhi ya uongo mbalimbali ambazo hazijakanushwa hadi leo ambazo mimi kama Mtanzania Mzalendo, kazi yangu ni kushauri tuu.
Hitimisho.
- Rais wetu alipotuhumiwa kuhongwa suti nilipinga na kushauri.Tuhuma za Rais wetu kuhongwa suti: Marekani ituombe radhi ...
- Hata kelele kuhusu udikikiteta wa Magufuli ziliposhika kasi nilishauriUdikiteta: Uongo Ukisemwa Sana na Kuachwa Bila Kukanushwa Hugeuka ...
- Magufuli aliposemwa vibaya na SABC, nilishauriSerikali ikanushe uongo huu wa SABC kumsema vibaya Rais wetu ...
- Rais Magufuli aliposemwa vibaya kuhusu Mimba za utotoni, pia nilishauriJe, Huku Sio Kudhalilishwa Kwa Rais Wetu na Media za Nje?. Jee ...
- Juzi kati hapa serikali yetu ilipoitwa Sinister na Authoritarian, pia nilishauri
Serikali yetu Kuitwa "Sinister" na "Authoritarian": Je, ni kweli ...
Uongo ukisemwa sana sana na kuachwa bila kukanushwa, mwisho wake, sio tuu utaonekana kama ni ukweli, bali una hatari ya kugeuka kuwa ukweli kwa sababu kauli huumba!.
Natoa wito kwa Watanzania wote wazalendo wa kweli wa nchi hii, tusikubali rais wetu kutukanwa. kudhalilishwa na kusingiziwa uongo huku sisi wazalendo tupo na tumenyamaza tuu kimya, bila kufanya lolote. Tusikubali.
Paskali