‪Tusikubali udhalilishaji wa Jarida la The Economist, lamwita Rais wetu "Dinasauria wa Dodoma” na "bullheaded socialist"

HAO ECONOMIST WAKO POA SANA, JE KUUNDA SHERIA NA KUHUKUMU WASIO ANZA NAYO SI UDINOSARIA HUO?*(MALIPO MIKOPO VYUO VIKUU), JE UKIICHALENGE SERIKALI HAWAKUBULLDOZZ ????TUACHE UNAFIKI UZALENDO HAUJENGWI KWA KUMINYA HAKI ZA WACHACHE. WAKALIFUNGIE NA ILO.
 
Amtume waziri alifungie miaka 3 au apambane mwenyewe kurudisha hadhi yake.
Kama watanzania walioko nje anasema "wanyongwe"tu,ya kwake ndo yatunyime usingizi???
 
Uzalendo haulazimishwi, how come mtu anabomelewa nyumba yake then umwambie awe mzalendo, au Mtu ni mfanya biashara ana bambikiziwa kodi na TRA then huyo mtu umwambie asomame aitetee Serikali.

Wale wanao pata keki na waendelee kuitetea


Haya uyasemayo ni maneno ya mtu asiye na akili timamu. Serikali si adui wa nchi, wale waliobomolewa nyumba zao walikuwa walijenga kiholela yaani hawakuwa na vibali kujenga. Waliobambikiwa kodi na TRA ilikuwa si serikali waliofanya vile bali watumishi wa serikali ndiyo walifanya vile na kusingizia wanafanya kwa niaba ya serikali kumbe walikuwa wanawaibia raia wema. Tumshukuru rais wetu Magufuli, ni sawa kabisa asemavyo Pascal Mayalla kuwa tusikubali haya matusi anayotukanwa rais wetu kwani mabepari wa nje hawapendi hata siku moja kuona nchi ya kiafrika ina msimamo, wao wanataka kutunyonya tu na kutudhalilisha. Cha kushangaza sasa, hata huko kwao uchumi wao uko controlled by the government ila tukifanya sie ni kosa, why? Watanzania hamkeni.
 
Mtu ni mfanya biashara ana bambikiziwa kodi na TRA
Mkuu tuwekee ushahidi wa hii tuhuma.
Nani na lini walibambikiwa kodi?
Je walikata rufaa kama sheria husika ya kodi inavyosema.
Kama walikata rufaa tuwekee hapa ushahidi wa nambari ya kesi au shauri pamoja na nakala ya hukumu.
Pia tuwekee nakala ya barua ya kwenda kwa kamishina wa kodi wa TRA kulalamikia hayo madai yao ya kubambikiwa kesi.

Kama hauna hivyo viambata vya ushahidi basi nawewe utakuwa mzushi, mchawi, na mtu hatari kwa mustakabali wa maendeleo ya nchi yetu.
Tena utakuwa kibaraka wa wanyonyaji.
 
paskali, paskali,paskali, Usishangae kuanza na herufi ndogo kwa jina lako, huwa nashangaa makala na post zako humu.Jua wako wengi wajuao lugha za fasihi.Huu ni mtizamo wangu tu lakini nakupa angalizo.
 
Wanabodi,

Uongo ukisemwa sana na kuachwa kurudiwa rudiwa bila kukanushwa, mwisho wake hugeuka ukweli, baada ya kutokukemea magazeti ya nje kuandika uongo kumhusu rais wetu na kumuita majina ya ajabu ajabu, huku sisi na serikali yetu tumenyamaza , sasa ni zamu ya jarida la The Economist, limemtukana rais wetu "dinasauria wa Dodoma" kisha wakamuita a bad president na hadi kumtukana Baba wa Taifa, "a bullheaded socialist!". Pia kumsingizia mambo mengi ya uongo katika toleo lake la hivi karibuni kama nilivyonukuu hapa.


Wakuu Mwanakwetu na Kibanga, kwanza asanteni kwa bandiko hili, pili
tusikubali uwongo huu wa gazeti la The Economist

Uongo Mbalimbali ambazo Hazijakanushwa.
Hi ni baadhi ya uongo mbalimbali ambazo hazijakanushwa hadi leo ambazo mimi kama Mtanzania Mzalendo, kazi yangu ni kushauri tuu.
  1. Rais wetu alipotuhumiwa kuhongwa suti nilipinga na kushauri.Tuhuma za Rais wetu kuhongwa suti: Marekani ituombe radhi ...
  2. Hata kelele kuhusu udikikiteta wa Magufuli ziliposhika kasi nilishauriUdikiteta: Uongo Ukisemwa Sana na Kuachwa Bila Kukanushwa Hugeuka ...
  3. Magufuli aliposemwa vibaya na SABC, nilishauriSerikali ikanushe uongo huu wa SABC kumsema vibaya Rais wetu ...
  4. Rais Magufuli aliposemwa vibaya kuhusu Mimba za utotoni, pia nilishauriJe, Huku Sio Kudhalilishwa Kwa Rais Wetu na Media za Nje?. Jee ...
  5. Juzi kati hapa serikali yetu ilipoitwa Sinister na Authoritarian, pia nilishauri
    Serikali yetu Kuitwa "Sinister" na "Authoritarian": Je, ni kweli ...
Hitimisho.
Uongo ukisemwa sana sana na kuachwa bila kukanushwa, mwisho wake, sio tuu utaonekana kama ni ukweli, bali una hatari ya kugeuka kuwa ukweli kwa sababu kauli huumba!.
Natoa wito kwa Watanzania wote wazalendo wa kweli wa nchi hii, tusikubali rais wetu kutukanwa. kudhalilishwa na kusingiziwa uongo huku sisi wazalendo tupo na tumenyamaza tuu kimya, bila kufanya lolote. Tusikubali.

Paskali
Fungia hili gazeti miaka 5
 
hii ndio economic warfare,na kuna kampeni kubwa sana huko duniani,dunia ya wawekezaji kufanya wawekezaji wasije Tanzania,kila mwekezaji anahakikisha mwenzie haji Tanzania
 
Alikuwa na sifa ya kuwa na ubongo mdogo sana kulinganisha na mwili wake.

Mi mnyama wa kutaka kutumia maguvu guvu sana badala ya akili.

Kama vile Magufuli alivyo na akili ndogo sana kulinganisha na cheo chake. Na anavyotumia maguvu sana badala ya akili.
Dah umepiga mule mule, wabongo si mchezo. Yaani mkulu kama Dinosaur
 
Pascal huyo jamaa ni Rais wako wewe na nani vile?????.
Ukweli siku zote unauma sana.
Ni rais wa Tanzania, ni rais wa Watanzania wote, waliomchagua, wasiomchagua, hata wasiopiga kura!, ndiye rais wa Lowassa, ni rais wa Mbowe, ni rais wa Lissu, ni rais wa Lipumba, ni rais wako, wangu, wetu na Watanzania wote!.

P.
 
Back
Top Bottom