Ni ukweli kuwa tupita kipindi kigumu sana katika kutafuta ajira, na maombi mengi tunayatuma na wala hatuitwi kuja kufanya interview, na wakati huohuo maisha ni magumu kwa namna hii mtu lazima alalamike, na kuona kwamba kuna tasisi au mtu anambania kazi, na hivyo kukata tamaa.
Mimi hadi kabla ya kuitwa kwenye interview pengine nilikuwa mtu wa fikra hizo, kwani nimetafuata ajira kwa mda mrefu sana, nimeandika barua nyingi, nimebadilisha CV za kila namna nikifikiri zitasanisaidia kupata kazi, lakini kwa muda mrefu kulikuwa na ukimya utadhani kama sijatuma kitu vile. kumbe ilikuwa ni suala la wakati kwani ikafikia kipindi nimeitwa na sekretarieti ya ajira nafasi tatu tofauti, na nimechaguliwa hapo jana katika interview ya kuanza tuu niliyoifanya katika maisha yangu hapo sekretarieti.
Cha msingi wenzangu tusikate tamaa, pale unapokataa tamaa ndipo ushindi wamwenzako unapoanzia, tusikatishane tamaa kuhusu Sekretariti ya ajira kwani kama kuna matatizo, hakuna taasisi yoyote hapa Tanzania ambayo haitafanya kazi bila matatizo, cha msingi Sekretariti imepunguza matatizo hayo. Cha msingi kuwa na sifa halafu uzitete sifa hizo kwenye interview utapita kama nilivyopita.
From Seniour job Seeker(As then was)
kwa mfano usingeitwa na hao sekretariet ya ajira ungesema hayo unayo sema? na unaweza kuonesha uhusiano wa kutokukata tamaa na kufanya uchaguliwe na kuitwa kwenye interview?Kaka Elli sisemi kuwa matatizo hayo hayapo, huenda yapo maana wote Tunaijua Tanzania, na unahaki ya kulalamika ili udhaifu huo uondoke, kwa mimi ninachosema licha ya hayo yote tusikate tamaa kutuma maombi kwani hata mimi mingekata tamaa singechaguliwa, kwa sisi ambao hatuna fedha au Ndugu silaha kubwa tuliyonao ni kutokata tamaa, kuwa na sifa na kuzitetea sifa hizo.
mwenzako nimetuma maombi zaidi ya 40, wala sikuitwa, na hayo uliyoyasema yalikuwa yakisemwa toka zamani, lakini kwa vile mimi nimepata wakati huu pamoja na senoiur job seekers wenzangu wengi wamepata napata tafsiri huenda tatizo limepungua.
mim ntaendelea kusema huu ukweli pale kama huna unayemjua imekula kwako . nchi ya wajanja bwana wanachukua mtoto wa mkulima mmoja nafac 70 za kwao ili mjipe matumaini mbona yule jamaa kapata tutasubiri hadi tujute
Sure..mi ni mrugaruga tu wa kijijini huko,ktk kijiji na kata naweza kuwa ndo msomi(?)pekee...nimehangaika kupata kaz kwa mda sana,sikuwa na mtu wala sikuwa namfahamu mtu yoyote ktk mfumo wa nchi..kiufupi hata nlpokuja mjin kufanya interview nlfikia Guest kwa kukosa mwenyeji...lakn tume ya ajira imeniita,ikanisaili na kuniona nafaa..leo nipo ktk ofisi nyeti..masela wamebaki kudhania kuwa mimi eti Usalama wa Taifa..kumbe "mburulaaa" tu toka Nanjilinji nliyepata bahati kwa mgongo wa Tume ya Ajira
Sasa huku ni kusafishana na kuficha maovu, nani asiyejua madudu ya wakubwa ofisini kwa tanzania hii, hili la kusafishana kwa Tanzania ni kivutio mojawapo cha maajabu ya dunia tukipigie kura nacho. HATUDANGANYIKI!!
unafanya ofisi gani? ambapo kuna madudu ya wa kubwa?
ninacho jua mimi kuchafuana na kubambikiana ni tabia ya watu wasio na ueledi ofisini!
alafu great thinker unatuletea mawazo ya kupigia kura kivutio gani? yaani kama unapata nafasi ya kuandika vitu vya aina hii,basi ata kibaruani kwako utakuwa haya ndio mazungumzo yako
kitu cha msingi rudi kwenye heading ya thread! ACHA KUKATISHA WATU TAMAA!
Kukata tamaa ni dhambi kubwa sana yaani nikuto muamini MUNGU
mim ntaendelea kusema huu ukweli pale kama huna unayemjua imekula kwako . nchi ya wajanja bwana wanachukua mtoto wa mkulima mmoja nafac 70 za kwao ili mjipe matumaini mbona yule jamaa kapata tutasubiri hadi tujute