Tusikatishane tamaa kuhusu sekretarieti ya ajira | JamiiForums | The Home of Great Thinkers

Dismiss Notice
You are browsing this site as a guest. It takes 2 minutes to CREATE AN ACCOUNT and less than 1 minute to LOGIN

Tusikatishane tamaa kuhusu sekretarieti ya ajira

Discussion in 'Nafasi za Kazi na Tenda' started by mwinukai, Oct 31, 2012.

 1. m

  mwinukai JF-Expert Member

  #1
  Oct 31, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 1,448
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Ni ukweli kuwa tupita kipindi kigumu sana katika kutafuta ajira, na maombi mengi tunayatuma na wala hatuitwi kuja kufanya interview, na wakati huohuo maisha ni magumu kwa namna hii mtu lazima alalamike, na kuona kwamba kuna tasisi au mtu anambania kazi, na hivyo kukata tamaa.

  Mimi hadi kabla ya kuitwa kwenye interview pengine nilikuwa mtu wa fikra hizo, kwani nimetafuata ajira kwa mda mrefu sana, nimeandika barua nyingi, nimebadilisha CV za kila namna nikifikiri zitasanisaidia kupata kazi, lakini kwa muda mrefu kulikuwa na ukimya utadhani kama sijatuma kitu vile. kumbe ilikuwa ni suala la wakati kwani ikafikia kipindi nimeitwa na sekretarieti ya ajira nafasi tatu tofauti, na nimechaguliwa hapo jana katika interview ya kuanza tuu niliyoifanya katika maisha yangu hapo sekretarieti.

  Cha msingi wenzangu tusikate tamaa, pale unapokataa tamaa ndipo ushindi wamwenzako unapoanzia, tusikatishane tamaa kuhusu Sekretariti ya ajira kwani kama kuna matatizo, hakuna taasisi yoyote hapa Tanzania ambayo haitafanya kazi bila matatizo, cha msingi Sekretariti imepunguza matatizo hayo. Cha msingi kuwa na sifa halafu uzitete sifa hizo kwenye interview utapita kama nilivyopita.


  From Seniour job Seeker(As then was)
   
 2. Elli

  Elli JF-Expert Member

  #2
  Oct 31, 2012
  Joined: Mar 17, 2008
  Messages: 26,829
  Likes Received: 10,141
  Trophy Points: 280
  hahaha alakini hata ka-ukabila, rushwa na upendeleo wanao bhana, ukibisha tu naweka mfano, au kabla hujabisha ngoja niweke mambo wazi....Chuo cha Biashara-CBE Dodoma wapo waliotoa rushwa kwa hao maofisa na wakapata hizo ajira, sipo kwa majungu ila huo ndio ukweli, more to come..../
  Ila kama wamejirekebisha basi ni jambo la heri, sina tatizo nalo wanahitaji kupongezwa.
   
 3. m

  mwinukai JF-Expert Member

  #3
  Oct 31, 2012
  Joined: May 3, 2011
  Messages: 1,448
  Likes Received: 44
  Trophy Points: 145
  Kaka Elli sisemi kuwa matatizo hayo hayapo, huenda yapo maana wote Tunaijua Tanzania, na unahaki ya kulalamika ili udhaifu huo uondoke, kwa mimi ninachosema licha ya hayo yote tusikate tamaa kutuma maombi kwani hata mimi mingekata tamaa singechaguliwa, kwa sisi ambao hatuna fedha au Ndugu silaha kubwa tuliyonao ni kutokata tamaa, kuwa na sifa na kuzitetea sifa hizo.
  mwenzako nimetuma maombi zaidi ya 40, wala sikuitwa, na hayo uliyoyasema yalikuwa yakisemwa toka zamani, lakini kwa vile mimi nimepata wakati huu pamoja na senoiur job seekers wenzangu wengi wamepata napata tafsiri huenda tatizo limepungua.
   
 4. Obama wa Bongo

  Obama wa Bongo JF-Expert Member

  #4
  Oct 31, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 4,771
  Likes Received: 2,506
  Trophy Points: 280
  naomba ninukuu yafutayo! soma mhubiri 9:11
  [SUP]11 [/SUP]I returned, and saw under the sun, that the race is not to the swift, nor the battle to the strong, neither yet bread to the wise, nor yet riches to men of understanding, nor yet favour to men of skill; but time and chance happeneth to them all.

  11 Nikarudi, na kuona chini ya jua, ya kwamba mashindano si mwepesi, wala vita kwa nguvu, wala wenye hekima wapatao chakula, wala utajiri bado watu wa ufahamu, wala neema wenye ustadi; lakini wakati na bahati huwapata wote.  nawaomba vijana wenzangu haya maneno yawatie nguvu mnapoona mnakata tamaa ya kupata ajira!
   
 5. Nicole

  Nicole JF-Expert Member

  #5
  Oct 31, 2012
  Joined: Sep 7, 2012
  Messages: 4,284
  Likes Received: 10
  Trophy Points: 0
  mkuu mie nko private nazuga ila future ya fani yangu naiona govt,so nasikilizia usail wa nov hebu nipe abc's za hayo maki2
   
 6. Ngaliba Dume

  Ngaliba Dume JF-Expert Member

  #6
  Oct 31, 2012
  Joined: Oct 6, 2010
  Messages: 1,604
  Likes Received: 1,716
  Trophy Points: 280
  Sure..mi ni mrugaruga tu wa kijijini huko,ktk kijiji na kata naweza kuwa ndo msomi(?)pekee...nimehangaika kupata kaz kwa mda sana,sikuwa na mtu wala sikuwa namfahamu mtu yoyote ktk mfumo wa nchi..kiufupi hata nlpokuja mjin kufanya interview nlfikia Guest kwa kukosa mwenyeji...lakn tume ya ajira imeniita,ikanisaili na kuniona nafaa..leo nipo ktk ofisi nyeti..masela wamebaki kudhania kuwa mimi eti Usalama wa Taifa..kumbe "mburulaaa" tu toka Nanjilinji nliyepata bahati kwa mgongo wa Tume ya Ajira
   
 7. Lyamber

  Lyamber JF-Expert Member

  #7
  Oct 31, 2012
  Joined: Jul 24, 2012
  Messages: 4,196
  Likes Received: 2,638
  Trophy Points: 280
  kwa mfano usingeitwa na hao sekretariet ya ajira ungesema hayo unayo sema? na unaweza kuonesha uhusiano wa kutokukata tamaa na kufanya uchaguliwe na kuitwa kwenye interview?
   
 8. x

  xiande Member

  #8
  Nov 1, 2012
  Joined: Oct 3, 2012
  Messages: 90
  Likes Received: 0
  Trophy Points: 0
  mim ntaendelea kusema huu ukweli pale kama huna unayemjua imekula kwako . nchi ya wajanja bwana wanachukua mtoto wa mkulima mmoja nafac 70 za kwao ili mjipe matumaini mbona yule jamaa kapata tutasubiri hadi tujute
   
 9. v

  valid statement JF-Expert Member

  #9
  Nov 1, 2012
  Joined: Sep 18, 2011
  Messages: 2,737
  Likes Received: 177
  Trophy Points: 160
  Unahitaji kuingia darasani ukasome vizuri somo la 'uvumilivu na kutokata tamaa'.
  Kisha uende tution ya 'kupata bahati na kuajiriwa bila kumjua mtu'.

  Baada ya hapo unaweza sasa kufanya mtihani wa kutafuta ajira.
   
 10. Matokeo1

  Matokeo1 JF-Expert Member

  #10
  Nov 1, 2012
  Joined: Oct 10, 2012
  Messages: 228
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Sasa huku ni kusafishana na kuficha maovu, nani asiyejua madudu ya wakubwa ofisini kwa tanzania hii, hili la kusafishana kwa Tanzania ni kivutio mojawapo cha maajabu ya dunia tukipigie kura nacho. HATUDANGANYIKI!!
   
 11. Obama wa Bongo

  Obama wa Bongo JF-Expert Member

  #11
  Nov 2, 2012
  Joined: May 10, 2012
  Messages: 4,771
  Likes Received: 2,506
  Trophy Points: 280
  unafanya ofisi gani? ambapo kuna madudu ya wa kubwa?
  ninacho jua mimi kuchafuana na kubambikiana ni tabia ya watu wasio na ueledi ofisini!
  alafu great thinker unatuletea mawazo ya kupigia kura kivutio gani? yaani kama unapata nafasi ya kuandika vitu vya aina hii,basi ata kibaruani kwako utakuwa haya ndio mazungumzo yako
  kitu cha msingi rudi kwenye heading ya thread! ACHA KUKATISHA WATU TAMAA!
  Kukata tamaa ni dhambi kubwa sana yaani nikuto muamini MUNGU
   
 12. Matokeo1

  Matokeo1 JF-Expert Member

  #12
  Nov 2, 2012
  Joined: Oct 10, 2012
  Messages: 228
  Likes Received: 2
  Trophy Points: 35
  Acha unafiki wewe unaejiita Obama wa Bongo, inaelekia hata wewe ni walewale wanafiki wa kibongo mnafagilia kitu flan au mtu flani ili mpate kitu flani, hapa ni sehemu ya kujiachia kimawazo na kero zetu, mambo yanayofanyika ofisin kwa watu ni ya ajabu sana na hayajawahi kutokea kwingine ila Tanzania tu, vitisho, rushwa za wazi wazi, ukabila, udini, undugu, jikumbushie haya BOT, TANROADS, SENSA, hata huko sipakubali sana, mi nimejibu kutokana na huyu jamaa siwezi kurudi kwenye THREAD
  [​IMG] By Ngaliba Dume [​IMG]
  Sure..mi ni mrugaruga tu wa kijijini huko,ktk kijiji na kata naweza kuwa ndo msomi(?)pekee...nimehangaika kupata kaz kwa mda sana,sikuwa na mtu wala sikuwa namfahamu mtu yoyote ktk mfumo wa nchi..kiufupi hata nlpokuja mjin kufanya interview nlfikia Guest kwa kukosa mwenyeji...lakn tume ya ajira imeniita,ikanisaili na kuniona nafaa..leo nipo ktk ofisi nyeti..masela wamebaki kudhania kuwa mimi eti Usalama wa Taifa..kumbe "mburulaaa" tu toka Nanjilinji nliyepata bahati kwa mgongo wa Tume ya Ajira
   
 13. A

  Agrodealer Senior Member

  #13
  Nov 4, 2012
  Joined: Mar 19, 2011
  Messages: 108
  Likes Received: 1
  Trophy Points: 0
  sina comment ila kilichotokea usaili wa weo kwa mikoani ni aibu tupu eti haiwezekani ma intellectual na akili zao watufanyishe interview watu zaid ya 70 wachaguliwe 5 kuingia oral na 7 watoke kwenye 98 huu ni ubabaishaji na usumbufu.wanaochaguliwa mtoto wa mkulima 1 rejesha hatufichani bana zali likikudondoke mshukuru mungu na uwaombee mungu wenzioover.
   
 14. Brother James

  Brother James Senior Member

  #14
  Nov 7, 2012
  Joined: Feb 21, 2012
  Messages: 158
  Likes Received: 16
  Trophy Points: 35
  Mmhhhhh.......mimi napita tu kwani haya ya Sekretariat ya Ajira endeleeni nayo wenyewe. watu kila siku wanalalamika, hivi kuna mtu anaweza kuomba nafasi fulani ya ajira bila kuwa na sifa? Kama yupo huyo atakuwa taahira kwa kweli....kwa ushindani huu wa ajira sidhani kama intellectuals wanaweza kuumiza pesa zao kwa applications ktk nafasi usiyo-qualify, kama mpo badilikeni kabisaaa. Ila kwa wale wenye sifa sio siri hii Secretariat ya Ajira Bongo wanatakiwa kukumbushwa kuwa angalau wawaite watu wote wenye sifa ktk interviews na kuwapa nafasi ya kuwasikiliza ndio wawaengue. Ni mawazo yangu kwa hili jambo.
   
Loading...