MtuHabari
JF-Expert Member
- Oct 16, 2020
- 321
- 1,020
View: https://youtu.be/KjjOEeWrH-g?si=0wWx5xKmO4wRtYdv
Yapo mambo hayafutiki mioyoni lakini kubwa hasa ni kudhalilika au kunyanyaswa na mtu aliye kuzidi cheo.
Makonda alipokuwa RC alimfedhehesha sana na hadharani DC wa Kinondoni wakati huo Daniel Chongolo hadi kumtukana na kiumri Chongolo ni mkubwa kwa Makonda alistahili heshima.
Leo hii Chongolo ndio Katibu mkuu boss wa Makonda aliye Katibu itikadi na uenezi.
Utata unakuja kuwa Makonda akikosea na kuonywa atafikiri ni visasi vya yaliyotokea nyuma, na Chongolo amri zake zisipotekelezwa atafikiri bado huyu ananidharau kama wakati ule!
Hapo ni kama sukari imekolezwa kwenye supu ikaungwa na nazi.
Labda kwa vile mwenyekiti (ambaye katika CCM ndio alfa na omega) anampenda Makonda amuondoe Chogolo.