Tusiende huku ni hatari

Tusiende huku ni hatari

tramadol

JF-Expert Member
Joined
Oct 10, 2015
Posts
5,383
Reaction score
4,323
Suala la madini na makinikia yetu tuyashughulikia kwa busara ili kuweka nchi salama.

Yasitukute yaliyowapata wenzetu kwa hao wanaojiita Wazungu kutuzunguka mlango wa nyuma na kutugawa.

Madini kwao ni moja ya bidhaa zinazowajengea miundombinu kwa kiwango juu sana.

Watanzania tuwe wamoja Katika kutetea rasilimali za nchi yetu.
 
vlcsnap-2017-06-17-19h03m16s307.png

Mandela akifanya upatanisho Zaire ya zamani Sasa DRC na Rais Mobutu kuondoka na Kabila kuchukua nchi
 
  • Thanks
Reactions: MC7
vlcsnap-2016-06-07-13h32m57s227.png
Miundo mbinu ya wenzetu ...USA
 
Suala la madini na makinikia yetu kuyashughulikia kwa busara ili kuweka nchi salama.

Yasitukute yaliyowapata wenzetu kwa hao wanaojiita Wazungu kutuzunguka mlango wa nyuma na kutugawa.

Madini kwao ni moja ya bidhaa zinazowajengea miundombinu kwa kiwango juu sana.

Watanzania tuwe wamoja Katika kutetea rasilimali za nchi yetu.
Mkapa na Kikwete watajwe au wasitajwe?
Tuanzie hapo.
 
Mbona wameshatugawa siku nyingi. Fuatilia uzi wako kwa makini. Uchangiaji ndo utabaini makundi yetu. Tanzania kwanza mengine baadae.
 
Mbona wameshatugawa siku nyingi. Fuatilia uzi wako kwa makini. Uchangiaji ndo utabaini makundi yetu. Tanzania kwanza mengine baadae.
Tunapinga dhana ya aina yoyote ya kuligawa Taifa na wanainchi wake kwa faida yao.
 
Mkapa na Kikwete watajwe au wasitajwe?
Tuanzie hapo.
Hilo huwezi kulizuia watatajwa tu.Wameshiriki ktk suala la madini kila mmoja kwa awamu yake.Sasa ukizuia kuwataja tuwataje wakina nani?

Ben Mkapa na Dr Kikwete wakiwa Marais kwa wakati tofauti ndiyo walioleta mapinduzi ktk sekta ya madini kutoka kwa umiliki wa wazawa kwenda kwa wawekezaji wakubwa wa Nje.
 
Tuwatajie hapa nyumbani au tusubiri kwenye ulingo wa kimataifa???
 
NAJUA WAJUA LAKINI NAKUJUZA ZAIDI KUHUSU SAVIMBI a FANTOCHE ALIYEKUWA KIBARAKA WA WAZUNGU NCHINI KWAKE

Jonas Malheiro Savimbi, Moja ya Vibaraka wa karne hapa Afrika,.Wakati ule Augustino Neto na MPLA wakiwa wamefanikiwa kuikomboa Angola kutoka kwenye Ukoloni wa Wareno ndipo akaibuka Savimbi akipambana na Nchi yake Mwenyewe kutokea Msituni kwa miaka 26 akisaidia Makaburu kupora dhahabu.

Inasemekana Savimbi akiwa porini alipata kila kitu, kuanzia Silaha na starehe zote alizozitaka yeye na kikosi chake cha wanamgambo wa chama chake maarufu kama UNITA,...aliletewa Silaha za kisasa kutoka Ulaya na hata Fedha akapambana mwanzo mwisho dhidi ya Taifa lake Mwenyewe akijiita Kamanda Jenerali.

Mwisho wa Ubaya aibu, umdhaniaye siye kumbe ndiye, Savimbi aliuawa Kinyama 22 feb 2002 akiwa na miaka 67, aliuawa huku akilindwa na walinzi wake 21 (body guards) huko porini jirani na Mto Luvuei ktk Jimbo la Moxico.

Kwa Miaka yote ya Utumishi Wa U-Kibaraka haikuwa rahisi kumkamata Savimbi, kwani kabla ya hapo alikuwa ameshakwepa Majaribio 12 ya kumuua, alisharipotiwa amekufa mara 15 lakini anaibuka, ila ajabu ni kwamba siku hii aliyouawa Operation ilikuwa Rahisi sana....kwanza kabisa alidhoofishwa kwa Mawasiliano yake yote kukatwa, redio zikawa kimya,..Kisha akavamiwa na majeshi akiwa amejipumzisha, haya yalikuwa ni mashambulizi ya kushtukiza sana..Savimbi alipigwa Risasi 15...Risasi Moja ya Koromeo.. Mbili za kichwa..na zingine 12 zikatawanywa Miguuni, Mikononi na Kifuani..Akafa na bunduki Mkononi, akazikwa huko huko chini ya Mti.

Kifupi Majeshi ya Angola yalishamshindwa Savimbi, Kufa kwake inasemekana aliuawa na wale wazungu aliowasaidia kupora Dhahabu ya Angola... Walipotosheka wakammaliza.. Vibaraka aina ya Savimbi wamejaa Afrika, Wapo Kila Nchi, Kuwajua hawa ni rahisi tu..Gusa Mambo ya Msingi na hasa hasa Rasilimali.
 
Mkapa na Kikwete watajwe au wasitajwe?
Tuanzie hapo.
mawio.jpg

Wewe ukiandika habari kama hii inategemea Serikali ikuache tu.Unataka kuleta mtafaruku ktk nchi Hata uhakiki wa habari wenyewe Haipo.
 
Back
Top Bottom