Tusidanganyane wana CHADEMA, Slaa asingefikisha kura milioni sita

ibesa mau

JF-Expert Member
Sep 17, 2015
2,109
1,692
Nimekuta mjadala wa wana chadema umepamba moto kwamba wakijadiliana angekuwa Slaa angevuka kura zile alizopata Lowasa lakinj ukweli ni kwamba Slaa huyu ninaye mfahamu kura zake zisingevuka milioni nne.
 
Ni kweli kabisa, labda nusu yake, Lowwsa ameleta hamasa ya ajabu ukawa. Na hata kuna majimbo ambayo imechukua decades kuyachukua kama monduli na longido
 
Si tuliambiwa kuwa lowassa alihama na mtaji wake wa wanaccm ndo waliofanya ifikie m6 hilo halina ubishi
 
Nimekuta mjadala wa wana chadema umepamba moto kwamba wakijadiliana angekuwa Slaa angevuka kura zile alizopata Lowasa lakinj ukweli ni kwamba Slaa huyu ninaye mfahamu kura zake zisingevuka milioni nne.
CCM pekee ndio wanaomsifia Dr Slaa!
 
Kama wachambuzi wengi makini wa siasa walivyotabiri, Chadema imeshindwa kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi october 2015. Ingawa kushindwa huko kwa Chadema kumechangiwa na mambo mengi, lakini kubwa zaidi ni makosa yaliyofanywa na mwenyekiti wake mh. Freeman Mbowe kushinikiza chama kimsimamishe mgombea asiyekubalika.

Ingawa baadhi ya watu wakiangalia juu juu wanaona mgombea aliyeletwa na Mbowe ameleta manufaa, lakini ukiangalia hesabu kwa makini utaona kuwa mgombea huyo hajakinufaisha chama na badala yake amekiletea chama hicho migogoro na kukitenganisha na agenda yake kuu ya ufisadi.

Mwaka 2005 mgombea wa Chadema mh. Freeman Mbowe alipata asilimia 5.88 ya kura za urais. Mwaka 2010 mgombea Dr. Slaa alipata asilimia 27.05. Hii ni tofauti ya asilimia 21.17 au ongezeko la asilimia 360 ikilinganishwa na 2005.

Vilevile, mwaka 2005 Chadema ilipata majimbo 5. Mwaka 2010 ilipata majimbo 23. Ongezeko hili la majimbo 18 ni sawa na asilimia 360.

Mafanikio haya waliyapata Chadema bila kuhitaji msaada wa mgombea wa kuazima toka CCM. Kama waliweza wenyewe kufika hapa, ni sahihi kuamini kuwa wangeweza kwenda mbali zaidi.

katika uchaguzi wa mwaka huu, Chadema wamepata asilimia 39.97. Hii ni tofauti ya asilimia 12.92 ikilinganishwa na matokeo ya chadema ya mwaka 2010. Hapa utaona kuwa ongezeko aliloleta mgombea "wa kuazima toka CCM" ni dogo kuliko ongezeko aliloleta Slaa la asilimia 21.17.

Kwenye ubunge, mwaka huu Chadema imepata majimbo 39. Hili ni ongezeko la majimbo 16 ambayo ni sawa na ongezeko la aslimia 69.6. Hapa utaona kuwa mgombea "wa kuazima toka CCM" ameshindwa kuongeza kiasi cha majimbo kama alichoongeza Slaa mwaka 2010.

Ikumbukwe kuwa mgombea wa mwaka huu aliungwa mkono na vyama vinne vya upinzani tofauti na miaka iliyopita ambayo mgombea wa chadema alikuwa anasimama peke yake. Kuungwa mkono huku kulimfanya pia mgombea huyo awe na wabunge wengi wa majimbo (47) wanaompigia kampeni Bara na Visiwani. Dr. Slaa alikuwa na wabunge watano (5) tu waliompigia kampeni.
Pamoja na kuungwa mkono huko lakini bado mgombea hajafanikiwa kuleta mafanikio zaidi ya mwaka 2010.

Hitimisho:
Woga wa Mbowe umeiponza Chadema bure. Chadema ilishaanza kujiimarisha kitaasisi na sasa sura ya kitaasisi imebomolewa na kujengwa sura ya kutegemea jina la mtu mmoja.

Kauli za Mbowe na viongozi wengine wa Chadema kuwa hawawezi kushinda uchaguzi bila kuchukua kigogo toka CCM itawatafuna siku za usoni na kuwakatisha tamaa wafuasi wao kwenye chaguzi zijazo iwapo hawatapata kigogo wa CCM wa kugombea kupitia Chadema.

Chadema ina jukumu kubwa la kutafuta mtu wa kufidia nafasi ya Dr. Slaa. Kihesabu hakuna mtu aliyevuna mafanikio makubwa kwa Chadema kama Dr. Slaa. Lowassa ameshafikia kilele chake, haongezeki tena nguvu. Kama ameshindwa kufikia level ya Dr. Slaa katika uchaguzi huu, basi hataifikia tena.

Uchaguzi huu ni fundisho kwa vyama kuthamini mafanikio ya hatua kwa hatua inayojipatia yenyewe kwa kuheshimu misingi yake kuliko kukimbilia tamaa za kuenda ikulu kwa kubomoa misingi iliyojengwa kwa miaka mingi.
 
Nimekuta mjadala wa wana chadema umepamba moto kwamba wakijadiliana angekuwa Slaa angevuka kura zile alizopata Lowasa lakinj ukweli ni kwamba Slaa huyu ninaye mfahamu kura zake zisingevuka milioni nne.

Acha kumvunjia heshima,Lowassa hakupata kura milioni 6,alipata kura zaidi ya milioni 10.Waulize necccm wanaujuwa muziki wake hadi imepelekea papaaa mukulu kutangaza 5/11/ kuwa siku ya mapumziko ili kuficha aibu ya mdololo uliosababishwa na ukimya wa watu kwa kuamua kususia sherehe feki za kumuapisha mshindi wa kuchongwa.
 
Kama wachambuzi wengi makini wa siasa walivyotabiri, Chadema imeshindwa kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi october 2015. Ingawa kushindwa huko kwa Chadema kumechangiwa na mambo mengi, lakini kubwa zaidi ni makosa yaliyofanywa na mwenyekiti wake mh. Freeman Mbowe kushinikiza chama kimsimamishe mgombea asiyekubalika.

Ingawa baadhi ya watu wakiangalia juu juu wanaona mgombea aliyeletwa na Mbowe ameleta manufaa, lakini ukiangalia hesabu kwa makini utaona kuwa mgombea huyo hajakinufaisha chama na badala yake amekiletea chama hicho migogoro na kukitenganisha na agenda yake kuu ya ufisadi.

Mwaka 2005 mgombea wa Chadema mh. Freeman Mbowe alipata asilimia 5.88 ya kura za urais. Mwaka 2010 mgombea Dr. Slaa alipata asilimia 27.05. Hii ni tofauti ya asilimia 21.17 au ongezeko la asilimia 360 ikilinganishwa na 2005.

Vilevile, mwaka 2005 Chadema ilipata majimbo 5. Mwaka 2010 ilipata majimbo 23. Ongezeko hili la majimbo 18 ni sawa na asilimia 360.

Mafanikio haya waliyapata Chadema bila kuhitaji msaada wa mgombea wa kuazima toka CCM. Kama waliweza wenyewe kufika hapa, ni sahihi kuamini kuwa wangeweza kwenda mbali zaidi.

katika uchaguzi wa mwaka huu, Chadema wamepata asilimia 39.97. Hii ni tofauti ya asilimia 12.92 ikilinganishwa na matokeo ya chadema ya mwaka 2010. Hapa utaona kuwa ongezeko aliloleta mgombea "wa kuazima toka CCM" ni dogo kuliko ongezeko aliloleta Slaa la asilimia 21.17.

Kwenye ubunge, mwaka huu Chadema imepata majimbo 39. Hili ni ongezeko la majimbo 16 ambayo ni sawa na ongezeko la aslimia 69.6. Hapa utaona kuwa mgombea "wa kuazima toka CCM" ameshindwa kuongeza kiasi cha majimbo kama alichoongeza Slaa mwaka 2010.

Ikumbukwe kuwa mgombea wa mwaka huu aliungwa mkono na vyama vinne vya upinzani tofauti na miaka iliyopita ambayo mgombea wa chadema alikuwa anasimama peke yake. Kuungwa mkono huku kulimfanya pia mgombea huyo awe na wabunge wengi wa majimbo (47) wanaompigia kampeni Bara na Visiwani. Dr. Slaa alikuwa na wabunge watano (5) tu waliompigia kampeni.
Pamoja na kuungwa mkono huko lakini bado mgombea hajafanikiwa kuleta mafanikio zaidi ya mwaka 2010.

Hitimisho:
Woga wa Mbowe umeiponza Chadema bure. Chadema ilishaanza kujiimarisha kitaasisi na sasa sura ya kitaasisi imebomolewa na kujengwa sura ya kutegemea jina la mtu mmoja.

Kauli za Mbowe na viongozi wengine wa Chadema kuwa hawawezi kushinda uchaguzi bila kuchukua kigogo toka CCM itawatafuna siku za usoni na kuwakatisha tamaa wafuasi wao kwenye chaguzi zijazo iwapo hawatapata kigogo wa CCM wa kugombea kupitia Chadema.

Chadema ina jukumu kubwa la kutafuta mtu wa kufidia nafasi ya Dr. Slaa. Kihesabu hakuna mtu aliyevuna mafanikio makubwa kwa Chadema kama Dr. Slaa. Lowassa ameshafikia kilele chake, haongezeki tena nguvu. Kama ameshindwa kufikia level ya Dr. Slaa katika uchaguzi huu, basi hataifikia tena.

Uchaguzi huu ni fundisho kwa vyama kuthamini mafanikio ya hatua kwa hatua inayojipatia yenyewe kwa kuheshimu misingi yake kuliko kukimbilia tamaa za kuenda ikulu kwa kubomoa misingi iliyojengwa kwa miaka mingi.

ukweli mchungu.
 
kuna watu wanajadili vitu kwa ushabiki sana. Ukweli ni kwamba kwa mwaka 2015 chini ya mwamvuli wa UKAWA angesimamishwa mgombea yoyote angepata kura alizopata Lowassa. Swali ni Je, CUF, NCCR MAGEUZI na CHADEMA KILA KIMOJA KINGESIMAMISHA MGOMBEA WAKE JE LOWASSA ANGESIMAMA KWA KUPITIA CHADEMA PEKEE ANGEPATA ASILIMIA ALIZOPATA. UKWELI NI NOOO! ANGEPATA ASILIMIA KATI YA 25 HADI 32 KWA MTAZAMO WANGU. NA JE ASINGEKUWA NA MABILIONI YA FEDHA ANGEFIKISHA ASILIMIA ALIZOPATA UKWELI ANGEPATA CHINI YA ALIZOPATA SLAA IWAPO ANGEGOMBEA KUPITIA CHADEMA. KWANINI? NI KWASABABU MBALI NA HELA NA KUKATWA KWAKE NA CCM, LOWASSA SI MJENGA HOJA, HANA USHAWISHI KATIKA KUONGEA KWAKE, HAFAFANUI MAMBO, NI MTU ANAYETOA AHADI TU KUWA NIKIWA RAIS MAJI YATATOKA! NYUMBA ZA NYASI ZITAISHA! HAAMINI KATIKA UFANYAJI KAZI WA KITAASISI, BALI YEYE ANAJIONA NDIYE TAASISI, HUYU HAWEZI KUITOA NCHI ILIPO UKAWA ITAFUTE MBADALA SAHIHI
 
Kama wachambuzi wengi makini wa siasa walivyotabiri, Chadema imeshindwa kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika mwezi october 2015. Ingawa kushindwa huko kwa Chadema kumechangiwa na mambo mengi, lakini kubwa zaidi ni makosa yaliyofanywa na mwenyekiti wake mh. Freeman Mbowe kushinikiza chama kimsimamishe mgombea asiyekubalika.

Ingawa baadhi ya watu wakiangalia juu juu wanaona mgombea aliyeletwa na Mbowe ameleta manufaa, lakini ukiangalia hesabu kwa makini utaona kuwa mgombea huyo hajakinufaisha chama na badala yake amekiletea chama hicho migogoro na kukitenganisha na agenda yake kuu ya ufisadi.

Mwaka 2005 mgombea wa Chadema mh. Freeman Mbowe alipata asilimia 5.88 ya kura za urais. Mwaka 2010 mgombea Dr. Slaa alipata asilimia 27.05. Hii ni tofauti ya asilimia 21.17 au ongezeko la asilimia 360 ikilinganishwa na 2005.

Vilevile, mwaka 2005 Chadema ilipata majimbo 5. Mwaka 2010 ilipata majimbo 23. Ongezeko hili la majimbo 18 ni sawa na asilimia 360.

Mafanikio haya waliyapata Chadema bila kuhitaji msaada wa mgombea wa kuazima toka CCM. Kama waliweza wenyewe kufika hapa, ni sahihi kuamini kuwa wangeweza kwenda mbali zaidi.

katika uchaguzi wa mwaka huu, Chadema wamepata asilimia 39.97. Hii ni tofauti ya asilimia 12.92 ikilinganishwa na matokeo ya chadema ya mwaka 2010. Hapa utaona kuwa ongezeko aliloleta mgombea "wa kuazima toka CCM" ni dogo kuliko ongezeko aliloleta Slaa la asilimia 21.17.

Kwenye ubunge, mwaka huu Chadema imepata majimbo 39. Hili ni ongezeko la majimbo 16 ambayo ni sawa na ongezeko la aslimia 69.6. Hapa utaona kuwa mgombea "wa kuazima toka CCM" ameshindwa kuongeza kiasi cha majimbo kama alichoongeza Slaa mwaka 2010.

Ikumbukwe kuwa mgombea wa mwaka huu aliungwa mkono na vyama vinne vya upinzani tofauti na miaka iliyopita ambayo mgombea wa chadema alikuwa anasimama peke yake. Kuungwa mkono huku kulimfanya pia mgombea huyo awe na wabunge wengi wa majimbo (47) wanaompigia kampeni Bara na Visiwani. Dr. Slaa alikuwa na wabunge watano (5) tu waliompigia kampeni.
Pamoja na kuungwa mkono huko lakini bado mgombea hajafanikiwa kuleta mafanikio zaidi ya mwaka 2010.

Hitimisho:
Woga wa Mbowe umeiponza Chadema bure. Chadema ilishaanza kujiimarisha kitaasisi na sasa sura ya kitaasisi imebomolewa na kujengwa sura ya kutegemea jina la mtu mmoja.

Kauli za Mbowe na viongozi wengine wa Chadema kuwa hawawezi kushinda uchaguzi bila kuchukua kigogo toka CCM itawatafuna siku za usoni na kuwakatisha tamaa wafuasi wao kwenye chaguzi zijazo iwapo hawatapata kigogo wa CCM wa kugombea kupitia Chadema.

Chadema ina jukumu kubwa la kutafuta mtu wa kufidia nafasi ya Dr. Slaa. Kihesabu hakuna mtu aliyevuna mafanikio makubwa kwa Chadema kama Dr. Slaa. Lowassa ameshafikia kilele chake, haongezeki tena nguvu. Kama ameshindwa kufikia level ya Dr. Slaa katika uchaguzi huu, basi hataifikia tena.

Uchaguzi huu ni fundisho kwa vyama kuthamini mafanikio ya hatua kwa hatua inayojipatia yenyewe kwa kuheshimu misingi yake kuliko kukimbilia tamaa za kuenda ikulu kwa kubomoa misingi iliyojengwa kwa miaka mingi.

Umesema kweli. Agenda ya ufisadi ingemfikisha Dr Slaa ikulu hata ccm waadilifu nao wangempa kura nyingi pia.
 
Nimekuta mjadala wa wana chadema umepamba moto kwamba wakijadiliana angekuwa Slaa angevuka kura zile alizopata Lowasa lakinj ukweli ni kwamba Slaa huyu ninaye mfahamu kura zake zisingevuka milioni nne.

Kama mlisema ni heri mngepigia jiwe au maiti, iweje sasa mseme mngemnyima kura Dr Slaa? Kwani Slaa si zaidi ya Jiwe? Huu ni mkakati wa Mbowe kuaminisha watu kuwa alifanya maamuzi sahihi...
#MboweMustGo!
 
Angefikisha na zaidi sababu wana ccm wengi wangempa kura na ambao jawana ushabiko wa chama chochote pia bila kuombwa kwa kuvutiwa na kazi yake ya upinzani kwa miaka mingi.

Acha kutafuta kujipoozesha mtamkumbuka sana tu.
 
Humu ndani kila mtu anajidai mtaalamu wa kuchambua mambo... ni kichaa tu atakae kubali kwamba eti dr slaa angeshinda urais.. mimi nasema hivii hata angesimama nyerere upinzani wasingepata urais.. mnasahau mabao ya mkono ya ccm vile yamekula kura halali za ukawa!? Uchaguzi ungekya fair lowasa angekua presidaa tayari... hv kura amepata lkn kaibiwa nyingi sana ba ushahidi upo wazi.. kuhusu kujenga chama nazo ni porojo.. wengi mmesahau comments zenu wakati zito anatoka chadema.. mlitegemea chadema ife lkn imekua tofauti sababu chama ni timu work hamna mtu mmoja anaeweza kufanya maajabu..uthibitisho wa hilo tizama act na zito... dk slaa zama zake zinepita tayari sasa ni wkt mpya.. poleni mnaishabikia mtu...
 
...ahsante sana kwa maelezo mafupi lakini yanayoekeweka vizuri...
 
Mkuu binafsi nautafuta sana ushahidi wa kura kuibiwa na haswa utofauti wa fomu za urais majimboni na ule aliusoma lubuva
Can you help me for this mkuu?
 
  • Thanks
Reactions: nao
Angefikisha na zaidi sababu wana ccm wengi wangempa kura na ambao jawana ushabiko wa chama chochote pia bila kuombwa kwa kuvutiwa na kazi yake ya upinzani kwa miaka mingi.

Acha kutafuta kujipoozesha mtamkumbuka sana tu.

Hata mimi ambae sina chama nimepigia CCM kwa hasira..
Tamaa itaiua CDM...
Ikulu mipango...si gia za angani

Nakwambia CCM ilivyochokwa wangemweka Slaa chini ya UKAWA hata baadhi ya CCM wangewapa kura...
Otherwise mtu ambaye si CDM au UKAWA ampigie kura Luwasa kwa lipi aswa?????

Na wasubiri anguko rasmi 2020 maana watavuna watu kwa gia ipi? Wao na Ufisadi damu damu...
JPM by that time atakuwa ana showcase tu..
 
Ni kweli kabisa, labda nusu yake, Lowwsa ameleta hamasa ya ajabu ukawa. Na hata kuna majimbo ambayo imechukua decades kuyachukua kama monduli na longido

Simuungi sana Lowassa mkono, lkn ilibidi nimuunge mkono na nimeiona impact yake. Naamini kabisa, kama sio nguvu na utisho wa Lowassa, CCM wangeshinda Zanzibar, lkn nguvu nyingi na uwekezaji mwingi CCM waliufanya huku Tanganyika na hivyo uchaguzi 'ukavurugika' Zanzibar.

Vv
 
Back
Top Bottom