Tusi Haliui.

Tusi Haliui.

Idd Ninga

JF-Expert Member
Joined
Nov 18, 2012
Posts
5,539
Reaction score
4,854
TUSI HALIUI.
1)katu halinyongi tusi,tukanwa utukanike.
Kama huna ukakasi,basi acha wasikike.
Tena wape mafulusi,kwa dharau uwacheke.
Wala haliui tusi,kwa mtu mwenye hekima.

2)kwako ni kama uasi,vipi yakija mateke.
Aliyaweza abasi,vipi udharaulike.
Kosa dogo nimkosi,vumilia lisifike.
Wala haliui tusi,kwa mtu mwenye hekima.

3)paka shume siyo pusi,wanga acha na waruke.
Ukiwanyima nanasi,wataanzisha makeke.
Watakutia najisi,utaishia lea upweke.
Wala haliui tusi,kwa mtu mwenye hekima.

4)alieanza kwa kasi,tuliona mwisho wake.
Wako mapema sa basi,vipi kutwa uwasake.
Ahadi yawa mkasi,kuwachinja watu wake.
Wala haliui tusi,kwa mtu mwenye hekima.

5)simba umewa farasi,sirisiri tukucheke
Na jeraha la utosi,litawaka lifumuke.
Mbona hilo ni rahisi,vipi lisivumilike.
Wala haliui tusi,kwa mtu mwenye hekima

Shairi=HALIUI TUSI
Mtunzi=Idd Ninga wa Tengeru Arusha.
+255624010160
iddyallyninga@gmail.com
Facebook page=Idd ninga mashairi.
 
Back
Top Bottom