Tushee haya MAUMIVU!

Pole sana
 
Kuna wakati tunalazimika kuweka matatizo yetu pembeni na kumshukuru Mungu, Baadae mambo yakiwa Sawa Utatazama ulipo toka na Mapito uliyopitia na kufurahia kwamba hukukata tamaa, Mungu akupe faraja katika kipindi hiki kigumu.
ni kweli kabisa yatupasa kuweka matatizo yetu kando na kutizama mbele kwa matumaini,Mungu ni wetu sote nae anajua hitaji la mioyo yetu!
 
High end, yaani zile zenye vuwango vya juu, mfano km ni simu ningekwambia iPhone au Samsung

Mambo yamekua mengi na Mengi yamekua Mambo
anhaa nimeelewa ndugu bahati mbaya uwezo wangu ni mdogo kwa sasa na hivi vifaa ni gharama kubwa
 
Pole sana kijana,I wish ningekuwa na uwezo wa kukusaidia...but don't feel so down,siku yako ipo
 
Najaribu kuvaa viatu vyako daaah! Aisee hii dunia haina usawa kabisa!

MUNGU akutimizie haja ya moyo wako mkuu

Young kilimanjaro
 
Ulirudi kwa Daktari aliyevi recommend hivyo vifaa ili akupe mbadala? Au ndo umekuja huku kulalama...? Unaonekana Wewe ni mgonjwa ambaye hajajikubali. Ushauri wangu wewe mwenyewe jikubali.Mfano Manara wa Simba amejitahidi anasonga mbele.Wewe jinsi unavyojipambanua yaelekea unaona aibu hata kuvivaa hivyo vifaa.
 
Dooh..
 
Mkuu hujamtendea haki kwani hapa jukwaani hakufai kuomba ushauri, kupeana faraja kwa matatizo yanayo tutokea kila siku.kabla hujafa hujaumbika.
 
Pole sana KAMANDA kwa pamoja tuliombee jiwe life maisha yawe laini tutapeana ajira wenyewe kwa wenyewe
 
Una sensory neural hearing loss au una conductive hearing loss...??

Ulishafanya kipimo cha Audiometry...??
 
Pole sana Bro,

Mungu ni mwema na kila mtu anakusudi lake katika ulimwengu huu.

Usikate tamaa!!
 
Una sensory neural hearing loss au una conductive hearing loss...??

Ulishafanya kipimo cha Audiometry...??
Ni sensor neural loss,

Ndio nimefanya hicho kipimo!
 
asante bro!

Sikwenda hospitali moja ninavyo vifaa nilivyopewa muhimbili hosptali,agakhan na vingine walikuja wataalamu toka marekani.

Mimi si mgonjwa bali ni mtu mwenye ulemavu wa kusikia nimepata ulrmavu huu nikiwa darasa la tatu mwaka 2005 hivyo si rahisi kusema sijikubali hapana! Najikubali sana na najiamini pia!

Ndio maana nipo pamoja nanyi tukipeana mawazo na ushauri hata tukiwa live sioni tabu wala haya kukuambia ongeza sauti mimi sisikii vizuri!
Nashukuru kwa ushauri wako mkuu mungu akuzidishie!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…