Tushangae na tujiulize sisi Watanzania

S V Surovikin

JF-Expert Member
Aug 8, 2015
13,615
32,711
Ndege yetu ilipokamatwa kule South Africa tuliona serikali ilivyofanya jitihada mpaka ndege yetu ikaachiwa, huku serikali ikijipiga kifua kwamba imemshinda mdai bila kulipa hata sent.

Serikali ilijisifu vilivyo kuwa ilipeleka watu wenye PhD zao ndio maana ilishinda kwa kishindo.

Wenye akili wengi walionya lakini walibezwa na kuitwa sio wazalendo! Sisi wananchi tulihitaji maelezo namna serikali ilivyoshinda hiyo kesi lakini tulifichwa, huku serikali ikijisifia tu na kumsifu rais.

Sasa nimeshangaa na kuduwaa jana baada ya ndege yetu nyingine kuzuiwa kuondoka kule Canada kwa kisa kilekile kwamba mkulima yuleyule tuliyemshinda kwa kishindo kule Afrika Kusini kashikilia ndege yetu nyingine kwa kesi ileile?

Je, serikali yetu inatuficha sisi wananchi wake kwa mambo ya msingi kama haya?
Kwanini basi wajisifie namna ile kama walijua wana mambo yao nyuma ya pazia? Kwa mtindo huu tutaweza kuiamini serikali?

Sisi kama wananchi tunahitaji maelezo ya ile kesi na namna serikali ilivyoshinda ili tujue adui yetu ni mkulima au ni serikali hii hii ya awamu ya 5.
 
Serikali mwanzo ilikua inapiga mayowe kua yule panya aliyekua akisumbua tayari tumedhibiti pasipo kuweka wazi ni mbinu gani waliyotumia kumdhibiti

Nyuma ya pazia kumbe panya aliyekua akisumbua walizibia shimo lake kwa kipande cha bumunda sasa ametoka serikali ijipange
 
Serikali mwanzo ilikua inapiga mayowe kua yule panya aliyekua akisumbua tayari tumedhibiti pasipo kuweka wazi ni mbinu gani waliyotumia kumdhibiti

Nyuma ya pazia kumbe panya aliyekua akisumbua walizibia shimo lake kwa kipande cha bumunda sasa ametoka serikali ijipange
Shimo la panya linazibwa kwa mkate
 
Haya yote ni mapungufu ya kukosa majasusi wa kiuchumi,tumechelewa ila ni muda Sasa wa kuanzisha taasisi ya majasusi wa kiuchumi.. tutafedheheshwa sana,Kama ni vita vya kiuchumi hatuna budi kusimama kiuchumi uchumi nasi..
 
Back
Top Bottom