Tusaidiane majibu hapa

W
Watu wanashabikia vyama lakini maslahi ya taifa ni muhimu sana. Katika tofauti tunazotaja kuwa zinasababisha chama cho chote kuchokwa na wananchi maslahi ya taifa yapaswa kuwa kigezo cha kupendwa au kuchokwa kwa chama cho chote. Mimi napendekeza mkuu wa kaya kama anavyosema yuko kwa ajuili ya watanzania wote, akae na viongozi wa vyama vyote, maslahi ya taifa yabainishwe na wote tufanye kazi ya kuwaletea wananchi maendeleo kwa kuzingatia maslahi ya taifa. Siamini kwenye utitiri wa vyama, vipunguzwe vibaki vine vyenye nguvu, vilivyoshindwa kupata viongozi katika ngazi za vitongoji, madiwani na wabunge wajiunge na vyama vilivyoimarika ili kuwa na nguvu ya kutosha kwa kila chama.
 
mkuu mimi sina uhakika sana na hiyo kauli yako ya kuwa CCM haijachokwa. Labda nikuulize unauamini mfumo wetu wa uchaguzi kuwa unayo democrasia na uhuru wa haki kutendeka? Nadhani jibu lake ndo sababu ya CCM kuendelea.
 
Ccm ilianguka vibaya sana na ushaidi nadhani upo ila basi tu watu wameichoka lakini kusimama kwenye mstari na kupiga kura kwa upinzani kwa 100% hakutoshi kuiondoa fisim pale ilipo, tukiacha siasa kuna mambo yanayochokwa na kuna mambo yasiyochokeka!
 
Mkuu,kunywa soda,the bill on me!umegonga mulemule!
Mirror Effect!safi sana!
Huo ndio ukweli mchungu CHADEMA wasiotaka kuukubali!
Hoja za kuruka ruka kama pimbi ni kupoteza muda, hukumbuki Msigwa aliwahi kusema atakayemuunga Mkono Lowasa akapimwe akili, je kauli hii mbona huiongelei unarukia mahakama na milioni kumi ? Ama kweli Nyani haoni Kundule.
Asante mkuu
 
Udhaifu wetu Umekuwa Nguvu Yetu!
Asante kwa Ufafanuzi!
 
Waliotuhumiwa kugawana milioni kumi kumi hivi karibuni ni kina nani?

Waliotuambia Mahakama ya Mafisadi imekosa watu ni kina nani?

Hawa watu hamuwakinai tu?
MKUU NAONA WATU WANAJARIBU KUKUTOA KWENYE HOJA HAWANA LOLOTE HAO AKINA NANIHI WAKO MADARAKANI KWA KUCHAGULIWA?REJEA ULE UZI"POGBA HUYU NI HASARA"
 
Lumumba mmechangamka mpaka raha haya hongereni mmeingiza siku
 
CCM iliwachosha sana watanzania ila hakukuwa na chaguo lingine.
Bora CCM iendelee kutawala milele kuliko kuchagua fisadi awe rais wa Tanzania.
Unamaanisha wagombea walikuwa wawili tu yaani fisadi na huyo unayeamini si fisadi? Tuna safari ndefu kama hawa ndo wapiga kura wetu!
 
CCM iliwachosha sana watanzania ila hakukuwa na chaguo lingine.
Bora CCM iendelee kutawala milele kuliko kuchagua fisadi awe rais wa Tanzania.
Buku 7 imekupofusha kabisa unajifanya ujui kinachoendelea nchini
 
Wewe akili imefubaa,inaleta malapulapu hapa?Endelea kuota ndoto za Tengeru!
 
Watu tunapenda miziki ya zamani kwa kuwa old is gold. Sijui unajua hilo. Unajua miziki ya 1970s and 1980s bado inapendwa sana kuliko hata baadhi ya nyimbo za sasa.
 
Aiseeee mie nakula ugali kuanzia mwanzo wa mwaka hadi mwisho na sichoki hivyo naona hizo arguments zako hazina mashiko japo kiukweli hata mie nimeichoka hiyo kijani
 
Salary slip, huwezi kulazimisha watu wakupende...ndio maisha yalivyo.
 
Ni wao hao wanaojenga mazingira magumu kwa vyama vya siasa shida ni katiba yenye elements za kikoloni
Ni kwel wao wamekua ni chanzo kwa kiasi fulani hv.. ivi unavyo ona [HASHTAG]#fisadi[/HASHTAG] anaweza kuongoza nchi hii!?
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…