mohoniajoseph1
Member
- Jul 23, 2018
- 46
- 66
Mhe. Esther Matiko (MB) amekuwa kiungo mzuri sana katika kuwasemea Askari Polisi na hasa askari wa Magereza kabla na baada ya kwenda gerezani Segerea. Baada kwenda Gerezani kuna mambo mengi aliyabaini tofauti na yale aliyokuwa nayo awali.
MAY 24, 2019 aliuliza maswali kwa Waziri Mkuu juu ya hali ya Polisi hawa, na hasa suala la Polisi kupungukiwa sare za jeshi ambapo ni jukumu la serikali kuwahudumia sare kama vile; Suruali, Shati, Sketi, Mikanda ya suruali, filimbi, mikanda ya filimbi, nembo za cheo, soksi, kofia, sweta, viatu, ambavyo majeshi haya hasa Askari Polisi na hili la Magereza wamekuwa wakijinunulia hizi sare kwa vitambaa vinavyopatikana pale kwa Premji, ambapo kuna baadhi ya askari wameamua kuchukua tenda za kushona kwa 70,000 kwa pair kwa gharama zao.
Lakini pia, hata viatu wengi wa Polisi hawa wananunua kwa fedha zao {50,000/=}kwa kuwa Serikali haijawapelekea sare za kazi kwa muda mrefu sana.
Swali hili halikujibiwa kwa undani wake mbele ya Bunge badala yake yalitoka majibu ya kawaida sana.
Ndani ya Kitengo cha Askari Magereza kuna tatizo lingine kubwa la kimfumo ukiachana na hili la sare ambalo karibia kila askari analisema.
Licha ya kwamba Askari Magereza, Askari wa Uhamiaji, Polisi wa ulinzi wa raia, na Askari wengine wote wapo chini ya Wizara moja, ambayo ni Wizara ya Mambo ya Ndani ya nchi lakini kuna utofauti mkubwa sana wa malipo ya mishahara yao pamoja na utofauti wa Elimu zao.
Askari Magereza ndio Askari wanaolipwa mishahara ya chini sana kuliko Askari wengine ndani ya Idara hii ya Usalama.
Bila kujali utofauti wa viwango vyao vya Elimu. Jeshi la Magereza linateseka sana kwa mshahara huu mdogo na hasa ikizingatiwa kuwa katika kipindi hiki hali ya maisha imepanda sana.
Iko hivi; Polisi wa Usalama wa raia, mwenye Elimu ya Shahada (Degree Level of Education) analipwa mshahara wa Tsh. 860,000/= kama BASIC SALARY.
Pia anapata 15% ya mshahara wake kama Posho ya ujuzi ambayo ni sawa na Tsh. 129,000/=. Hivyo pesa ya (Grand Total) anayopokea Askari wa Usalama wa raia ni Tsh. 989,000/=.
Tangu mwaka 2015 Polisi wa Magereza wa Elimu ya Shahada (Degree Level of Education) wamekuwa wakilipwa Tsh. 400,000/= tu kama BASIC SALARY Sawa na askari Magereza mwenye elimu ya Kidatu Cha Nne.
Ukiondoa makato na pengine kama Askari huyu amekopa Benki, kwa mwezi Askari wa Magereza anaweza kujikuta amepokea Tsh. 180,000/=.
Kiwango hicho apange Nyumba, nauli na matumizi mengine.
Mishahara ya askari wa Magereza haiendani na Elimu zao tofauti na Askari wa kada zingine licha ya kuwa wote wapo chini ya Wizara moja.
Madai ni mengi ambayo serikali ameayaacha na kuwa mzigo ambayo kwa nyakati tofauti Mhe Matiko amekuwa akayasemea ili serikali ishughulikie kama Fedha za likizo, kupandishwa madaraja, wanatumia Fedha zao kusafirisha mahabusu/ wafungwa, Fedha za kuhamishwa n.k
Je, kwanini Serikali imepuuza kilio hiki cha Askari wa Magereza?
Ni wakati sasa wa kuwasaidia askari hawa, ili kuiomba Serikali iwasikilize na kufanyia kazi vilio vyao kwani wote hawalali usiku na mchana katika kutekeleza majukumu yao ya msingi.
Tumsaidie Mhe. Esther Matiko katika hoja zake juu ya Jeshi la Polisi kwa kulifanya jambo hili kuwa lenye sura ya Kitaifa. Asiachiwe mtu mmoja, kwakuwa ndugu zetu ndio wanaoteseka.
MOHONIA JOSEPH