Turufu kubwa ya Serikali ya Tanzania katika Ukanda huu wa Afrika ya Mashariki ni Burundi na Uganda

Hata Sina kinyongo

Senior Member
May 16, 2020
118
280
Tanzania bado ni nchi itayoitawala Afrika Mashariki kwa miaka mingi ijayo. Kwanini;

Ieleweke, usalama na uhakika wa kuwa hapo alipo Rais Museveni bado ni uimara wa kiulinzi, kiintelijensia na kwa kutotaka kuungana kwa Serikali ya Tanzania na Rwanda ili kumuondoa Kaguta pale alipo japo Rwanda muda wote anatamani kuweka mapandikizi yake ktk utawala wa Rwanda.

Kuhusu Burundi Tanzania ni zaidi ya baba kwake! Bila msimamo wa Tanzania kuihusu Burundi leo ingeshabaki historia kwamba ulikuwepo utawala wa Nkurunzinza....

Muktadha wangu ni huu; Rwanda hana cha kuifanya, kuikomoa ama kuiumiza katika lolote serikali ya Tanzania kwa sababu atakayeathirika mno na uamuzi wowote hapo juu yeye ndiye hasa ataathirika zaidi.

Wenye jicho la kiintelijensia ndiwo pekee wataelewa kuhusu kipi nimeongelea.
 
Hapa sijakuelewa unamaanisha nini!
Kama ni hili swala la kifunga mipaka, hili ni kitokana na janga la dunia, korona, na hili halihusiani na nguvu za kijeshi.
 
Ukiwa na wateja kumi akipungua mteja mmoja lazima kipato chako kitapungua na kikipungua itaathiri bajeti yako na pia bajeti yako ikiatirika lazima wanaokutegemea wapate shida.

Sent using Jamii Forums mobile app
 
Mkuu ni bora uendelee hivyo hivyo kutokuwa na kinyongo maana hiyo Professor Kibudi anazidi kuichafua Diplomasia ya Bongo. Hayo ndio matatizo ya too much knowing.
 
Hakuna unachofahamu hata nikuuliza nini maana Ya Intelijensia sijui kama utapata majibu....Yaani Hapa East Africa Kenya ndo jicho la nchi zote sio hawa madikteita.
 
Ukiwa unajadiliana na Baba mkwe wako huko usikurupuke kuja huku kuleta theory ambazo hazina mashiko wala ha uelewe ki!!
 
Kwanza pole sana kwa kuwa na mawazo ya kizamani sana.
Tanzania hatuitawali east africa.
East africa ina nchi huru na zinazojitegemea. Hizo nchi si makoloni ya tanzania. So nchi hizo kufanya maamuzi binafsi kusionyeshe kuwa wanaiumiza tanzania..
Wanafanya maamuzi kwa ajili ya nchi zao wenyewe.
 
Weka wazi Basi ushahidi wako tuone kuwa kumbe sisi ndiyo mababa wa haya mataifa. Naona Kama post Ina mapungufu

Sent using Jamii Forums mobile app

Jiografia ya Tanzania inaibeba sana

Tanzania imeUngukwa na nchi takriban 8

Kenya,uganda,Rwanda,Burundi,DRC,Zambia,Malawi na msumbiji upande wa mashariki.ukiwa.na kilometa zaidi ya 1800 za ufukwe wa bahari ya hindi

Rwanda hata afanye vipi kupitisha.mzigo mombasa,kwake.ni hasara,inakula.zaidi ya kilometa 200

Uganda,mzee anaamini ni Tanzania tu kuwa anaweza kuingia hata usiku wa manane akatoka salama

Kenya kwa sasa wamezama tulikotoka kwenye ufisadi,bandari ya mombasa inabeba bidhaa za sudan ya kusini na uganda kidogo,ndio maana wanajitahidi sana kuimeza bandari ya dar,lakini wanajikuta wanaharibikiwa

Msumbiji ana uwezo wa kupitisha mzigo wake na zimbabwe kidog,malawi,zambia,DRC na Burundi hawana njia nyinggine zaidi ya Tanzania

Hii inafanya Tanzania tuonekane tuna nguvu,na akitokea Rais mwenye akili za kibeberu,atazisanbaratisha kiuchumi hizo nchi ndani ya mwezi mmoja tu,kama wanavyofanya urusi kwa ukraine,kufunga ghafla koki za bomba la gesi linalokwenda ulaya hasa italy,wakati watu wanaganda kwa kukosa nishati,ikabidi ukraine aache kiburi na kupiga magoti
 
Back
Top Bottom