Turudi kwenye misingi: Kama Taifa hatutaweza kuendelea (kupiga hatua) kwa kutegemea viongozi wa kuokoteza

Conwel Ngani

Senior Member
Sep 16, 2018
134
149
Nadhani wengi mtakubaliana na mimi kuwa viongozi wengi tulionao hasa wa kisiasa hawajalelewa au hawajaandaliwa kushika nafasi walizoshika, wengi wao wamefika mahali walipo kwa juhudi binafsi na kwa kujilea wenyewe. Kama Taifa lazima tukiri kuwa hili ni tatizo linalohitaji kupatiwa suluhu kama tunahitaji kusonga mbele. Ndio maana siku za leo utaona tuko katikati ya tatizo wanaotuongoza wanaanza kurushiana maneno, badala ya kushirikiana wamalize tatizo kwanza ndio kwanza wanaanza kutugawa wananchi kwa vitisho, maneno ya kejeli na kutuaminisha fulani ni mbaya na fulani ni mzuri.

Maadili ya uongozi ya namna hii tumeyatoa wapi? Ni wazi kuwa viongozi wetu wamekosa maadili/malezi na makuzi ya kiuongozi. Kipindi cha Tanu na badae CCM walikuwa na mfumo wa kufundisha wanachama wao wanaoandaliwa kushika nyazifa mbalimbali kitu ambacho siku za leo hakifanyiki mara kwa mara kwenye vyama vyetu. Mafunzo kama haya yanapaswa kuandaliwa mara kwa mara ni iwe ni sharti la lazima kwa viongozi na wale wanaotarajia kugombea nyazifa mbalimbali

Magufuli ataka makada wa vyama wapikwe Chuo cha Nyerere

Katibu Mkuu CHADEMA kuanza kutoa mafunzo kwa viongozi wote wa chama - JamiiForums

MAMA SAMIA AFUNGUA MAFUNZO YA VIONGOZI NA WATENDAJI WA CCM MKOA WA KASKAZINI UNGUJA

Mafunzo haya yawe ya muda mfupi (Short courses) na ya mara kwa mara na za ngazi tofauti.

Pia, vyama vijitahidi kubuni program za malezi ambazo zitasaidia kupima kama watu wao wamefuzu au wamefikia kiwango cha kuaminika kupewa nafasi wanazoziomba au wanazozigombea. Na hapa ndipo vyama vya upinzani vilibugi step, viliamini watu ambao hawakuwa na mikono yao katika malezi/ makuzi yao kwa lugha nyingine waliokoteza (Kwasasa CCM inafanya kama wao ila nadhani ina mkakati mkali sana mbeleni, ni kama mwizi wa kuku anaporusha punje za mchele ili kuku wasogee kwenye anga lake). Hili likifanyika inaweza kusaidia kupunguza hisia za wabunge wa upinzani kununuliwa na chama tawala.

Bahati mbaya kama Taifa tumepuuza sana elimu ya namna hii, lakini tukae tukijua kuwa elimu yoyote haijalishi ni ndogo kiasi gani ina nguvu/uwezo wa kubadirisha fikra au mtazamo wa mtu juu ya jambo fulani, ni silaha kubwa ya kuondoa ujinga.
 
Nanukuu "Elimu yoyote haijalishi ni ndogo kiasi gani ina nguvu/uwezo wa kubadirisha fikra au mtazamo wa mtu juu ya jambo fulani, ni silaha kubwa ya kuondoa ujinga" Hapo upo sahihi mkuu
 
Awamu ya Tano hata ukiwa kama Dr shika kama unawatukana Chadema 24/7 lazima upewe shavu....Kabakia :cool: kulamba shavu tu la UDC maana ma_Super friend wake wote wamelamba uDC You know ha ha ha ha.
 
Awamu ya Tano hata ukiwa kama Dr shika kama unawatukana Chadema 24/7 lazima upewe shavu....Kabakia :cool: kulamba shavu tu la UDC maana ma_Super friend wake wote wamelamba uDC You know ha ha ha ha.
Kama hiki ndio kigezo cha kupata udc nadhani kama taifa tutakuwa tumepotea sana, ila sidhani kama tumefika hapo
 
Kama hiki ndio kigezo cha kupata udc nadhani kama taifa tutakuwa tumepotea sana, ila sidhani kama tumefika hapo
Ndio Kigezo namba moja cha kupata uDC,si umeona kina Jenny Murro walivyojitoa ufahama kwa sasa kashatulia,ona Musiba na yeye anavyopagawa na mapumba kibao ili mradi na yeye ateuliwe.
 
ccm ilikuwa zamani mkuu sio ya sasa. Kwa sasa ni juhudi zako kupongeza,kujipendekeza, kutukana na kusuta wapinzani wallah unaukwaa japo u-DC.
 
Back
Top Bottom