Nanren
JF-Expert Member
- May 11, 2009
- 2,910
- 3,018
Wanajukwaa,
Kwa maoni yangu ni kwamba sheria zilizopo kuhusu dawa za kulevya zinapoteza muelekeo wa mapambano dhidi ya dawa hizo.
Kitendo cha kuiweka mirungi na bangi katika level moja na Cocaine na Heroin, kinapelekea nguvu kubwa kuelekezwa kwenye mashamba ya bangi na mirungi wakati tungeweza kukomaa kwanza na "unga" (Cocaine na Heroin). Ni vigumu sana kupambana na bangi ambayo kiasili inalimwa kwa wingi hapa hapa nchini. Tungeanza kwanza na Heroin na cocaine ambazo huletwa kutoka nje ya nchi na ndizo zenye madhara zaidi kwa vijana, then bangi na Mirungi itungiwe sheria zake na kushughulikiwa kitofauti kidogo. Hii hata hivyo haimaanishi kwamba bangi na mirungi ndio iachwe tu, hapana. Ila isipewe kipa umbele kama ilivyo kwa aina nyingine ambazo ni hatari zaidi.
Karibuni kwa maoni.