Tupunguzeni kunung'unika!, Tujilazimishe katika Ubunifu na Uvumbuzi.

Azizi Mussa

JF-Expert Member
May 9, 2012
9,172
7,429
Mtu mwenye tabia ya kunung'unika kila wakati hana sifa ya uongozi!,
Mtu mwenye tabia ya kulalamika kila wakati hana sifa ya uongozi!,
Mtu mwenye Tabia ya kukosoa tu bila kubuni mbinu mbadala ya kushughulikia alichokikosoa hana sifa za uongozi!.

Nakumbuka kuna msemo unasema usiwe "Jipu la kwapa" mtu akipandisha mkono linauma! na akishusha linauma na hata akilala linauma vile vile!.

Mara nyingi miongoni mwetu tumekuwa tunamlalamikia rais Kikwete, akicheka kwamba ni kiongozi gani mwanaume kazi kucheka cheka tu!.Akiamua kuwa mkali; tunasema kiongozi gani dikteta kiasi hiki!, akilalamika, tunasema kiongozi gani katika level ya urais kazi kulalamikalalamika tu! sasa leo tumeona maonesho ya majeshi yetu ambayo inaonekana wazi kwamba yamejiimarisha sana: Tunalalamika tena kwamba Rais Kikwete anataka kumtisha nani!? badala ya kumpongeza kwa kujenga jeshi la kisasa kabisa kwa ajili ya ulinzi wa nchi yetu.

Ndugu zangu, Kwa mwendo huu tusipokuwa makini, tutadhani kwamba ndio eti tunafanya upinzani kumbe tunaweka mazingira ya watanzania wenzetu kushuku uzalendo wetu tena wakiwa na sababu za msingi kabisa kufanya hivyo. Hivi wewe ambae unalalamika kwa nchi yetu kufanikiwa kujenga jeshi imara na la kisasa, lenye askari weledi na wazalendo; halafu unajinasibisha na upinzani, unafikiri sawa sawa?Hivi hauoni unachafua sura na muonekano wa upinzani pamoja na nadharia nzima ya upinzani nchini?

Ndugu zangu, hivi hatuoni kwamba ipo haja ya kukubaliana katika mambo ya msingi na hata kupongezana ili hata tutakapokosoa mambo ya msingi iwe na mantiki kwa kuwa tukiwa watu wa kunung'unikia kila kitu; hata siku tunapokosoa jambo la maana tunaonekana ndio wale wale tu!?Mimi najiuliza tumeingiliwa na nini!?

Hivi kuna haja gani ya viongozi wa vyama vya upinzani kutohudhuria shughuli na sherehe za kitaifa kana kwamba sherehe hizo za kitaifa ni sherehe za chama cha siasa! hivi hii inasaidia nini na kwa nani?Hivi hatuoni kwa kufanya hivyo sasa ndio tunatoa picha kwamba chama hicho kinachohudhuria na kushiriki shughuli hizo; ndicho chenye uchungu na nchi hii! just simple tu! Hebu tufikirieni ndugu zangu! masuala ya kitaifa ni yetu wazalendo wote.

Nakumbuka hata shule za kata zilipoanzishwa, wengi wetu tuliziponda sana lakini hatupendekezi nini kifanyike badala yake.Mtu tu! anasema shule za kata hazina maana kwa sababu hazina madawati halafu anapendekeza bora zisingekuwepo (kisa kaziweka mwingine), badala ya kupendekeza kwamba akichaguliwa yeye atazifanya ziwe mpaka na internet! hivi kweli lengo letu ni maendeleo ya nchi hii? mwenye nia njema na nchi hii ni yule mbunifu na si yule wa kulalamika na kulaumu kila kitu tu.Hivi ni nani akipewa kazi ya kulaumu tu anashindwa! lakini inaweza kutufaa nini basi kazi hiyo?


Bungeni tumeona; eti mtu anasema anataka serikali mbili halafu kutetea hoja yake anatoa udhaifu wa serikali tatu, na mwingine anasema anataka serikali tatu kutetea hoja yake anatoa udhaifu wa serikali mbili.Masikini wala hata hatufikirii kwamba udhaifu wa serikali mbili sio sababu tosha ya kuwa na serikali tatu na kinyume chake.

Ndugu zangu; Tunasumbuliwa na tatizo kubwa la kuwa na tabia ya kunung'unika wakati wote na kukosa ubunifu na uvumbuzi wa namna tunavyoweza kushughulikia matatizo sugu yanayotukabili. Hata hivyo jamii hujengwa katika mrengo fulani kutokana na jitihada na mitizamo za wajenzi; hivyo ni lazima tuwe na "institutional framework" (chama) kinachoweza kutujenga kuwa viongozi wabunifu na wavumbuzi badala ya kuendelea kuwa watu wa kunung'unika wakati wote.

Niwapongeze wote waliofanikisha shughuli za maadhimisho ya muungano na naudumu muungano wetu!.
 
Na kama kuna alietaka kuvunja muungano, ajue makomandoo wapo na wanapasua matofali kwa vichwa! tehe! kuna mzee mmoja pale jukwaaa kuu alikuwa anakuna kichwa kweli.
 
Tatizo hilo liko kwa wote sio chama tawala wala upinzani, ukijaribu kuangalia wazo hata liwe zuri vipi linaangaliwa nani kalitoa kama ni mpinzani chama tawala atapinga na kinyume chake. Kibaya zaidi wote wanafanya kwa kukomoana huku kila upande kujifanya ni mshindi hata kwa mambo ya kipuuzi.
Kwa mfano sherehe za muungano leo zimeongozwa na chama tawala kama kuwatambishia wapinzani huku wapinzani wakibeza kwamba si lolote si chochote. Kwa ujumla mafanikio ya jeshi letu hayakutakiwa yawe kama ni mafanikio ya chama kilochoko madarakani bali ni sifa ya wananchi wote walipa kodi lakini ukiangalia ni kama walioko madarakani wanaona kama ni silaha yao dhidi ya wapinzani. Hii ndio inapelekea wapinzani kubeza kwani wanaona jeshi linatumika kama kizingiti dhidi yao.
 
Hata ndani ya bunge maalumu nilimsikia mhe Mkosamali akiwakosoa wale wenye tabia ya kupinga kila kitu hata mambo ya msingi. Baadhi ya WaTZ wana akili kama ya fisi.....
 
mkuu tindo naomba nikuulize mashwali kadhaa unijibu objectively.
1.Ni kwa vipi ubora wa jeshi letu unaweza kuwa tatizo kwa upinzani? au linatakiwa kuwa imara lakini tusijue?
2.Ni sahihi kwa ccm kushiriki kikamilifu kwenye mambo ya kitaifa kwa sababu yoyote ile!

3.Ni sahihi kwa mtu yeyote kutoshiriki mambo ya kitaifa kwa makusudi kwa hoja ya kwamba ndio uzalendo!
4.Wote wanaohudhuria kwenye mambo ya kitaifa wanakua wamealikwa?
 
Last edited by a moderator:
Jamani, tujiulizeni kuwa ni kwa vipi tunaweza kuzitumia fursa zilizotuzungunga kuboresha maisha na ustawi wa jamii kwa ujumla, au ni kwa vipi unaweza kupunguza changamoto zilizopo kwenye eneo unaloishi.
 
, tujiulizeni kuwa ni kwa vipi tunaweza kuzitumia fursa zilizotuzungunga kuboresha maisha na ustawi wa jamii kwa ujumla, au ni kwa vipi unaweza kupunguza changamoto zilizopo kwenye eneo unaloishi.
Mkuu nadhani wewe huijui Tanzania. Hizo fursa ambazo unasema, zinaweza kuwepo lakini serikali ikazivuruga. Nakupa mfano, hapa musoma kulikuwa na wavuvi ambao huuza samaki zao sehemu ambayo wanajua wateja watafika na wako radhi kutoa ushuru. Serikali hii hii, juzi wamefukuzwa pale eti si sehemu stahiki waende sokoni. Je, huko sokoni kuna market ya biashara yao?Je? hapo fursa zao zimeharibika au hazijaaribika? Watu wanapolalamika, lazima kuna kitu. Jirani hawezi kukusingizia kuwa wewe ni mchawi, kama hajawahi kukuona. Ni bora unyamaze kimya na hizo fursa zao unazozisema
 
Mkuu nadhani wewe huijui Tanzania. Hizo fursa ambazo unasema, zinaweza kuwepo lakini serikali ikazivuruga. Nakupa mfano, hapa musoma kulikuwa na wavuvi ambao huuza samaki zao sehemu ambayo wanajua wateja watafika na wako radhi kutoa ushuru. Serikali hii hii, juzi wamefukuzwa pale eti si sehemu stahiki waende sokoni. Je, huko sokoni kuna market ya biashara yao?Je? hapo fursa zao zimeharibika au hazijaaribika? Watu wanapolalamika, lazima kuna kitu. Jirani hawezi kukusingizia kuwa wewe ni mchawi, kama hajawahi kukuona. Ni bora unyamaze kimya na hizo fursa zao unazozisema
Pole ni Kwa mkasa uliowakumba ila sasa hata hapa jukwaani au huko huko kusoma wadau walitakiwa wapange hoja zao vizuri watetee hiyo ishu kama sana hoja ya msingi wangesikilizwa lakini Kwa kulalamika tu hamuwezi kuwasaidia maana hata hao waliowatoa lazima wana sababu Fulani ya kufanya hivyo
 
Back
Top Bottom