Tupike wali samaki

Leejay49

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2023
Posts
19,295
Reaction score
60,915
Hi guys,.hope mko poa

Tunavyoendelea kumwomba Mungu kuelekea kesho D9 basi tusisahau kula..... Haya tuanze

Ukishaweka mchele wako kwenye rice cooker au vyovyote vile utakavyoupika,. Pembeni tutaanza kupika samaki,. Kwenye sufuria yako utaanza kuweka mafuta kidogo,. vitunguu hoho na carrot kama nlivyofanya Mimi hapo



Ukishavikaanga vikiiva vizuri utaweka nyanya na chumvi kiasi then utaendelea kukaanga
Nyanya zikishaiva utaweka tomato paste kiasi utaendelea kupika dakika chache then utamweka samaki wako ambae ulishamtengeneza vizuri
Taratibu utamsambazia viungo,. Akishashikana na viungo vizuri utaongezea nazo yako ambayo ulishaichuja vizuri,.. utakoroga taratibu taratibu ili Nazi isijikate
Utaacha Kwa mda kidogo na mchuzi wako utakua tayari kama hivi
Hapo sasa unaweza ukaonja kama nilivyofanya Mimi hapo,. Na samaki wangu alikuwa sooooo tasty

Unaweza ukaserve na chochote,. Wali ugali au ndizi ila Mimi nilisave na wali wangu ambao mpaka namaliza kupika samaki ulikua umekwisha iva

You can try it,. Na uenjoy mwenywe au na familia yako😍
 
Na huyo muhuni ni wewe😆😆

Thanks 😍
Sasa huu msosi utupikie mwingi ili ubakie wa asubuhi tukipige kiporo na mchuzi wa samaki chini kuweka na ukoko tuchangange na ndondo (harage).

Hapo Nina uhakika hatutakuwa na muda wa kurudi home kustua tumbo hiyo kesho. Ni mwendo wa maandamano hadi waseme basi inatosha.
 
Maagizo yameeleweka mwashimiwa
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…