Tupike ndizi

Leejay49

JF-Expert Member
Joined
Feb 10, 2023
Posts
19,711
Reaction score
62,651
Hi guys, habari za siku nyingi??
Bila kupoteza mda tupike ndizi nyama pamoja…

Kwenye sufuria yako ya kupikia utaweka mafuta kidogo sana, yakipata moto utaweka kitunguu hoho na karoti

Utakaanga vikilainika utaweka ndizi zako ambazo ulishamenya na kuzikwangua vizuri

Utazikaanga kwa dakika mbili au tatu halafu utaweka nyama yako ambayo ulishaichemsha na kitunguu saumu tangawizi na chumvi,. Then utaongea chumvi kidogo

Utakaanga tena kidogo then utaweka supu ya nyama pamoja na tui la nazi vikombe viwili,. Then utafunika uache zipikike kwa dakika tano hadi kumi

Then utafunua utageuza kwa kuzungusha sufuria ili ndizi zisijikate kate,. Then utaziacha zipikike zikiwa wazi kwa dakika 1 au mbili ,. Na ndizi zako zitakua tayari zimeiva

Utaserve and ready to chop

Hope you enjoyed 😍😋😘 min -me
 

Similar Discussions

Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…