John Achila Mukumwa
Senior Member
- Jan 4, 2024
- 111
- 214
Tupige Vita Roho ya Yezebeli
Yezebeli ni Nani
Yezebeli alikuwa ni mwanamke mwenye asili ya nchi ya Lebanoni, mahali pajulikanapo kama Sidoni (1Wafalme 16:31), karibu sana na mji wa Tarshishi, ule mji ambao Nabii Yona alienda kuhubiri (akaacha kwenda mji wa Ninawi alioagizwa na Mungu). Alikuwa ni binti wa kifalme, hivyo alitokea katika familia tajiri.
Mwanamke huyu hakuwa Muisraeli, ila aliolewa na Mfalme wa Israeli, aliyeitwa Ahabu. Hivyo, ilimbidi ahame kutoka katika taifa lake la Lebanon na kuhamia Israeli, katika mji wa Samaria, akiwa na miungu yake, na tamaduni zake.
Mfalme wa Israeli akamfanya kuwa Malkia, jambo ambalo Mungu alishalikataza kwa kinywa cha mtumishi wake Musa, kuwa wana wa Israeli wasioe wanawake wa kimataifa, kwa sababu watawageuza mioyo waabudu miungu mingine (1Wafalme 11:2).
Lakini Mfalme Ahabu alifumba macho yake asione hilo, na badala yake akamwoa Yezebeli.
Yezebeli, kwa kuwa si Muisraeli, bali alitoka taifa lingine lenye miungu mingine, aliingia Israeli na miungu yake na makuhani wake.
Hapo ndipo mambo yalipoanza kuwaharibikia wana wa Israeli. Shida ikawa kubwa hadi Mungu kumnyanyua Eliya Nabii.
Tabia za Malkia Yezebeli
Malkia Yezebeli alikuwa na roho aina tatu ambazo zililiharibu Taifa la Israeli, na zinazofanya uharibifu hadi leo, ndani na nje ya kanisa.
1. Ukahaba
Hii ni sifa ya kwanza ya Malkia Yezebeli. Biblia inasema alikuwa ni mzinzi, kwani ndiye mwanamke pekee aliyeonekana katika biblia amepaka wanja usoni na kujipamba kichwa. Yote hayo yalikuwa ni kwa lengo la kuvutia ukahaba. Hakuna mwanamke mwingine ye yote katika biblia anayetajwa kufanya mambo hayo.
Hebu tuangalie katika kitabu cha 2Wafalme 9:30: “Hata Mfalme Yehu alipofika Yezreeli, Yezebeli akapata habari; akatia wanja machoni mwake, akapamba kichwa chake, akachungulia dirishani”.
Yezebeli akamwona Yehu anakuja. Kwa tabia yake ya uzinzi, akaanza kujipaka wanja machoni, na kupamba kichwa ili amlaghai Yehu, apate kulala naye. Na wala hata hakuwa na uchungu kwa kifo cha mwanae, yeye anawaza uzinzi tu.
Roho hii inatenda kazi hadi leo. Leo hii, baadhi ya watu wanaenda misibani wamejipodoa. Mahali pa kwenda kutafakari mwisho wa safari ya mtu ulimwenguni, wengine wanaenda wamejipodoa kwa lengo la kuvutia ukahaba kama alivyofanya Yezebeli, katika msiba wa mwanae. Ni jambo la kusikitisha.
Roho hii imeingia hadi makanisani. Utaona baadhi ya wanawake na mabinti sehemu za ibada, wanaingia kwa mionekano kama ya Yezebeli, bila aibu wala hofu. Viungo vyao vipo wazi, nguo walizovaa ni za nusu tupu, nyuso zimejaa rangi, na vichwa vimepambwa kama Yezebeli, na hawaambiwi chochote, na wala wenyewe hawasikii dhamira yo yote ikiwahukumu mioyoni mwao. Hao, wanafanya hivyo pasipo kujua kuwa hiyo ni roho ya Yezebeli, inaishi na kutenda kazi, kama ilivyokuwa enzi za Mfalme Ahabu, mume wa Yezebeli.
Kupamba uso ndani na nje ya kanisa ni roho ya Yezebeli, ya ukahaba. Tusidanganywe na shetani kuwa ni urembo tu. Hakuna urembo ndani ya mavazi ya kikahaba. Hiyo ni sawa na kuvaa sare ya askari na ukasema ni urembo tu. Ni mavazi mawili yenye malengo tofauti.
Roho ya Yezebeli ni roho kama roho nyingine. Roho hiyo tayari imeingia hadi kwa baadhi ya wanaume. Kwa mfano, kwa wale wanaume wanaosuka nywele, na kupaka wanja usoni, na kuvaa nguo nusu tupu, na kujichora mwili wake. Roho ya Yezebeli inatenda kazi ndani yao, kwani roho ni ile ile.
2. Uchawi
Pamoja na Yezebeli kuwa kahaba, biblia inasema kuwa, pia alikuwa ni mchawi. Uchawi wa Yezebeli ulianzia nchini kwake alikotoka, kutokana na aina ya miungu aliyokuwa anaiabudu.
Alikuwa anamuabudu “mungu baali" ambaye kwa asili, makuhani wote wa baali walikuwa ni wachawi, na Yezebeli ndiye aliyekuwa mkuu wao.
Kitabu cha 2Wafalme 9:22, kinasena: “Ikawa, Yoramu alipomwona Yehu, akasema, Je! Ni amani, Yehu? Akajibu, Amani gani, maadamu uzinzi wa mama yako Yezebeli na uchawi wake ni mwingi". Mbali na uchawi wa Yezebeli wa kuloga, pia alikuwa ni mkaidi.
3. Nabii wa uwongo
Kitabu cha Ufunuo 2:20 kinasema: “Lakini nina neno juu yako, ya kwamba wamridhia yule nwanamke Yezebeli, yeye ajiitaye nabii na kuwafundisha watumishi wangu na kuwapoteza, ili wazini na kula vitu vilivyotolewa sadaka kwa sanamu”.
Roho ya Yezebeli inawafundisha watu kuzini. Inawafundishaje? Inawafundisha kwa injili kwamba “Mungu haangalii mwili, bali anaangalia roho”. Injili hii, inawafanya watu wavae watakavyo, ili lile neno Bwana Yesu alilolisema kuwa “amtazamaye mwanamke kwa kumtamani amekwisha kuzini naye moyoni mwake” (Mathayo 5:28), litimie juu yao, kupitia yale mavazi ya kikahaba wavaayo.
Ni muhimu kufahamu kuwa mwanamke akivaa mavazi ya kikahaba kama Yezebeli, halafu mwanamume akamtamani, tayari amekwishazini naye, hata kama hajamshika mkono. Mwanamke na mwanamume, wote wamezini, yaani hata kama mwanamke hajui kama ametamaniwa kwa mavazi aliyovaa, lakini tayari amezini.
Kwa hiyo, tujiulize, mwanamke anapotembea mtaani amevaa nguo kama za nusu uchi, anazini na wanaume wangapi moyoni?
Tunaona hii roho ya Yezebeli ipo pia makanisani na kwingineko. Ipo hata kwa baadhi ya wanaotambulika kama watumishi wa Mungu. Hii ni roho ya unabii wa uongo, inayowafundisha watu uzinzi kwa kujua na kutokujua. Hivyo, tujihadhari na injili hiyo ya adui, isemayo “Mungu anaangalia roho na haangalii mwili”. Ulinde mwili wako, usiwe chanzo cha kuipoteza roho yako moja kwa moja.
Roho ya Yezebeli
Kutokana na tabia ya Malkia Yezebeli, roho ya Yezebeli ni zile roho zenye tabia za uzinzi, usherati, uchawi, na za nabii wa uwongo. Inaweza pia kuwa na moja kati ya hizo tabia tatu zilizotajwa hapo awali. Tabia ya roho ya Yezebeli hushindana na Roho ya kweli ya Mungu.
Ndiyo maana Malkia Yezebeli katika uzinzi wake, uchawi wake na unabii wake wa uongo, hakuwahi kamwe kupatana na Nabii Eliya, wala kujinyenyekeza kwake. Badala yake, Yezebeli baada ya kusikia ishara Eliya aliyoifanya ya kushusha moto na kisha kuwaua manabii wake (wa baali) 450, aliapa kulipa kisasi kwa Eliya, na wala hakumuogopa hata Mungu. Ni roho ya kiburi. Roho ya kiburi haina woga.
Roho hii ya Yezebeli ikishakita mizizi ndani ya mtu, inamfanya kuwa na kiburi, na mkatili, hususan katika mtumishi wa kweli wa Mungu, na inamfanya mtu kuichukia njia ya kweli na watumishi wa Mungu wa kweli.
Roho ya Yezebeli ni zile roho zenye tabia za uzinzi, usherati, uchawi, na za nabii wa uwongo.
Leo hii, tunaona "Yezebeli" wako wengi kwenye jamii, kutokana na tabia zinazofanana na za Malkia Yezebeli.
Hizi ni siku za mwisho na Bwana Yesu yuko karibu kurudi. Hivyo, ni muhimu kuamua kujivua roho ya Uyazebeli, na kuvaa Bwana Yesu, kama kitabu cha Warumi 13:14 kisemavyo: “Bali mvaeni Bwana Yesu, wala msiuangalie mwili, hata kuwasha tamaa zake”.