Tupende na Kujali NYETI zetu.

Page 94

JF-Expert Member
Oct 22, 2015
5,205
15,162
Heshima kwenu Wakuu.

Nyeti zetu ni moja ya viungo muhimu sana katika miili yetu. Ndizo hututambulisha kwa jinsia. Pamoja na umuhimu huo, watu wamekuwa hawazijali na kuzitunza ipasavyo maeneo hayo kutokana na ukweli kuwa yamejificha humo ndani.

Nami leo nataka nitoe wito kwa WanaJF wote na jamii kwa Ujumla katika swala zima la kuzitunza na kuthamini maeneo tajwa. Wengi wetu tumekuwa tukiziacha tu na kuzikumbuka walau pale inapohitaji kufanya kazi.

Unakuta mtu ananunua nguo yenye thamani ya Tsh 500,000 (hasa wanawake) lakini nguo za ndani ananunua za Mtumba za Tsh 2,000 hadi 3000. Yaani juu kavaa nadhifu kabisa lakini kunako nguo ya ndani inatepeta. Natoa rai tununuo nguo za ndani mpya kabisa ili kuepuka madhara yaletwayo na nguo hizo za mtumba. Natambua kabisa kuna wakati zilipigwa marufuku lakini ukweli ni kwamba bado zinauzwa sana tu masokoni na kwingineko.

Pili, unakuta mtu ana nguo nyingi mno karibia kabati mbili au tatu lakini nguo za ndani ni mbili au tatu tu. Yaani unakuta mtu anapiga nguo moja wiki nzima, yaani inavaliwa daily mpaka baada ya siku saba. Duuh, inakuwa chafu kulikotukuka. Yaani hata chawa hawawezi kusogelea maana imepitiliza kabisa. Na wale waliopo kwenye jiji la BASHITE, na joto lile lote, Duuh!. Sijui inakuwa katika hali gani.
Tununue nguo nyingi hata dozen ili upate muda wa kuvaa moja kwa siku au hata mbili kwa siku moja. Hii itaacha nanilii katika hali ya usafi mororo kabisa. Siyo vema kujipiga manukato ili kukata harufu za uchafu wa nguo zako za ndani. Haipendezi na badala yake italeta harufu nyingine mbaya zaidi. Kuna wengine wana moja tu ya kuvaa siku anaenda kwenye gemu yaani hiyo ni spesheli kwa siku ya huduma. Baada ya hapo akifika anaivua na kuitunza mpaka siku nyingine tena.

Pia tupende kuzisafisha kwa kuondoa nywele katika maeneo yanayoizunguka huko. Natambua kuwa hizo vinyweleo au nywele yana mzuka wake lakini haipendezi ikiachwa na kuwa kama msitu wa Koromije. Mtu anajipiga makeup nyingi usoni lakini huku kwenye papuchi yake imepauka kama imeangukiwa na udongo wa Mgoti GGM. Papuchi unakuta imezungukwa na nywele utadhani inavuta weed kama marasta fari. Tupunguze na kubakiza kiasi chake kama vile zinakua kwa mbali.

Pia wale wasiopenda kuvaa nguo za ndani hamzitendei haki sehemu hizo. Imekuwa ni kama fasheni kwa baadhi ya wanawake (na baadhi ya wanaume) kutopenda kuvaa nguo za ndani, sijajua kuna raha gani katika hili. Natambua kuna joto sana lakini hiyo haihalalishi kutokuvaa. Kutovaa nguo ya ndani ina madhara yake. Moja ni kukomaza mbeneki (jiongeze), yaani inakuwa ngumu kama pembe ya faru John kutokana na misuguano ya nguo ngumu haswa suruali za kubana za jeans. Wanawake nawashauri muepuke hili. Hasa Miss Na uchukue hili maana ulishapuyanga mara kibao humu kuwa huvai nguo za ndani.

Katika hili pia tuangalie na size za kuvaa. Usipende nguo za kubana sana wala zenye kupwaya sana. Chagua ya size tu ili utoe nafasi kwa nyeti zako kuhema na kuendelea vizuri. Hii ni muhimu sana.

Tujitahidi sana kupenda na kujali nyeti zetu kama tunavyojali muonekano wetu wa sura na mavazi yetu ya kila siku.

Nawasilisha.
 
Asante mkuu! Ebu nianze kununua makufuli ya buku teni!!!
Me namuiga gigy money!!! No kyupi... Mwendo wa kupunga upepo
Hahahaa, alafu una kesi ya kujibu Mkuu.

Nunua hata ya laki Mkuu. Patunze hapo maeneo maana yenyewe ndo yanakupa ulaji. Hahahaa
 
Back
Top Bottom