Uchaguzi 2020 Tupeane mikakati ya mwisho ya kuifuta CCM

Huijui CCM wewe, kaa kimyaa.
 
Kila siku nawaambia Tundu Lissu hawezi kuja kuwa Raisi wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania, sio 2020 tu bali kamwe(NEVER). Kwa anayejua system ya Tanzania inafanyaje kazi peke yake ndio atanielewa. Kwa wengine mliojaa kelele za kijipa matumaini za "NI YEYE", hamuwezi kunielewa. Ila nina uhakika hata Lissu mwenyewe na Mbowe wanajua. Tanzania ni zaidi ya mnavyoijua na kuijadili mitandaoni. Mpaka tarehe 30 mwezi huu ndo mtaelewa ninachomaanisha hapa.
 
Umesahau kututaja tulio maliza vyuo miaka 4 sasa ajira hakuna saizi tunaoneka wasomi ni wapumbavu flani ,kura yangu ni Lisu
 
Kinachosikitisha lakini ni ukweli, NEC na CCM wamejipanga sana kudhurumu uchaguzi na Magufuli atatangazwa mshindi.

Kamanda usikate tamaa mapema... Hata ikipita wiki baada ya matokeo ya uchaguzi... Wengi wapo tayari kuingia barabarani kudai haki sehemu mbalimbali nchini... Nguvu ya umma itaonekana na haitoweza kuzuiwa..

Amin
 
2015 nilifanya ujinga ambao umenitesa kwa miaka 5 tena nirudie kosa ? Never ever
Makosa ya 2015 watanzania wengi tunajutia. Lakini sio kosa letu, alijivisha vazi la malaika kwa nje, wakati ni shetani kwa ndani. Alijifanya malaika wa nuru hivyo ilitakiwa macho ya rohoni kumuona. Gwajima na watumishi wengi wa Mungu waliona lakini....
 
Tumkatae tuwaambie na ndugu zetu tumkatae ametutesa sana nafsi zetu
 
Kinachosikitisha lakini ni ukweli, NEC na CCM wamejipanga sana kudhurumu uchaguzi na Magufuli atatangazwa mshindi.
Kutangazwa atatangazwa kama jamaa wa Malawi....ila guarantee ya kuongoza itategemea reaction ya watanzania...CDM...vyombo vya kimataifa nk....

Na hali iliyopo hata system inaweza kumbetray....CCM kapandikiza chuki sana na hakuwaheshimu wazee ambao wengi ni wazee wa system...kumbuka kauli yake kuwa waache kiherehere.....

Pia angalia support waliyompa katika kampeni...refer maneno ya mama Maria Nyerere....

Magu ana wakati mgumu sana
 
1.Nenda kapige kura,

2.Jitoe kulinda kura au wawezeshe Mawakala

3.Shinikiza mshindi atangazwe,

Tutakuwa tumeifuta Ccm.
 
1. Tushikamane sote kuthibiti wizi wa kura vituoni na udanganyifu unaofanywa na wasimamizi wanaonunuliwa na ccm
2.Tusaidiane kuvielimisha vyombao vya dola kuwa watwndaji wake ni waajiriwa wa serikali, hivyo hata kikingia madarakani chama kingine ajira zao bado zitakuwa palepale
3.Tuwaelimishe wataz wote kujitokeza kumpigia kura mgombea wa upinzani mwenye maono mbadala wa ccm
4.Tuzidishe sala na maombi ili Mwenyezi Mungu awanyongonyeze wote waliopanga njama na hila za kujipatia uongozi isivyo halali
 
Wahutu wa Mpanda na Tabora wamtosa Magufuli Huu ulikuwa mtaji mkubwa wa CCM huko mishamo.

Lissu ni Ushindi mkubwa ambao haijawahi kuonekana
 
Hahahaha! Jamani CCM siyo TLP au NCCR mageuzi ya mbatia, CCM Ni mfumo na umejisimika kwa mikakati thabiti,

Tatizo nyie wapinzani hamjitambui, mnakubalije kuingia kwenye uchaguzi kwa tume mnayoamini Ni ya CCM?

Mimi upinzani naupenda ila approach zenu hazifai na hazina madhara yoyote kwa CCM.

Hata hivyo tusipepese macho, Lissu hawezi na Hana uwezo wa kuwa Rais wa JMT.
 
Mkakati mkuu ni kulinda kura zetu.

Sana sana kiti cha Urais.
Huko mita 200 kutoka kituoni,wakala wa chama chako ametia sahihi ya kukubali matokeo.
Unacholinda ni nini wakati wewe huoni kilicho mezani?
Kuna haja gani ya kuwa na wakala?
 
CCM itaendelea kuwepo hapa mpaka TADEA watakapokuwa chama kikuu cha upinzani..sasa hesabu itoke Chadema,ACT,NCCR,TLP,UDP,CHAUMA.......TADEA...Safari ni ndefu Makamanda hii syndicate ishakuwa ngumu kutafuta rudini ngome mkajipange.


October 28th kura zote za ndio ni kwa JPM
JPM ANATOSHA
CCM KWA MAENDELEO YA TANZANIA
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…