Tupeane dondoo kuhusu online business - Sehemu ya kwanza

Mr. Purpose

JF-Expert Member
Nov 12, 2016
1,063
2,000
Na Mr. Purpose.

Nimekuwa nikifanya online business kuanzia mwaka 2018, ambapo nakumbuka nilikuwa nafanya application za vyuo, mkopo na usajili wa makampuni kupitia BRELA.

Huduma hizo nilianza nazo na nilikuwa na uwezo wa kuwahudumia wateja popote walipo Tanzania.

Haikuwa rahisi mwanzoni kwani ilibidi kutumia nguvu kubwa hasa katika kutafuta wateja kupitia mitandao ya kijamii ikiwemo Facebook ambayo ndiyo niliyotumia sana kuliko hizi platforms zingine kama whatsapp, instagram, twitter, LinkedIn pamoja na platform ya Jamii Forum.

Kuna changamoto nyingi ambazo nilikutana nazo mpaka kufikia hatua ya kupata wateja wa uhakika na wa kuaminiana.

Niseme tu kiukweli haikuwa rahisi hata kidogo hasa ukilinganisha na asilimia kubwa ya Watanzania kutokuielewa online business na kuamini pia kama ni kweli unaweza hudumiwa na kila kitu kikawa sawa.

CORONA ILIVYOSAIDIA KUKUZA ASILIMIA KUBWA ZA ONLINE BUSINESSES.

Baada ya msoto wote huo, kiukweli Corona, janga lililotikisa Dunia imeleta matokeo chanya kwetu sisi tuliokuwa tukifanya online business na mabadiliko makubwa tuliyaona ndani ya miezi michache ya uwepo wa Corona.

Hapo ndipo nilipopata idea ya kuanza kusambaza study materials

Niseme ukweli usamabazaji wa softcopy za hayo materials yalikuwa na mapinduzi makubwa sana na matokeo yalikuwa makubwa siyo siri (mpaka sasa).

KWANINI NIMEKUANDIKIA??

Wewe mfanya biashara ambaye unayo biashara yako, una frame security fulani ila biashara yako haipo online, aisee, UNAKOSEA SANA.

Kwanini unakosea??

Wateja wamehama mzee, kwasasa wapo Facebook, Whatsapp, Twitter, Instagram, yaani namaanisha, wapo mitandaoni, hasa hii mitandao ya kijamii.

Ebu fikiria kampuni kubwa zote kwasasa zinakuelekeza kuwasiliana nao kupitia mitandao ya kijamii kama whatsapp, instagram na Facebook. Nakupa mfano wa kampuni ya Vodacom, kwasasa huduma kwa wateja ukitaka kuongea nao ni mpaka instagram, Facebook au Whatsapp moja kwa moja.

Wao wanachokifanya wanakuwekea link tu na inakupeleka moja kwa moja hadi inbox yao, MA wanakujibu kwa wakati.

Unadhani kwanini wamehamia huko?

Kwasababu ulimwengu unabadilika hivyo lazima nao pia wabadilike kuendana na hali.

Mfanya biashara unamiliki kampuni au biashara ya kawaida halafu hata blog au pages kwenye mitandao ya kijamii biashara yako haipo, unasubiria wateja hapohapo ulipo , shtuka mzee utashangaa mwenzio anaongeza vitu tu na wateja wanajaa kwake uelewi wametoka wapi.

Kwa leo ngoja niishie hapa ila kumbuka wewe unayefanya biashara jinsi ambavyo miaka mitano huko nyuma ilikuwa ikifanyika mzee utaachwa na utashangaa mauzo yanashuka.

Baadhi y wasanii wa muziki nao wameshtuka wameanza kuuza Album zao kupitia mitandao ya kijamii, Nikki Mbishi kwa wale wanaomfahamu kazi zake ukihitaji ni mpaka kumfuatilia instagram nakumbuka interview yake aliyoifanya Clouds FM, jamaa ana madini sana na ndipo nikakugundua kumbe kuna wasanii ambao wapo vizuri kabisa upstairs.

Wapo wengi ambao kwasasa mtandao umekuwa ni sehemu kubwa ya kuwaingizia kipato kuliko hata jinsi ambavyo ofisi halisi zinaingiza.

Dada, Mama, Kaka, Baba na wote wengine kuna baadhi ya vitu havikuwepo Tanzania, ila tunakoelekea vinaenda kutawala, kuwa na jicho kuitazama fursa, usisubiri anza leo.

Mwisho, wale waalimu mnaofundisha online business halafu hata biashara ya online hamna hata moja, acheni kutoa vitu nadharia. Speak from your own experience (nitawaletea makala pia kuhusu hawa watu)

Pia kama utahitaji kutazama zaidi na kunifuatilia zaidi,

Bonyeza link hii

Karibu kwa ushauri kuhusu lolote NATOA BURE KABISA.

Muwe na asubuhi njema.

TUKUTANE SEHEMU YA PILI.............. .

Share na wengine pia.
 
Max Marketer

Member
Oct 13, 2020
47
125

Sent from my E2333 using JamiiForums mobile app
Congrats boss.. Waiting for part two.
 
Mr. Purpose

JF-Expert Member
Nov 12, 2016
1,063
2,000
Huu msemo kuna watu utawadumaza sana na sio kweli kwamba kila anayekuita kwenye fursa wewe ni fursa.

Akili za kuambiwa.....
Upo sahihi mkuu. Wengi muda wa kufikiria jambo kwa kina hawawezi hivyo kuishia kuchukulia mambo juujuu tu.
 
SN.BARRY

JF-Expert Member
Oct 12, 2012
3,318
2,000
Huu uzi hauna wachangiaji kwa kuwa hauzungumzii NGONO, watanzania wengi wanawaza ngono badala ya mambo ya maendeleo kama haya.
 
Toa taarifa ya maudhui yasiyofaa!

Kuna taarifa umeiona humu JamiiForums na haifai kubaki mtandaoni?
Fanya hivi...

Umesahau Password au akaunti yako?

Unapata ugumu kuikumbuka akaunti yako? Unakwama kuanzisha akaunti?
Contact us

Top Bottom